beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Spika Job Ndugai amesema Bunge la Tanzania linaahidi kutoa ushirikiano pale wanapohitajika akiongeza, watajitahidi kuhakikisha muhimili wa Mahakama unaheshimiwa ndani ya nje ya Bunge.
Ameeleza hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu Jijini Dodoma, ambapo miongoni mwa masuala mengine amesema, jukumu la Mahakama kutoa Haki ni zito na linahitaji hofu ya Mungu.
Aidha, amesema kuna mashauri mengi yanayoshughulikiwa na Viongozi wa chini bila kufika Mahakamani. Ameomba kundi hilo kusimamia na kuwatendea Haki Watanzania, akisisitiza adui mkubwa katika ngazi za chini ni Rushwa.