Ma-RAS wawe makini na Wakuu wa Shule wanaowateua sasa baada ya kutumbua majipu

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Ma-RAS wawe makini na Wakuu wa Shule wanaowateua sasa baada ya kutumbua [HASHTAG]#majipu[/HASHTAG].

Binafsi nipongeze utumbuaji wa baadhi ya wakuu wa shule za umma ambao walikufuru katika ubadhilifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka kwa muda mrefu.

Wakuu wa shule waliotumbuliwa kwa wizi wa fedha za Serikali, chain ya wizi huo inafanyika hadi kwa mkuu wa idara (afisa elimu), mkuu wa shule mwenyewe, makamu mkuu wa shule, mkuu wa taaluma, wakati mwingine hata mhasibu. Sasa kama mkuu wa shule katumbuliwa kwa wizi, halafu mmojawapo katika hiyo chain kateuliwa tena kuwa mkuu wa shule, ni sawa na kuhamisha mwizi toka shule x na kumpeleka shule y halafu tunarudi Kule Kule maana huyo mwizi anakuwa ana mafunzo toka kwa aliyekuwa mkuu wake na endapo tena mkuu wa idara akiwa ni yule yule. Ni vema kuangalia vizuri hiyo chain ya hayo majipu kabla ya uteuzi.
 
Back
Top Bottom