Isack Michael
Senior Member
- Jan 12, 2017
- 122
- 35
Kuna tatizo mkuu
Programming language ipi napaswa kuijuaHii mada ni deep zaidi ya unavyofikiria, kama upo interested mara mia ugoogle tu au kama unaweza programming vizuri ingia coursera(bure), udemy au udacity(za kulipia) chukua course ya AI, soma yote upate mwangaza. Ujue tu programming na most importantly Algebra na basic statistics.
Kua open minded tu, computer haziwezi kufikiria zenyewe pamoja na neno AI, ukigundua learning algorithms zinazotumika utagundua kua ni statistics tu, mara nyingi hua wanaexaggerate kwenye media kuhusu statenof AI.
Programming language ipi napaswa kuijua
Pitia humu unaweza pata mwangaza http://learn4feature.ga/courses/learn-artificial-intelligence-modelling-language/Ningependa kufahamu kwa undani zaidi juu ya AI asanten...
Nakumbuka juzi tu ulikuja humu na thread unataka kujua usome language gani, ulikua unasoma C. Uliishia wapi?Nimekuelewa mkuu kwaiyo unanishauri nisome kwanza AI au?
Asante sana mkuu nimekuelewa vizuri sana na nimependa maelezo yako kwakuwa ww ni mzoefu ungenishauri nisome language gani C++, PYTHON, JAVA etc?Nakumbuka juzi tu ulikuja humu na thread unataka kujua usome language gani, ulikua unasoma C. Uliishia wapi?
Mi nadhani unajaribu too much, yaani unataka kufanya vitu vingi kwa wakati moja, unasoma kimoja, haujafika pazuri unataka uanze kingine na kingine.
Kuna vitu vitamu kwenye computer leo hii ni general AI, kesho utataka self driving cars, kesho kutwa games, utakua unahama hama, sio kitu kibaya maana unatafuta ambacho utakipenda. Ila nahisi knowledge yako ya programming bado ni ndogo sana, pa kuanzia nakushauri soma kwanza data structure na algorithms, fanya mazoezi ya kutosha unaweza pitia hata ProjectEuler.net fanya maswali hata 50 ya kwanza kuzoea algorithms. Kwa datastructures jipe mazoezi mwenyewe kwa kutengeneza apps mbalimbali, mfano wa apps ambazo zinaweza kukuchallenge.
System ya buses, mfano una vituo 20, vipo connected, unataka kutoka kituo A kwenda D, utafute njia rahisi ya kufika from A to D alafu unamrudishia user, same concept inaapply kwenye subways e.t.c. Hapo utahitaji ujue graphs na graph traversal algorithms, kujua graphs utakua umesoma other data structures kama lists.
Fanya hivyo uzoee kwanza, rudi kusoma AI baada ya mwaka, sasa hivi utakimbia tu, nikwambie ukweli sio rahisi kama unavyofikiria, kama huna hizi basic concepts hutoweza kuhandle AI. Alafu achana na C tafuta general purpose language nyingine usome ambayo inatumika sana, C ni nzuri kwa kuanzia kujifunza basic concepts za programming, ila that's it, ikimbie kama hutokaa ufanye low level stuff.
Asante sana mkuu nimekuelewa vizuri sana na nimependa maelezo yako kwakuwa ww ni mzoefu ungenishauri nisome language gani C++, PYTHON, JAVA etc?
Kwa sasa nataka nianze na python cha msingi kwenye python ni kipi?Unataka desktop software au very intense software kama browsers, heavy kwenye calculations, games, then C++
Unataka enterprise software au mobile (Android) then soma Java
Unataka machine learning, Artificial intelligence? web servers then soma Python.
Mwisho wa siku utakaposoma language moja na ujue concepts za programming ni rahisi sana kusoma language mpya na kuanza kuitumia, nikupe mfano nilisoma Go ndani ya mwezi nikawa tayari nachangia github open source software written in go, swift wiki mbili nikawa nishaanza kutengeneza iOS apps with time unazoea na kujifunza new concepts, ila design patterns mara nyingi zinajirudia kwenye language nyingi.
Ushauri usikae unakariri syntax, utarudiarudia mara nyingi mwisho wa siku zitakaa zenyewe. Concentrate on the idea of solving the problem, don't concentrate on the tool.
Ukichagua language hapo, isome, jua basics zake, then stop, soma DataStructures kwa kutumia hiyo language, implement mwenyewe from scratch na ujue kwa nini zinatumika, mfano wa datastructures za muhimu kusoma
- Arrays
- Lists
- Maps
- Trees
*Binary Trees
*Heaps
*B trees
- Stacks
- Queues
- Graphs
Algorithms soma sanasana za sorting na searching. Zipo nyingine special purposes ila achana na hizo kwanza, you'll get to them later.
Ukimaliza hapo utakua na msingi, nadhani bila shaka utakua ushajua unataka ufanye nini next. Jaribu kukaa kiprogrammer sasa kama umeamua kweli, fuatilia kila siku, fungua google, youtube angalia videos kuhusu programming daily, watu wanafanya nini, some cool tricks. Learn learn, ila most importantly Practice Practice.
Kama baada ya miezi kama minne bado huna mwanga basi nitakushauri achana na hii field fanya kitu kingine.
The Python Tutorial — Python 3.6.2rc1 documentationKwa sasa nataka nianze na python cha msingi kwenye python ni kipi?