ma-migodi yanatusaidia nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ma-migodi yanatusaidia nini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .."Hivi haya ma-migodi yanatusaidia nini katika hili? Maana hizi ndiyo raslimali zetu na kila siku zinachimbwa zinaisha na sisi hatuoni faida yoyote ile katika maisha yetu...tusihoji? Itafika siku tutatukanwa na wajukuu zetu, watazifukua maiti zetu na kuzining'iniza huku wakilia kwa machungu. Maana tutakuwa tumeshindwa kuijenga nchi yao, tumeshindwa kuzilinda raslimali zao na wao wanahangaika hawana pa kushika! Kama sisi hatuko tayari kuvuna raslimali kwa faida kwa nini tusiwaachie wajukuu zetu labda watakuwa na uwezo zaidi yetu?

  sisi wananchi wa hali ya kawaida tunafaidika kweli na mapato yatokanayo na dhahabu??? Bwana Maganga mkulima ukimwambia leo uchumi umekuwa na mgodi uliopo jirani yake umechangia ukuaji huo, anakuelewa kweli? Huku hawezi kununua chumvi na kuweka kwenye mboga yake?.."


  Labda leo niongelee kidogo kuhusu ushirikishwaji wa wananchi kwenye shughuli za maendeleo zinazowahusu. Wananchi wa hawaoni faida ya mgodi kwao na wala kwa taifa lao, hawaoni mabadiliko yaliyoletwa na mgodi kwenye maisha yao - leo hii tunaongelea inflation kila mahali - hivi imesababishwa na nini? Mnielimishe hapa. Hivi haya ma-migodi yanatusaidia nini katika hili? Maana hizi ndiyo raslimali zetu na kila siku zinachimbwa zinaisha na sisi hatuoni faida yoyote ile katika maisha yetu...tusihoji? Itafika siku tutatukanwa na wajukuu zetu, watazifukua maiti zetu na kuzining'iniza huku wakilia kwa machungu. Maana tutakuwa tumeshindwa kuijenga nchi yao, tumeshindwa kuzilinda raslimali zao na wao wanahangaika hawana pa kushika! Kama sisi hatuko tayari kuvuna raslimali kwa faida kwa nini tusiwaachie wajukuu zetu labda watakuwa na uwezo zaidi yetu?


  sisi wananchi wa hali ya kawaida tunafaidika kweli na mapato yatokanayo na dhahabu??? Bwana Maganga mkulima ukimwambia leo uchumi umekuwa na mgodi uliopo jirani yake umechangia ukuaji huo, anakuelewa kweli? Huku hawezi kununua chumvi na kuweka kwenye mboga yake? bei imepanda...zamani wakati wa wachimbaji waodgo wadogo alikuwa anapata hata fursa ya kuuza mihogo yake na wali kwa wachimbaji na anapata hela ya kutosha. Watu leo hii wanawaunga mkono CDM kwenye maandamano si kwamba kweli wameichoka CCM na hawaoni kazi iliyofanyika, la hasha. wanaona na wanafaidi matunda ya maendeleo ya nchi yetu yaliyopatikana hadi leo, lakini wanaona maendeleo haya ya uchumi hayajitafisri kwenye mabadiliko ya hali zao za maisha ya kila siku...!


  imefika wakati watanzania wamekua hawana nguvu ya kufanya vibarua vya kupalilia nyasi? vya kufungua mageti? Hizi nazo ni kazi zinazohitaji weledi wa hali ya juu kabisa?wakenya kibao wanaajiliwa mpaka popo yaani wanigeria wanakuja kula bongo sasa sijui tunakwenda wapi
   
Loading...