wanajanvi heshima kwenu wakuu !!
Mkuu Radii, tulishatoa na tunaendelea kutoa ushauri kwa watu wenye mawazo mgando kama wewe, kujiunga JF siyo lazima uanzishe au uchangie kila mada ni bora ukabaki msomaji wa post za great thinkers zinaweza zikakusaidia kuelimika.
Ni dhahiri kwa ulicho kiandika hapo, wewe ni mmojawapo wa masalia unaye jitutumua kumuokoa Zitto, ilkhali Zitto mwenyewe kesha jutia makosa aliyo yafanya na kuomba msamaha.
Mkuu Radii, ni vyema ukatambue watanzania wa leo siyo wale miaka ya 1995s, wanajua kutofautisha ukweli na uongo, wanajua kuchambua mchele na pumba, kiu-fupi tu ni kwamba
hatudanganyiki.
Mkuu Radii ukumbuke mwisho wa siku hii dhambi ya kutumiwa kama condom itawatafuna nyie wenyewe na vizazi vyenu, mfano mzuri angalia kesi inayowakabili wale vijana waliotumiwa kufungua kesi dhidi ya Kamanda Lema, baada ya Lema kurejeshewa ubunge wake CCM imewaruka na sasa wanahaha wapi wapate mamilioni ya pesa wanayotakiwa kuyalipa kufidia gharama alizo zitumia Kamanda Lema.
Mkuu Radii, yakupasa uelewe watanzania siyo vipofu wanaona;
- Mnavyosafirisha Twiga wetu wakiwa hai kwenda ugaibuni.
- Mnavyoficha mabilioni yetu Uswis.
- Jinsi mfumuko wa bei unavyotutesa
- Mnavyotafuna fedha za walipa kodi.
- Mnavyoteua majaji wasiokuwa na sifa.
- Mlivyotuletea Richmond mpya ya ving'amuzi.
- mnavyo liingiza taifa kwenye mikataba tata ya madini.
- Polisi wanavyo ua raia wasiokuwa na hatia.
- Jinsi wanafunzi wa UDOM wanavyo jiuza kwa sababu serikali imeshindwa kuwapatia hela ya kujikimu.
- Mnavyotumia mabilioni ya pesa kutaka kuisambaratisha CHADEMA.
- Jinsi ambavyo hospital hakuna madawa.
- Jinsi watu wanavyo kufa kwa njaa huko Loliondo.
- Jinsi mgawo wa umeme unavyolitesa taifa hili.
- kupanda kwa gharama za umeme.
- kupanda kwa gharama za usafiri.
- kupanda kwa deni la taifa kufikia trilion 22.
- Mnavyowatumia mavuvuzela yenu ( Nape na Mwigulu) kuwakashfu viongozi wa CHADEMA.
- Jinsi Kinana anavyomaliza tembo wetu bila kuchukuliwa hatua.
- Mnavyozidi kutoa ahadi hewa.
- Jinsi gani M4C inavyozidi kuelimisha watanzania.
Mkuu hongera sana kwa post yako, hivyo basi nenda Lumumba ukapokee posho yako kwani ndo' kazi inayokuweka mjini, ila amini usiamini mwisho wa siku zitakutokea puani.
wana janvi naomba kuwasilisha.