M4C-OPD ndani ya Dodoma - Jan 27, 2014

M4C-OPD ndani ya Dodoma - Jan 27, 2014

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,178
Reaction score
162,653
Previously:

DODOMA DODOMA OPARESHENI PAMOJA DAIMA NDANI YA DODOMA KESHO.

karibu wakazi wa dodoma kesho katika viwanja vya barafu karibu na uwanja wa jamhuri stadium
makamanda watakuwa wanatoa elimu ya uraia,karibu sana.ukipata taarifa hii mweleze na mwenzako

by MICHAEL JUMA,SABASABA PHONE 0765129913

Habari wakuu,

Niko hapa Dodoma katika uwanja wa Barafu ambapo mkutano wa Operesheni Pamoja Daima umeshaanza.Hivi sasa ni viongozi wa ngazi wa ngazi za kata,wilaya na mkoa ndio wanaongea na kutupa matumaini kuwa viomgozi wa kitaifa watatua muda si mrefu.

Hata hivyo,mpaka muda huu saa 11:20 viongozi wanaosubiriwa kufika kwa "chopa" hawajafika na muda ndio unakwisha.Hakika hili ni kosa kwani wananchi wanasubiri kwa hamu viongozi hao wafike.

tHata hivyo,tunambiwa mafuta ya "chopa" yalicheleweshwa kwa dakika 15.Tunavuta subira.Uzuri hali ya hewa ni nzuri na watu wametulia wakisubiri viongozi wafike.

Makamanda wanaosubiriwa ni mh.Lissu na kamanda Heche.

Update:Muda huu ikiwa ni saa 11: 28 "chopa" ndio inazunguka angani ikitaka kutua.Watu wanashangila.

Kamanda Heche anasema CCM wameondoa mawaziri mizigo na badala yake wameleta mawaziri "vifurushi".

Kuhusu CCM kubeza wao kutumia chopa,mh.Heche anahoji kwani wao CHADEMA wanatumia hela za walipa kodi au wanatumia hela za CCM kurusha chopa hizo?!Mh.Heche kaonya kuwa endapo CCM watachakachua katiba mpya basi CHADEMA watarusha chopa 10 kuelimsha umma kuikataa katiba hiyo.

Kauli za mh.Lissu
Lowassa anatoa fedha makanisani huku akisema sasa ni zamu yetu kwani Kikwete wa sasa ni muislamu.

Lissu anasema serikali inawaibia polisi kwani wakiajirirwa wanaanza na mkataba wa miaka 3 na kisha wanaongezewa mkataba mwingine wa miaka 3 na tena wanapewa mkataba mwingine wa miaka 3 na mwisho wanapewa mkataba wa mwisho wa miaka 3 hivyo wanakuwa wamefanya kazi kwa mkataba kwa jumla ya miaka 12.Kwa maana hiyo polisi akistaafu,kwa mfano akiwa amefanya kazi kwa muda wa miaka 30 atalipwa mafao yamiaka 18 kwani ile miaka 12 ya mwanzo inakuwa imepotea.

Mh.Lissu kasema katika mazingira hayo ndio maana mtu ukipelekwa polisi,unapigwa kama umeua kumbe polisi wanakuwa na hasira za kuchakachuchuliwa na hivyo wanamalizia hasira kwako.

Mh.Lissu ameongelea kuhusu kero za muungano na akasema sasa hivi mtu kujiita ni mtanzania ni kujidanganya kwani kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na katiba ya muungano,hakuna tena nchi inayoitwa Tanzania.Lissu kasema ma-CCM yameshavunja muungano na akasema wazanzibari wanalazimishwa tu.

Kuhusi kuwa na amiri jeshi wawili,mh.Lissu amehoji itakuwaje siku maraisi hawa wakipishana kauli?Mh.Lissu kasema vikosi vya zanzibar chini ya raisi wa Zanzibar ni kwa ajili ya kupigana na vikosi vya JWTZ siku mambo yakiharibika

Jamano watu ni wengi sana na inatia moyo kwakweli.
 
Hongereni fanyeni kazi dodoma bado tuna hitaji ukombozi.


Maeneo ya mvumi,mlowa barabarani,chamwino ,bahi,mpwayumgu ,mpwapwa na kwingineko!

Pipozzzzzzzzzzzzzzzz
 
Kumekucha,Kamanda wa anga badilisha mawani vaa meupe hayo meusi yanatisha.Piipoozz!!
 
wafike hadi alipo job ndugai na juma nkamia ( mzee wa lugha chafu )
 
Dahhh!!!! Jamani Chadema punguzeni kunipa raha....

M4C-OPD with no apology..
 
CHAMA CHA SIASA ni MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .
 
Hongera wana idodomya! Chadema nendeni kondoa, mpwapwa, kongwa na maeneo mengine ya dodoma! Dodoma kuna umasikini wa kutisha sana! Chadema toeni elimu ya uraia hapo dodoma!
 
Ewaaaa! Ndo muda mwafaka wa kuwazindua wana idodomia! Toa muda tafadhal
 
NARCO, KIBAIGWA,CHALINZE Moja........ Piga Chini *******:car:
 
Nadhani watakuwa hawajatenda haki kama hawatapiga mikutano Kongwa na kibaigwa kwenye jimbo na Ndugugay, Kisha miwili kwenye jimbo la Mkaamia! Kisha Kibakwe kwa Simbachawene!
Baada ya hapo wanaweza kwenda!
Pamoja Daima!
 
Back
Top Bottom