Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
Nikiwa Mzaliwa wa Jimbo la Bumbuli, nashangaa ni kwa nini CHADEMA na M4C hawajafika Bumbuli. Bumbuli ni moja ya majimbo yaliyo nyuma sana kimaendeleo, lakini nashangaa CHADEMA wanazunguka nchi bila kukumbuka jimbo letu.
Kumbukeni 2010, tulinyimwa haki yetu ya msingi ya kumpigia kura mbunge wetu, matokeo yake tukapewa mbunge wa vyombo vya habari na ahadi kemkem. Mara kapanda bajaji, mara kaanzisha mradi wa mendeleo, mara mpinga ufisadi kwenye magazeti ulaya wakati sisi hayo maendeleo hatuyajui.
Huyu wetu mbunge sharobaro akipita kijijini kwetu anajifanya amelala kwenye gari ili vijana tusimuone.Ndo hayo mambo ya kurithishana madaraka. CHADEMA fanyeni kweli njooni jimboni. Bumbuli hata mkisimamisha Jiwe litapita ila siyo mwana CCM.
Bumbuli tumemmiss mzee Shelukindo.