M4C (Hurricane) yatikisa ndani ya Mkutano Mkuu CCM

M4C (Hurricane) yatikisa ndani ya Mkutano Mkuu CCM

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
26,011
Reaction score
25,351
CCM : Yatangaza mkakati kukabili kasi ya M4C

CHAMa cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetawala mjadala wa mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Mapinduzi (CCM), unaofanyika mjini hapa.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, mawaziri wa pande zote mbili za Muungano, viongozi wengine na baadhi ya wajumbe waliopata nafasi ya kuzungumza, walikuwa wakiilalamikia CHADEMA kwamba inaeneza uongo dhidi ya CCM. Ingawa wazungumzaji wote, hawakutaja moja kwa moja jina la chama lengwa, ni dhahiri kwamba waliilenga CHADEMA, chama pekee kinachofanya ziara nyingi mikoani kupitia operesheni zake za Sangara na sasa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Aliyeibua mjadala wa CHADEMA kwenye mkutano mkuu huo wa CCM, alikuwa mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda, ambaye alialikwa kama mwakilishi wa Mpango wa Kujitathmini Kimaendeleo Afrika (APRM). Shibuda akizungumza katika mkutano huo, aliishangaa CCM kwa kukaa kimya wakati CHADEMA inazunguka nchi nzima kuishambulia kwamba haifanya kitu.

Alisema ni makosa ya CCM kwani wajumbe hawafanyi mikutano ya hadhara kujibu mapigo ya CHADEMA. "Mnasubiri viongozi wakija toka makao makuu ndipo mnajibu wakati wapinzani wanafanya mikutano, wananchi wanabaki na mihemko...na mnajua mtu akisema uongo mara saba wa sabini huwa ukweli...," alisema Shibuda.

Huku akitumia misamiati migumu kama kawaida yake, Shibuda aliiambia CCM kuwa ndiyo daktari na wapinzani na maradhi, hivyo kila yanapotokea maradhi ni wajibu wao kuyatibu.

Kauli hiyo ya Shibuda ni kama iliiamsha usingizini CCM kwani Mwenyekiti wake, Rais Kikwete, mara kwa mara alirejea kauli ya Shibuda na kuwataka wajumbe waamke kujibu mapigo mara moja.

Rais Kikwete aliwataka wajumbe kutumia taarifa za utekelezaji zilizowasilishwa na baadhi ya mawaziri, kuwaeleza wananchi mambo yanayofanywa na CCM katika kutekeleza wajibu wao.

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, aliwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo iliainisha gharama, mahala ilipo na kasi ya ujenzi inavyoendelea.

Alieleza kuwa ujenzi wa daraja la Kigamboni, ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, barabara za juu katika eneo la Tazara na miradi mingine ya ujenzi iko katika mikoa mingine nchini.

Baada ya kuwasilisha taarifa hizo, wajumbe walikusanyika katika makundi kuzijadili ambapo sehemu kubwa ya majadiliano, CHADEMA iliendelea kuwa gumzo kwa wajumbe.

Vikundi hivyo jana viliwasilisha taarifa za majadiliano hayo na kuwaeleza wajumbe namna ya kuzitumia kujibu mapigo ya CHADEMA.

Akieleza namna ya kufikisha taarifa hizo kwa wananchi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alieleza njia tatu za kufikisha ujumbe huo ili wananchi wajue ukweli.

Njia ya kwanza alisema ni kupitia vyombo vya habari vya chama na serikali, pili kuziweka kwenye CD, kutengenezea majirida maalumu kwa lengo la kufikisha taarifa hizo kwa wananchi.

Awali Pinda aliwasilisha taarifa ya serikali ya utekelezaji wa Ilani ya chama wakati Katibu Mkuu, Willson Mukama, aliwasilisha taarifa ya CCM.


Source: Tanzania daima
 
Nyie ccm hayo mnayosema hamuwezi kuyatekeleza kwani wenyewe kwa wenyewe hampendani na kila mtu ana uchu wa madaraka. mmeshapoteza misingi ya chama chenu na hamuwezi kurudia misingi ya awali kwani wanaoongoza chama hawajui misingi wala falsasa ya ccm zaidi ya kila mtu kutafuta upenyo wa kujineemesha. Mnadhani hao wafanyabiashara waliomo ndani ya chama na kuwa wafadhili wakuu wa chama wanatafuta nini zaidi ya faida na maslahi yao binafsi. Kuna mkulima au mfanyakazi anayeweza kupata madaraka hata ya kati katika chama chenu? Subirini tu kifo chenu 2015. nyie ni sikio la kufa halisikii dawa. Kila mtu ana ndevu kama kambare katika ccm. CCM BYE BYE. Endeleeni kupumulia mashine hadi hapo 2015. Lakini yote mmeyataka wenyewe. Mlidhani nyinyi ndio kila kitu nchi hii na mnaweza fanya lolote. POLENI SANA. SISI TULIWAPENDA LAKINI MABADILIKO YAMEWAPENDA ZAIDI.
 
Back
Top Bottom