M23 wadaiwa kubaka na kuua DRC

M23 wadaiwa kubaka na kuua DRC

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
130606180115_drc_m23_304x171_afp_nocredit.jpg


Baada ya kuwahoji zaidi ya watu 100, Human Rights Watch lilisema kuwa waasi hao pia wanawasajili kwa nguvu vijana DRC na wengine kutoka Rwanda.

130715165324_drc_fighting_304x171_reuters_nocredit.jpg


Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi la wapiganaji la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrsia ya Congo limewaua zaidi ya watu arobaini na kuwabaka zaidi ya wanawake na wasichana sitini tangu Machi mwaka huu.
Baada ya kuwahoji zaidi ya watu mia moja eneo hilo, shirika hilo lilisema kuwa waasi hao wanawasajili kwa nguvu vijana huko DRC na wengine kutoka nchi jirani ya Rwanda.
Kundi hilo limeongeza kuwa Jeshi la Rwanda bado linawasadia moja kwamoja waasi hao licha ya serikali ya Kigali kupinga hilo mara kwa mara.
Wakati huohuo, jeshi la DRC hapo jana lilishambulia ngome za waasi hao karibu na mji wa Goma Mashariki mwa DRC.
Haya yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu vita kati ya pande hizo mbili kuanza Jumatatu asubuhi na kusitishwa siku hiyo mchana.
Kundi hilo limesema liko umbali wa kilomita nne kutoka mji wa Goma, ingawa limesema lengo lake ni kulazimisha serikali kufanya mazungumzo nao wala sio kuteka mji wa Goma.
M23 liliuteka mji wa Goma, kwa siku kumi mwezi Novemba kabla ya kuondoka mjini humo kufuatia shinikizo za jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na serikali ya rais Joseph Kabila.
Mazungumzo na serikali yalianza mjini Kampala mwezi Disemba ingawa baada ya miezi miwili jeshi likaanza tena mapigano na waasi hao mwezi Julai tarehe 14.
Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano hayo yamesababisha takriban watu 4,200 kutoroka makwao

© 2013 BBC
 
Japokuwa siwaungi mkono M23 naona hii thread lengo lake ni ku-neutralize aibu waliyopata majeshi ya DRC kwa sababu ya kudhalilisha maiti za waasi wa M23.
 
Human rights watch are just fraud scammers,and Mokala is another clueless idiot!!
 
Human rights watch are just fraud scammers,and Mokala is another clueless idiot!!

idiot ni wewe unayekimbia nchi yako kisa inaongozwa kidhalimu na kwenda kuolewa USA! BILA AIBU UNAENDELEA KUUTETEA UHALIFU WA KAGAME,!
 
idiot ni wewe unayekimbia nchi yako kisa inaongozwa kidhalimu na kwenda kuolewa USA! BILA AIBU UNAENDELEA KUUTETEA UHALIFU WA KAGAME,!
Ha aahaha ahahah eti nimekimbia,you don't know me like that na wahalifu ni nyie na akili zenu za interahamwe and Kagame is my HERO!!!
 
Hii ni hatari. Kama wanajeshi wa serikali ya DR Congo ndo wanaofanya hivi nafikiri tunapoteza nguvu ya wanajeshi wetu.
Jeshi letu itabidi liwe na kazi ya kuhakikisha kuna jeshi jipya DRC maana hili si jeshi tena. Jeshi la serikali ndo linakuwa unpopular!
 
Hii ni hatari. Kama wanajeshi wa serikali ya DR Congo ndo wanaofanya hivi nafikiri tunapoteza nguvu ya wanajeshi wetu.
Jeshi letu itabidi liwe na kazi ya kuhakikisha kuna jeshi jipya DRC maana hili si jeshi tena. Jeshi la serikali ndo linakuwa unpopular!


watu wengi ndani ya hii JF wana habari nusu nusu au hawana muda wa kuchambua kwa undani na pengine kuna watu humu kwa sababu zao wanaanzisha topic kwa malengo maalum kisha sote tunadandia hilo basi.
 
kama dikteta kagame asingeiundia DRC kikundi cha waasi kwa tamaa zake za uporaji yote yasingetokea, bado wakulaumiwa ni huyu muuaji, nduli, kizazi cha kaini, fashisti kagame! mungu tusaidie tuondokane na joka hili lenye sumu kali.

Man did you open da link and follow the story? it is an International broadcasting agency. Is you are response while quoting my post relevant to what is in da Clip? I think we should be arguing point against point in this forum or at-least is what I was lead to believe in various forums where I am a member, am new here but arguments are not answered accordingly I don't know if the Mod. here is comfortable with such trend
 
Ha aahaha ahahah eti nimekimbia,you don't know me like that na wahalifu ni nyie na akili zenu za interahamwe and Kagame is my HERO!!!

We all knw kagame is your hero because you all have the same interahamwe and m23 ideology of exterminating one another
 
M 23 ni katili sana haitakiwi wafumbiwe macho kabisa
 
Back
Top Bottom