Hiyo tisa kumi ni hii..mimi ni wakala wa Mpesa..jana kuna mtu kaja kutoa 350,000 sms ya Mpesa ikaingia na nikaangalia salio limeongezeka..nikampa pesa na nikaandika huo muhamala kwenye kitabu.. salio langu likawa ni 400000 maana kabla ya muhamala wa mwisho nilikua na 50000..nilipotoa hizo 350,000 nikawa na salio la 400,000.baada ya muda alipokuja mtu nimtumie 300000 nikashangaa naambiwa sina salio..kucheki salio nakuta ipo 50,000.nimewapigia voda wanasema hiyo no. Iliyotoa hela ilifungiwa isitoe hela toka siku nyingi na hawakua na kingine cha kuniambia..swali langu imekuaje no. Iliyofungiwa imeweza kutoa no. Na sms ya Mpesa kuja kwangu wakala??kuna mchezo hapa