hatusikii mengine? selelii selelii! who is selelii by the way? am fed up with kila siku selelii selelii hamna cha kuandika!
Hivi RA ndo anayewapangia wananchi wa nzega na Tabora kwa ujumla wawakilishi wao??
Iam fed up.
Kabonde sijaropoka ila nimeuliza kwa nini nguvu yake ni kubwa mpaka kwa wananchi??
Nyauba wewe uko dunia ipi ??????????????,yaani mpaka leo humjui king maker wa Tanzania.Wakati mwingine kukaa kimya ni busara zaidi kuliko kukimbilia kuropoka na hatimae ujinga wako unajulikana kwa umma wote.
Kabonde sijaropoka ila nimeuliza kwa nini nguvu yake ni kubwa mpaka kwa wananchi??
Najua nguvu yake ya kutengeneza mtandao wa kuweka watu madarakani kwa kutumia vikundi au kikundi ndani ya chama chake ila hadi kwa wananchi sikuwaa naamini nguvu hiyoo!!!
Anaweza kuweka kibaraka wake na bado wananchi wakamtosa kwa kura..
Au wananchi huchagua chama na si mgombea bora?
Katika kile kinachoonekana kuchafuka kwa hali ya hewa mkoani Tabora, jana jioni kwenye kikao cha wazee, mkiti wa ccm mkoa wa Tabora Hasan wakasuvi alimpigia debe la wazi Ndg Lucas selelii bila woga wala kificho na kwa kujua kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya uongozi wa ccm. sakata lenyewe lilianza hivi, baada ya kukaribishwa na katibu wa ccm mkoa bwana Ame ambaye ni muunguja, mkiti alianza kwa mkwala mzito kuwa baadhi ya watendaji wa ccm wilayani nzega wanapigia debe wagombea ubunge watarajiwa mbali na mbunge aliyepo madarakani na kuwaambia kuwa kama watendaji wanaetakiwa kumpigia debe ni selelii peke yake na si vinginevyo kwani ndiye mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi kadhaa hivyo hakuna sababu ya kubadilisha mbunge! wakasuvi aliendelea kusema kuwa endapo atathibitisha kuwa bado watendaji wanambeba selelii basi atahakikisha kuwa wagombea hao wanakatwa majina
Taarifa zaidi zinadai kuwa Mkiti huyo wa mkoa anampigia debe selelii ili nae aje amsaidie kwenye uchaguzi mkuu ujao wa ccm ili aendelee kuwa mkiti kwani wagombea watarajiwa wote wanaojitokeza wanaelekea kutomuunga mkono mkiti huyo kwa kuonekana mtu wa visasi sana
poleni wana Nzega! ongezeni bidii, ndio kumekucha kwani kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.
Kibonde! najua utakuwa unanifahamu vizuri lakini nikuweke wazi jambo moja unapofika wakati wa uchaguzi kila raia anakuwa free kumpigia kura yeyote anayemtaka regardless hafai kiasi gani!
Huyo selelii ambaye wewe umesema kuwa wamtaka sisi watu wa nzega hatuhitaji hata kusikia jina lake, ametukwamisha swala la umeme hasa kwa kiji cha Ndala na puge kwa upuuzi wake, bara bara ya Tabora Nzega haifai kabisa lakini kibaya zaidi elimu yake kwa karne hii haistahili hata kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa achana na udiwani wala ubunge. umenipata
Heshima kwako M-bongo,
Naomba kukuuliza swali dogo sana hivi kina Mtemi Mkwawa,Mirambo na kina Mangi sina walikuwa na elimu gani ?.Mzee wa vijicent ana degree ya sheria from Havard university ebu ona madudu aliyotufanyia Wadanganyika,mikataba yote ya madini ilipita chini yake,ununuzi wa rada na mambo mengi machafu kashiriki.
Jaribu kucheck web ya bunge anagalia CV za waheshimiwa wabunge utashangaa jinsi walivyo na vyeti vizito lakini uwakilishi wao ni tofauti na usomi wao.
M-bongo vipi au wewe uko kwenye kamati ya yule msomali anayenyemelea jimbo la mpigananiji wetu.
Seleli ni miongoni mwa wabunge tuonawataka warudi tena mjengoni,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora kafanya jambo zuri sana kumpigia debe Lucas Seleli.Najua zipo juhudi kubwa zinazofanywa na kundi la mafisadi za kumpeleka yule kibaraka wa Rostam Azizz mjengoni lakini safari hii hakuna wa kumdanyanya.