Katika kile kinachoonekana kuchafuka kwa hali ya hewa mkoani Tabora, jana jioni kwenye kikao cha wazee, mkiti wa ccm mkoa wa Tabora Hasan wakasuvi alimpigia debe la wazi Ndg Lucas selelii bila woga wala kificho na kwa kujua kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya uongozi wa ccm. sakata lenyewe lilianza hivi, baada ya kukaribishwa na katibu wa ccm mkoa bwana Ame ambaye ni muunguja, mkiti alianza kwa mkwala mzito kuwa baadhi ya watendaji wa ccm wilayani nzega wanapigia debe wagombea ubunge watarajiwa mbali na mbunge aliyepo madarakani na kuwaambia kuwa kama watendaji wanaetakiwa kumpigia debe ni selelii peke yake na si vinginevyo kwani ndiye mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi kadhaa hivyo hakuna sababu ya kubadilisha mbunge! wakasuvi aliendelea kusema kuwa endapo atathibitisha kuwa bado watendaji wanambeba selelii basi atahakikisha kuwa wagombea hao wanakatwa majina
Taarifa zaidi zinadai kuwa Mkiti huyo wa mkoa anampigia debe selelii ili nae aje amsaidie kwenye uchaguzi mkuu ujao wa ccm ili aendelee kuwa mkiti kwani wagombea watarajiwa wote wanaojitokeza wanaelekea kutomuunga mkono mkiti huyo kwa kuonekana mtu wa visasi sana
poleni wana Nzega! ongezeni bidii, ndio kumekucha kwani kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.