Lyimo: Huwezi kuwa tajiri kwa kulima dawa za kulevya

Lyimo: Huwezi kuwa tajiri kwa kulima dawa za kulevya

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema hakubaliani na dhana kwamba taifa linaweza kutajirika kwa kulima dawa za kulevya. Amesema mitazamo hiyo haina mashiko kwani inaleta madhara makubwa kijamii, kiafya na kiusalama kwa wananchi.

Soma pia: Aretas Lyimo: Tanzania inaongoza udhibiti wa dawa za kulevya


Amefafanua kuwa taifa lina mazao mengi ya kibiashara yenye tija ambayo yanaweza kukuza uchumi bila kuathiri afya za watu na mustakabali wa vijana. Kwa mujibu wake, juhudi za kuwekeza katika mazao halali na kuimarisha uzalishaji zitachangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya taifa kuliko kulinda biashara haramu ya dawa za kulevya.
 
Huu ni uongo bana. Mbona mataifa yanatajirika kwa kulima kahawa! Wanaolima shayiri au zabibu kwa ajili ya kutengeneza bia si wapo humo? Wanaolima Coca wanapesa nzuri tu.
 
Kamishina hana logic kabisa, anatetea ugali wake tu bila kuweka facts na ukweli mezani.
Hawani matajiri wa bangi
1. Bruce Linton
2. Andrew Modlin
3. John Cervini
4. Steve DeAngelo
5. Irwin Simon
 
Ruba 1 ya mrungi Daslam ni shillingi 50, gunia 1 la mahindi Daslam ni shillingi elfu 60.
Ruba 1 unaiweka ndani ya mfuko wa jeans.

Debe 1 la bangi Daslam ni shillingi laki 2.
Debe 1 la mahindi Daslam ni shillingi elfu12.

Hata sijui kwanini naotaga ndoto mbaya hivi, God forbid
 
Back
Top Bottom