Lwenge alalamikiwa kumbeba Mangula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwenge alalamikiwa kumbeba Mangula

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 24, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati vikao ngazi ya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vikiendelea mjini Dodoma kuchuja majina ya wagombea, Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, ametupiwa tuhuma kuwa anambeba Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho, Philip Mangula anayewania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya kupitia Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa Njombe.

  Endapo Mangula jina lake litarejeshwa na vikao vya chama atapambana na wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ambao ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Magharibi, Yono Kevela, Julieth Kadodo na Mechard Msigwa.

  Habari kutoka mkoa wa Njombe zinadai kuwa, mvutano mkali umeibuka katika wilaya ya Wanging’ombe, huku Lwenge katika kile kinachoelezwa ni kuwathibiti baadhi ya wagombea ambao hawaungi mkono anadaiwa amekuwa akizuia shughuli zozote za uchangiaji katika kata za jimbo la Njombe Magharibi kwa madai kuwa zinaandaliwa ili kuwapigia kampeni wagombea fulani.

  “Mhe. Gerson Lwenge amepiga marufuku harambe ya kuchangia kata ya Luduga ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Yono Kevela, harambee hiyo ilipangwa kufanyika Septemba 8 mwaka huu na maandalizi yalikuwa yamekamilika,” alisema kiongozi mmoja wa CCM ngazi ya wilaya.

  Alidai kwamba tangu wagombea wachukue fomu za kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC, siasa chafu zimekuwa zikijitokeza katika wilaya hiyo, baadhi ya wagombea wanajinadi kwamba wametumwa na viongozi wa CCM Taifa ili wapewe majukumu makubwa zaidi ndani ya chama baadaye.

  Akijibu tuhuma hizo dhidi yake, Lwenge akizungumza na NIPASHE kwa simu alisema shutuma zinazoelekezwa kwake hazina ukweli akisema wanaomzushia mambo hayo ni mahasimu wake wa kisiasa.

  “Mimi sigombei nafasi yeyote ndani ya chama, kwani wajumbe wa NEC wanagombea ubunge hadi nianze kununua watu wa kumpigia kampeni Mangula,” alisema Lwenge.

  Lwenge ambaye ni Mbunge wa Njombe Magharibi, alisema siyo sahihi kuanza kumlalamikia katika mambo ambayo hayana ukweli na kwamba wanaofanya hivyo kama wana ushahidi walalamike kwenye vikao vya chama .

  Kuhusu madai ya kupiga marufuku harambee katika kata ya Luduga, alisema yeye ni Mbunge wa Njombe Magharibi hivyo jambo lolote la kuchangia maendeleo anapaswa kujulishwa ili naye aweze kushiriki.

  “Suala la maendeleo ni muhimu sana lakini haiwezekani mtu aje afanye harambee kwenye jimbo langu ambalo mimi ni mbunge halafu sifahamishwi, hiyo siyo sahihi,” alisema Lwenge.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mangula anatafuta nini kwenye frontline politics wakati wazee wenziwe wanang'atuka? Ana nini zaidi ya siasa za kizamani za kisoviet?
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Bado yumo tu....Mangula anatafuta kufa kwa pressure tu yaani kutoka Katibu Mkuu mpaka kugombea kupitia Wilaya! Mbona mwenzie Makamba ametulia? Kuhusu Lwenge nadhani huyu ni miongoni mwa wabunge wa hovyo kabisa kuwahi kutokea katika Wilaya ya Njombe
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  naona wastaafu wanatafuta uwakilishi.bila shaka ni kujijenga upya kwa wastaafu.wameona warudi tena.nadhani ni kundi la akina mh.sumaye...
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ameona kazi ya kilimo hailipi?!
   
 6. Miaghay

  Miaghay JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hii mijianasiasa saa ingine inakera sana.
   
Loading...