Tutegemee nini basi, kwa wale waliozaliwa kati ya tarehe 13 juni hadi 20, na desemba 13 hadi 20 wakae chonjo kwani wana miaka saba ya machungu. Pia kwa wale wenye sayari ktk nyuzi hizi 20-28 Mapacha na Mshale (ikiwemo nchi yetu). Kubwa zaidi kutakuwa na ugunduzi mkubwa wa habari za uongo ambazo zilikuwa zikijulika kama za kweli, hii inaweza kuleta mtafaruku. Kwa kuwa Mars ndiye atakuwa bwana wa kupatwa huku ambako nako kunatokea ktk nyota ya moto - mshale; kwa hiyo machafuko, vifo vya jumla, mioto, vitegemewe sana. Uzuri mmoja ni kuwa Mars akiwa ndiye bwana wa kupatwa ataonyesha na njia ya kutokea pia ktk matatizo hayo.