Lukuvi+sugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi+sugu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHEMPO, Jul 18, 2012.

 1. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sugutuambie lukuvi alikuwa anakuambia nn..anakutisha?au wanataka ukashiriki kwenye muvy inayofanyiwa marekebisho na kova......
   
 2. d

  decruca JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Anamwambi nini wapi? hebu iweke vzr.
   
 3. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimemwona lukuvi akiwa amemfwata sugu mahali alipokaa bungeni,kipindi ambacho mbunge machemli alipokuwa anatoa maoni juu ya wizara ya mambo ya ndani...hivyo nilikuwa najaribu kujua je?lukuvi alikuwa anaongea nn na sugu..maana sugu alikuwa anaonekana kuongea kwa hisia kwa kutumia mikono kama ilivyo kawaida yake..
   
 4. d

  decruca JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mhh! hapo kuna jambo.
   
 5. M

  Magesi JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siasa s uadui mkuu
   
 6. B

  Blessing JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  SUGU usiogope kabisa hata kama wanakutisha. Ni nyanya mbovu usichanganye nao otherwise utaabukizwa alafu utakua umeoza. Kweli tumekusikia jana SUGU na hawa Serikali na Wakuu wasifike kabisa. SUGU KAA KISUGU
   
 7. L

  Lekakui JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,411
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Na Joyce Mmasi
  WAKATI mwingine namwonea huruma Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye amegeuka na kuwa mwalimu au kiranja kwa kuwaonya mara kwa mara watu wazi ambao wabunge.

  Spika amekuwa akifanya hivyo mara nyingi, kutokana na wabunge wengi kuonekana wanakwenda kinyume na kanuni, sheria na taratibu za bunge.

  Hivi karibuni, Makinda alieleza kuchoshwa na tabia za baadhi ya wabunge na kulazimika kutamka hadharani kuwa amechoshwa na utoro.

  Makinda alikwenda mbali zaidi na kuwakumbusha kuwa ruhusa zote za wabunge kuondoka Dodoma zitatolewa na Spika badala ya Ofisi ya Waziri Mkuu kama ilivyokuwa awali.

  Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa na tabia ya kukwepa vikao na kuutumia muda wa kuwawakilisha wananchi kufanya mambo yao binafsi.

  Tabia hii ya baadhi ya wabunge ni mbaya na inatia aibu, inalidhalilisha chombo hicho na zaidi inawaondolea heshima watu hao wanaopenda kuitwa waheshimiwa.

  Limekuwa jambo la kawaida kuona viti vitupu bungeni kila siku hasa nyakati za jioni. Bahati nzuri Bunge linaonyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni, hivyo wananchi ndani na nje ya nchi, wanawaona wabunge wachache wanaendelea na vikao huku walio wengi, wakiwa hawajulikani waliko.

  Jambo baya pengine kuliko yote ni kitendo cha wengi wao kukwepa vikao hivyo bila ya kutoa taarifa yoyote kwa Spika, jambo ambalo ni utovu ni nidhamu, na na kupuuza kanuni zinazosimamia Bunge.

  Nasema hawatoi taarifa kwa kuwa, malalamiko ya wiki iliyopita ya Spika yanadhihirisha hivyo. Siamini Spika angeweza kulalamikia waziwazi na kwa uchungu utoro wa wabunge wakati anakuwa ametoa ruksa kwa wabunge wasiohudhuria vikao.

  Wengi wa wabunge huonekana nje ya mji wa Dodoma kama vile Dar es Salaam, wakiendelea na shughuli zao binafsi au za vyama vyao, na kupuuza kile kinachoendelea katika kikao hicho muhimu, hasa Mkutano wa Bajeti.

  Katika kipindi hiki, Bajeti za Serikali katika wizara mbalimbali zinawasilishwa kwa 2012-2013, Serikai inaeleza mikakati yake ya maendeleo na kujibu hoja za wabunge, lakini baadhi ya wabunge wanatoroka, na kuwakosesha fursa muhimu wapiga kura wao.

  Naamini katika mkutano huu, wabunge walipaswa kujadili, kukosoa na kutengeneza mipango kupata Bajeti za Wizara zitakazoweza kulivusha taifa katika mwaka ujao wa fedha na kuwanufaisha watu wa majimbo yao na taifa kwa ujumla.

  Kwa maneno rahisi ni kwamba umakini na michango ya wabunge ndiyo pekee inayotarajiwa kusaidia kupatikana Bajeti bora na ambayo italinufaisha taifa na wakati huo huo kuwaacha wananchi wakiwa na fursa ya kumudu maisha yao.

  Katika mkutano huu wa Bunge wabunge kwa ujumla wao, wangetarajiwa kuonyesha umakini katika kujadili hoja, kuibua mambo yaliyofichika na kukemea mambo machafu yanayoonekana kuhatarisha maslahi ya taifa.

  Hii ndilo jukumu la mbunge yeyote, kumwakilisha wananchi na kuwatetea, kuwasemea na kupigania maslahi yao, , lakini kazi hiyo wameachiwa wachache na wengine wanamshangaza hata Spika, kwa kufanya mambo binafsi wakati wa vikao.

  Katika Bunge la Bajeti lililopita, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo alituhumiwa kwa kuhonga baadhi ya wabunge ili kupitisha Bajeti ya wizara yake na suala hilo bado limeachwa kiporo, na hakuna mbunge anayeliulizia.

  Hapa ndipo linapokuja suala la wabunge wetu kuwa makini na kweli kuwa wawakilishi wazuri wa wapigakura na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa, badala ya mtindo wa sasa wa kupoteza muda kulumbana bila hoja na kushabikia matukio zaidi.

  Kwa kumbukumbu za matukio kama haya, wabunge ndipo wanapotakiwa kuwa makini katika kuibua, kukemea, kuzuia na kupigia kelele mambo yasiyo ya kiadilifu.

  Wabunge kama wawakilishi wetu wasijisahau badala yake wakumbuke kuwa wanatakiwa kuamka usingizini na kuanza kutimiza wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi waliowapa dhamana, na wananchi waone kuwa kweli wanawakilishwa.

  Inafaa wabadili mtindo wa kutumia kipindi cha Bunge kufanya kazi binafsi, badala yake wakumbuke kuwa kipindi hiki wanapaswa kuwa bungeni wakisikiliza na kutoa michango yenye tija, ambayo italeta mabadiliko katika mfumo wa kiutawala.

  Ikumbukwe kuwa uchache wa wabunge ndani ya Bunge, hutoa mwanya kwa baadhi ya hoja au mipango isiyomnufaisha mwananchi ikipita, hivyo kuondoa matumaini kwa waliowachagua.

  Mbali na suala la utoro kwa wabunge, yapo matukio mengine yanayokera ya ushabiki wa wabunge, ambao unawafanya wasahau maslahi ya taifa na kujali maslahi ya vyama vyao.

  Hili la ushabiki wa vyama na kusahau maslahi ya taifa, limeanza muda mrefu, ambapo tumeshuhudia matukio ya kuzomeana, na hata wabunge kurushiana maneno.

  Yapo matukio makubwa yaliyoshindikana kupatiwa suluhisho bungeni baada ya wawakilishi hao kutanguliza itikadi na ushabiki wa vyama vyao badala ya kuzingatia maslahi na mahitaji ya wananchi.

  Jaji Joseph Warioba amepata kuonya dhidi ya tabia na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wabunge na kuwashauri wabadilike, watumie mamlaka na heshima waliyopewa kulinda hadhi ya Bunge.

  Jaji Warioba, kama walivyo watanzania wengi, anashangazwa na lugha inayotumika na kutumiwa na baadhi ya wabunge kuwa si ya staha, kuna kubezana, kejeli na kelele za ovyo ovyo.

  Anasema hali hiyo huwafanya watazamaji wa kipindi cha Bunge kujiuliza iwapo wanaofanya hivyo ni viongozi kweli, na wanatoa mafunzo gani kwa wananchi waliowachagua.

  Nawakumbusha wabunge watambue na kutumia nafasi zao kama wawakilishi ili kutimiza wajibu waliotumwa na wapigakura wao.

  Heshima ya Bunge inatokana na aina ya wabunge waliopo, hivyo ni wajibu wao kuisimamia Serikali na kuhakikisha inakaa kwenye mstali.

  Hii ina maana wabunge wote kwa ujumla wao, wanatarajiwa kuweka kando itikadi za vyama, na kubakia na jambo moja kichwani kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi, hivyo wajibu wao ni kusimamia maslahi ya taifa na wananchi wake.
   
 8. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ....hakuna kipindi ambacho Mh. Lukuvi ameshikishwa adabu na Wapambanaji kama hiki...
   
Loading...