singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza wakuu wa mikoa kumpatia orodha ya migogoro yote ya ardhi kwenye maeneo yao kwa ajili ya kutatuliwa mwaka huu.
Alitoa maagizo hayo juzi kwa nyakati tofauti alipokutana na viongozi wa serikali mkoani hapa na pia kwenye uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Kanda ya Mashariki.
Kwa upande wa kikao, alikutana na viongozi wa serikali ya mkoa huo chini ya mkuu wa mkoa pamoja na wa halmashauri za wilaya ya Morogoro na wengine kutoka Manispaa ya Morogoro.
“ Katika migogoro ya ardhi, haiwezi kutatuliwa na wizara moja pekee, bali inatakiwa kutembea kama timu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Kilimo... na ikichambuliwa migogoro hiyo kwa umoja wake itapata majawabu kamili na utamalizwa,” alisema Waziri Lukuvi.
Alisema migogoro mingi ya ardhi imegawanyika katika makundi tofauti yakiwemo ya mipaka ya ardhi ya vijiji kwa vijiji, ndani ya vijiji, hifadhi za misitu na vijiji, hifadhi za wanyamapori na vijiji na wawezaji na wananchi.
Pia alitaja migogoro mingine ya ardhi ni ya kiutawala katika ngazi za wilaya kwa wilaya na mikoa kwa mikoa .
Kwa upande wa mashamba pori, Waziri Lukuvi alieleza kushangazwa na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kulalamika kuwepo kwa idadi kubwa ya mashamba pori yasiyoendelezwa wakati wana uwezo wa kisheria wa kutoa notisi kwa wamiliki wake kwa lengo la kufutiwa hatimiliki.
Alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, orodha ya mashamba 15 makubwa ambayo wamiliki wake wameyaweka rehani kwenye benki na kuchukua mikopo ambayo inadaiwa imetumika katika shughuli nyingine na si za uendelezaji wa uwekezaji wa sekta ya kilimo kama ilivyokusudiwa.
Waziri Lukuvi aliutaka uongozi wa mkoa kufuatilia mashamba hayo kwa kufanya ukaguzi wa kina kubaini kama yameendelezwaje kulingana na sheria. Alitaka kazi hiyo ikamilike ifikapo Machi mwaka huu kabla ya hatua hatua za mwisho za kisheria kwa wahusika kuchukuliwa.
“Morogoro ndiyo yenye migogoro mingi ya ardhi, lakini viongozi wake hawachukui hatua, hii ni mara yangu ya tatu kila nikija hapa ni kwenye taarifa ni kulalamika mashamba pori, sioni hatua zinazo chunguliwa,” alisema Lukuvi.
Alisema, “ Katika halmashauri zote za mkoa huu, nane ... ni Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero pekee imechukua hatua na Rais amefuta hati za mashamba makubwa saba yasiyoendelezwa. Hizi nyingine sijaona maombi yao ikiwemo Kilosa ambayo ndiyo ina migogoro mikubwa.”
Waziri Lukuvi pia alimkabidhi orodha ya majina ya watu binafsi wenye mashamba makubwa 14 kutoka katika ardhi ya vijiji na kutaka watu waliopewa mashamba hayo kufuatiliwa kuona endapo wanayaendeleza au yamewekwa kuwa ni akiba na yasipojendelezwa hatua za kisheria zikiwemo na kuwanyang’anya mara moja.
“ Watu wote waliochukua ardhi kubwa ya vijiji ukaguzi uanze kufanyika mara moja ili kuona kama yameendelezwa na yasipoendelezwa hatua zichukuliwe za kuwany’anyanga mashamba hayo ili kundoa migogoro ya ardhi kwa wananchi vijijini,” alisema Waziri Lukuvi.