Lukuvi ndani ya Kumekucha ITV

akizungumza na ITV muda huu, waziri wa nchi maswala ya bunge mh. William Lukuvi, amesema ndani ya bunge huwa kuna caucas mbalimbali za kivyama. Amesema wao kama chama tawala hujifungia kuzungumzia maendeleo ya taifa, na vyama vya upinzani hujifungia kupanga kuzomea na kuleta vurugu bungeni, pale serikali na chama tawala wanapoleta hoja nzito.

Nadhani nahitaji kujua akili za hawa viongozi tulionao..

is it fact????
 
awaita ukawa wazushi. rasimu sio maoni ya mwisho ndiyo maana kuna kura ya maoni.
 
Hawana jipya,

hii nayo ni aina nyingine ya umbea ndani ya bunge!

Badala ya kutuambia lini watajipunguzia mshahara mpaka shs 5m, wanakaa kutengeneza majungu tu!
 
Anazidi kupotosha kwamba waliotoa maoni ya muundo wa muungano ni wachache. Nashangaa kwanini mtangazaji hamuuliza mbona walittoa maoni kuhusu mfumo dume ni watu 2 tu, Je ina maana watu wengine ambao hawakuongelea kuhusu mfumo dume Tanzania wana support mfumo dume. Nafikiri CCM kama utetetezi wao uko kwenye takwimu wanazidi kujipakaza kinyeshi.
 
Akili za wapinzani zinawatosha wenyewe tu kuzomea wanaona ni bonge la ishu kwao.
 
Hawana jipya,

hii nayo ni aina nyingine ya umbea ndani ya bunge!

Badala ya kutuambia lini watajipunguzia mshahara mpaka shs 5m, wanakaa kutengeneza majungu tu!
Mkuu kwani wanalipwa kiasi gani mpaka sasa.
 
anasema hatuwezi kujadili maoni ya kuhusu idadi ya serikali ambapo ni watanzani wachache sana waliozungumzia maswala ya muundo wa serikali..

Anasema hata ukawa wasiporudi bungeni, waliobaki wanaweza kuendelea na mchakato wa kutunga katiba.
 
Anasema kupata theluthi mbili ya kura ya maoni si lazima ukawa wawepo bungeni.. hiyo inapatikana kwa maridhiano ndani ya bunge kwa waliopo.
 
Sitta amewaita Ukawa kwa majadiliano ya kurudi bungeni..
tutaona kama wataenda au watakataa - Lukuvi
 
Kama ukawa wanataka marekebisho ya sheria mbalimbali za uchaguzi kwa dharura, basi warudi bungeni tuyazungumze kupitia katiba mpya..
 
Yani serikali inawaza wapinzani tu badala ya kufanya vitu muhimu kwa taifa sasa waziri mzima anaalikwa kwenye kipindi anaongea umbea kama huo.si kujizalilisha kweli kama wanajifungia yeye kajuaje pointless kama hivi ni za kujizalilisha tu na kuonyesha upeo mdogo
 
awaomba ukawa warudi bungeni ili angalau wajadili muundo wa tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom