Luka: Daktari, Mtafiti, na Mwinjilisti

Luka: Daktari, Mtafiti, na Mwinjilisti

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,640
Mwandishi wa Injili yenye utafiti wa kitaalamu kuhusu maisha ya Yesu Kristo

Luka, mmoja wa waandishi wa Injili nne katika Agano Jipya, ni mtu wa pekee. Tofauti na Mathayo, Marko, au Yohana – Luka hakuwa Myahudi, bali alikuwa Mgiriki, Daktari wa tiba, Mtaalamu wa uandishi, na Mwandani wa Mtume Paulo. Zaidi ya hayo, aliandika Injili ya Luka na kitabu cha Matendo ya Mitume, akionesha kwa kina historia, maisha, mafundisho, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo kwa mtazamo wa kitaalamu, wa kihistoria na wa kihuruma kwa watu wa mataifa yote.

LUKA KAMA DAKTARI NA MTAFITI

Mtume Paulo mwenyewe anamtaja Luka kwa heshima kubwa kama "daktari mpendwa":

"Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu."
Wakolosai 4:14

Katika enzi za kale, madaktari waliheshimika sana kwa sababu ya elimu yao ya juu na uwezo wao wa kuchunguza mwili na tiba. Kwa kuwa Luka alikuwa daktari, basi ni wazi alikuwa mchunguzi, mtafiti, na mwandishi makini wa taarifa sahihi. Hili linathibitishwa moja kwa moja na jinsi alivyoanza Injili yake kwa kusema:

“Kwa kuwa wengi wamejaribu kuandika habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu... nimeona vema nami pia... baada ya kuyaandikia kwa taratibu yote tangu mwanzo, nikakuandikia wewe mpendwa Theofilo, ili upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.” Luka 1:1–4

Luka hakuwa shahidi wa macho, lakini alikusanya ushahidi wa wale waliomwona Yesu, akawahoji, akapima taarifa kwa uangalifu mkubwa. Alifanya kazi ya mtafiti wa kihistoria na kitaalamu kama daktari wa akili timamu alitumia mbinu ya “kutathmini mashahidi” ambayo leo inatumika hata kwenye uandishi wa vitabu vya kihistoria na tafiti.

MUUNDO WA UANDISHI WA LUKA

Injili ya Luka ni mojawapo ya maandiko yaliyoandikwa kwa Kigiriki fasaha zaidi katika Agano Jipya. Ana mtiririko mzuri wa mawazo, msamiati mpana, na mtindo wa kisomi. Pia alizingatia mtazamo wa kimataifa Injili yake inamuelezea Yesu kama Mwokozi wa watu wote, si tu Wayahudi.

Tofauti na

Mathayo, aliwaandikia Wayahudi na kuonesha kuwa Yesu ndiye Masihi aliyetabiriwa katika Tanakh,

au Marko, aliyelenga nguvu za Yesu,Miujiza na kazi zake.

na hata Yohana, aliyelenga kuonesha uungu wa Yesu Kristo kwa kuanzia na

"Naye Neno alikuwako kwa Mungu... naye Neno alikuwa Mungu" (Yoh. 1:1),

Luka alielezea maisha ya Yesu kwa muktadha wa kihistoria, kiubinadamu na kiunabii, akilenga watu wa mataifa mengine (non-Jews).

Aligusia uzazi wa Yesu, uhusiano na wanawake, watu wa chini, maskini, na watu wa mataifa jambo ambalo halikupewa uzito sawa katika Injili zingine.

THEOFILO NI NANI?

Katika utangulizi wa Injili yake, Luka anamwandikia mtu aitwaye Theofilo:

"... nikakuandikia wewe, mpendwa Theofilo..." Luka 1:3

Jina “Theofilo” linamaanisha “mwenye kumpenda Mungu” au “rafiki wa Mungu” (kutoka Kigiriki Theo = Mungu, phileo = kupenda). Hapa kuna mjadala kati ya wachambuzi wa maandiko

Wengine wanaona Theofilo ni jina la cheo au mwakilishi wa waumini wote.

Lakini wengi wa watafiti wa Biblia na historia wanakubaliana kuwa Theofilo alikuwa mtu halisi pengine kiongozi Mroma au mtu mwenye cheo cha kifalme aliyeamini Ukristo au alikuwa anafundishwa.

Tafsiri ya Kigiriki ya neno “mpendwa sana” (kratiste) ni neno lililotumika kwa maafisa wa ngazi ya juu (kama vile katika Matendo 23:26 na 24:3). Hii inaonesha Luka aliandika kwa mtu muhimu, akieleza kwa undani taarifa za maisha ya Yesu kama ushahidi wa kweli.

USHAHIDI WA KI-AKIOLOJIA NA KIHISTORIA

Luka anatajwa na wasomi wa Biblia na historia kama mwandishi wa kihistoria mwenye usahihi mkubwa. Mtaalamu wa kale wa Kihistoria, Sir William Ramsay, ambaye awali alikuwa mtaalamu asiyeamini Biblia, baada ya miaka ya kuchunguza maeneo ya Biblia aliandika:

“Luka ni mwanahistoria wa daraja la kwanza... Anafaa kuhesabiwa miongoni mwa waandishi wakuu wa historia.”

Ramsay alithibitisha kuwa mambo mengi ya kihistoria aliyoyaandika Luka katika Injili na Matendo ya Mitume (kama majina ya miji, cheo cha viongozi, nyakati, na sheria) yalikuwa sahihi kabisa, hata zaidi ya wanahistoria wa wakati wake.

Pia utafiti wa akiolojia umeonesha usahihi wa mambo aliyoyataja Luka, kama vile mji wa Listra, Darbe, Ikonio, na majina ya magavana kama “Sergius Paulus” (Matendo 13:7), ambao walikuwepo kihistoria kama maandiko ya kale yanavyoonyesha.

LUKA NA UUNGU WA YESU

Ingawa Luka hakuelekeza sana kwa misamiati ya moja kwa moja kama “Yesu ni Mungu” kama Yohana, bado anaweka wazi kuwa Yesu ndiye Mwana wa Mungu, Masihi aliyeahidiwa, kwa mfano:

"Mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu."
Luka 1:35

"Leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."
Luka 2:11

Kwa hiyo, ujumbe wa Luka unasisitiza kuwa Yesu ni wa kipekee, ana asili ya Kimungu, na amekuja kuokoa wanadamu wote bila kujali kabila, cheo, jinsia wala historia.

Luka si tu mwandishi wa Injili – alikuwa daktari, mwanahistoria, na mtaalamu wa kutafuta ukweli kwa undani. Mtindo wake wa kisomi, uchambuzi wa ushahidi, na mtazamo wa kiulimwengu unamfanya awe kiungo muhimu sana katika kuelewa ujumbe wa Yesu Kristo kwa watu wote.

Alimwandikia mtu halisi Theofilo lakini ujumbe wake ni wa milele: Yesu Kristo ni Mwokozi wa watu wote, na habari zake zimehakikiwa kwa utafiti makini si hadithi za mtaani.
images (1).jpeg
 
Injili ya Luca, Marco na Matayo ni synoptic kwa mfanano wa mtiririko wa masimulizi. Yohana yeye alıandika kwa utofauti.
 
View attachment 3407612
Hii imenyooka.
 
Umeisimulia vizuri. Asante.

Pia umeonesha muunganiko ulio kati ya mitume waliohudumu kipindi cha Yesu, (kutia ndani Luka) na Paulo. Namtaja Mtume Paulo kwa maana kuna wengine wanapinga kwamba, hapaswi kuitwa mtume kwa maana hakuhudumu kipindi ambacho Yesu alikuwa hai
 
Asante sana. Bwana Yesu akubariki mno🙏🏾🙏🏾
 
Kile kitabu kakipangilia vizuri sana kuliko kina yohana wavuvi,

Uandishi wake unaona kabisa ni msomi wa Hali ya juu
Mtumish yohana alitisha sana acha kumchukulia poa

Yote kwa yote ubalikiwe sana unaletaga vitu Kong sana usiwe na unaleta uzi pasipo kunitag
 
Asante kwa historia, Hivi Paulo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani? na walikutanaje na Dokta Luka?
 
Mtumish yohana alitisha sana acha kumchukulia poa

Yote kwa yote ubalikiwe sana unaletaga vitu Kong sana usiwe na unaleta uzi pasipo kunitag
Sawa mkuu nitakuwa na kutag

Biblia tamu sana aisee,

Zile injili bhana zimeandikwa kila moja kwa tabia ya muandishi

Mfano angalia ya Yohana ,ile kukaa sana karibu na Yesu ,akaajifunza sana upendo wa Yesu ,

Hata uandishi wake wa injili anapita mule mule kwenye maswala ya upendo wa agape

Mathayo yeye ni myahudi haswa halafu mtoza ushuru , anajua kiasi chake Sheria ,alikuwa farisayo

Injili yake yeye anatamani sana ndugu zake wayahudi wamjue Yesu ndiye aliyeandikwa na manabii ,

Injili yake imejaa Quotation nyingi sana za agano la kale

Luka yeye ni researcher ,mtafiti ,anafata taratibu zote za utafiti

Biblia kitabu kitamu sana
 
Umeisimulia vizuri. Asante.

Pia umeonesha muunganiko ulio kati ya mitume waliohudumu kipindi cha Yesu, (kutia ndani Luka) na Paulo. Namtaja Mtume Paulo kwa maana kuna wengine wanapinga kwamba, hapaswi kuitwa mtume kwa maana hakuhudumu kipindi ambacho Yesu alikuwa hai
Hao wanaompinga Paulo ni wanatapatapa

Paulo alikutana na mitume wengine kama Petro ,yohana ,n.k

Paulo alikuwa Anaijua Torati kiundani sana ,

Yule jamaa nyaraka zake sio za kuzikurupukia

Imagine Petro alizisoma zikamchanganya ,akatoa kabisa tahadhari kuhusu nyaraka za Paul

Jamaa alikuwa msomi wa Hali ya juu sana

Nipo naandaa documentary fupi fupi za miji aliyopita kama Efeso, foinike huko Lebanon, n.k

Athari zake zipo mpaka Leo

Paulo alikuwa ukimpa nafasi umekwisha
 
Sawa mkuu nitakuwa na kutag

Biblia tamu sana aisee,

Zile injili bhana zimeandikwa kila moja kwa tabia ya muandishi

Mfano angalia ya Yohana ,ile kukaa sana karibu na Yesu ,akaajifunza sana upendo wa Yesu ,

Hata uandishi wake wa injili anapita mule mule kwenye maswala ya upendo wa agape

Mathayo yeye ni myahudi haswa halafu mtoza ushuru , anajua kiasi chake Sheria ,alikuwa farisayo

Injili yake yeye anatamani sana ndugu zake wayahudi wamjue Yesu ndiye aliyeandikwa na manabii ,

Injili yake imejaa Quotation nyingi sana za agano la kale

Luka yeye ni researcher ,mtafiti ,anafata taratibu zote za utafiti

Biblia kitabu kitamu sana
Mathayo sura ya tano alitisha sana
 
Back
Top Bottom