GE2025 Luhaga Mpina hajafikiria vizuri

GE2025 Luhaga Mpina hajafikiria vizuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
279
Reaction score
389
🔸Kwenda ACT ni faida kwa CCM na ACT.

🔸Hajaikomesha CCM ila kajikomesha Mwenyewe.
🔸Karata ya "win win situation" hajaichanga vizuri.

Hakuna asiyejua kuwa Luhaga Joelson Mpina ni mtu mwenye msimamo thabiti katika masuala mbalimbali ya Kitaifa hasa yanayogusa maslahi ya umma na anakubalika na wengi wenye chembechembe za uzalendo wa rasilimali za Taifa.
FB_IMG_1754468488114.jpg


Mpina ni 'Public Figure' ama kwa Sauti ya Mama Samia "Mpina ni Mbunge wa Taifa' hii ni kutokana na Ujasiri wake wa kuhoji mambo mbalimbali ya Kitaifa kuliko kwenye jimbo lake.

Msimamo wake umemjengea umaarufu wenye heshima akiwa ndani ya CCM.

Maamuzi ya Mpina ni ya hasira za kukatwa jina na kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Ubunge Jimboni Kisesa.

Maamuzi yake kwenda ACT ni ya hasira na kutaka kuikomesha CCM na watesi wake na hasa anapokwenda Moja Kwa Moja kupeperusha bendera ya ACT kwa Nafasi ya Urais. Baada ya Uchaguzi 2025, atakuwa ndio amejimaliza Kisiasa.

Mpina kwenda ACT hajafikiria kanuni maarufu ya "Win Win Situation". Kanuni hii hutumiwa kwenye nyanja nyingi ikimaanisha pande zote mbili kunufaika.

ACT ina faida zaidi kuliko Mpina yaani ACT ina-Win, Mpina ana-loose.

Hapa ACT itamtumia Mpina kama mgombea Urais kuji-brand. Na kwa namna yoyote ile ACT haitaweza kushinda kiti cha Urais 2025.

Mpina atatapika hasira zake zote na pengine kampeni zikawa za moto lakini baada ya Uchaguzi kuisha ni ACT ndio itakuwa imejengeka ikimwacha Mpina amechuja umaarufu wake.

Upande wa CCM, Mpina atakuwa amesaidia kuleta uwiano na umaana wa mfumo wa Uchaguzi wa vyama vingi na hivyo kukata mzizi wa Fitina wa Mataifa ya Magharibi kuituhumu Serikali ya CCM kuwa inabinya Demokrasia baada ya Chadema kutoshiriki Uchaguzi kama Chama Kikuu Cha Upinzani TZ.

Mpina atatumika, atachokwa, atatupwa. Ni heri zaidi angenyamaza kimya ndani ya CCM, kujiandaa 2030 kama alikuwa na nia ya kugombea Urais~Ukimya ungempa heshima kubwa sana.

Akisema aje kurudi CCM baada ya Uchaguzi 2025, tayari atakuwa ameshajipaka Matope ya kuwa "Mwanasiasa Malaya Malaya~by Mwalimu Nyerere" kwahiyo hataaminika tena na itathibitisha kuwa ni kweli ulikuwa mkakati wa CCM kama wengi wanavyodai kwa sasa.

Yote Kwa Yote Tuwe Wazalendo Kwa Nchi Yetu.
 
Back
Top Bottom