Lugumi na Sarakasi za Serikali

franklin12xx

Member
Sep 24, 2014
28
31
Hakika tunapoelekea nchi hii ni kubaya mno. yaani ukiiba hela ndefu basi ndio usalama wako tofauti na waiba kuku ambao lengo ni kupata kitoweo kutokana na hali duni ya maisha iliyosababishwa na serikali hii ya CCM.

Gazeti la nipashe la leo linasema report ya lugumi itawasilishwa soon na kamati maalum iliyopewa jukumu la kuichunguza ila haitotaja majina ya waliohusika.
hapa kuna swali la kujiuliza, lengo la kufanya uchunguzi kwa kutumia fedha za umma ni nini? kama wanatoa report bila majina maana yake si ni report nusu sasa hiyo report ya nini si wakae nayo tu.

Maana sakata lenyewe limeletwa na upinzani bungeni na kama muonavyo sasa hivi naibu spika kazi yake ni kuminya democrasia sasa hiyo report kwenda bungeni bila majina na upinzani ndio umeamua kutoka nje baada ya democrasia kuwekwa pembeni bungeni, kuna haja kweli ya kuwasilishwa.

mii nchi aisee ni ajabu la nane la dunia. sijui lini hakika tutatoka katika hili giza.
 
Kumbe siasa za kulindana bado zinaendelea kwa hali hii sitashangaa kuona washitakiwa kwenye mahakama ya ufisadi wakihukumiwa bila kutajwa majina.Ngoja tuone muda utaeleza
 
Hakika tunapoelekea nchi hii ni kubaya mno. yaani ukiiba hela ndefu basi ndio usalama wako tofauti na waiba kuku ambao lengo ni kupata kitoweo kutokana na hali duni ya maisha iliyosababishwa na serikali hii ya CCM.

Gazeti la nipashe la leo linasema report ya lugumi itawasilishwa soon na kamati maalum iliyopewa jukumu la kuichunguza ila haitotaja majina ya waliohusika.
hapa kuna swali la kujiuliza, lengo la kufanya uchunguzi kwa kutumia fedha za umma ni nini? kama wanatoa report bila majina maana yake si ni report nusu sasa hiyo report ya nini si wakae nayo tu.

Maana sakata lenyewe limeletwa na upinzani bungeni na kama muonavyo sasa hivi naibu spika kazi yake ni kuminya democrasia sasa hiyo report kwenda bungeni bila majina na upinzani ndio umeamua kutoka nje baada ya democrasia kuwekwa pembeni bungeni, kuna haja kweli ya kuwasilishwa.
.
Ni matumizi mabaya ya pesa za umma.
 
Hiyo ndio nia thabiti ya kupambana na mafisadi unawalinda na kutowataja majina! Ukija jukwaani mnasema mnapambana na mafisadi na ufisadi!! Saw sawa
 
Report bila majina Ni report Hiyo au upuuzi? Hata hadithi za kusadikika na kufikirika zina majina ya wahusika. Huo upuuzi wa hiyo report wasomeane wenyewe .
hii issue ya LUGUMI yao wanaelekea nayo pabaya. Tutaona mengi hadi 2020 kitaeleweka tu
 
Back
Top Bottom