neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba, mashamba na madanguro kunusuru waathirika wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu hasa watoto.
Pia ameagiza kuondolewa haraka kwa Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti biashara hiyo, Abubakar Yunusu kwa kushindwa kumpa idadi ya vyombo vya usafiri vilivyotaifishwa na serikali kwa kusafirisha wahamiaji haramu.
Lugola amelitoa maagizo hayo jana Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu akiwa mgeni rasmi.
Amelaani tabia ya watu kuwadanganya na kisha kuwasafirisha binadamu wenzao kwa lengo la kuwapatia kazi nzuri yenye maslahi makubwa mijini na kisha kuwatumikisha kwenye shughuli zisizokuwa za kimaadili na hatarishi kwao pia.
Amesema watu ambao huenda mikoani kuwarubuni wazazi na walezi wa watoto kuwa wanawapeleka mjini kuwatafutia kazi nzuri watoto hao huku wakijua fika kuwa wanakuja kuwafanyisha kazi za hatari bila ya malipo.
Alisema kwa kuwa usafirishaji haramu wa watu unafanyika nchini, Jeshi la Polisi lina kila sababu ya kukabiliana nayo huku pia akiahidi kudhibiti wanaosafirisha watu nje.
Aliagiza Polisi kuzunguka katika nyumba za watu, mashamba na madanguro kuwanusuru waathirika wa usafirishaji huo hasa watoto.
“Hapa nchini wapo watu kwenye nyumba, mashamba na madanguro hufanyishwa vitendo na huwa hawana pa kwenda kulalamika, hivyo nyie mnaweza kuwanusuru watu hao,” alisema.
Aliagiza wakuu wa vituo vya Polisi kusaidia waathirika wa biashara hiyo wanaopeleka malalamiko yao huko akitaka wajue watu hao ni waathirika wa biashara hiyo, hivyo wawasikilize na kuchunguza kujua wanaofanya biashara hiyo.
Pia ameagiza Idara ya Uhamiaji, balozi za nje ya nchi zilizopo hapa nchini kuwafuatilia kwa undani zaidi, Watanzania wanaoomba vibali vya kwenda kufanya kazi nje ya nchi kwa kuwa wapo wanaosafirishwa kwenye biashara hiyo.
Waziri Lugola aliongozana na wageni wengine na alitembelea mabanda ya maonesho na katika banda la kwanza la Idara ya Uhamiaji, alisikiliza maelezo idara hiyo inavyoikabili biashara hiyo.
Abubakar Yunusu alimwelezea Waziri mikakati na mafanikio kukabili hilo kwa kutaifisha vyombo vya usafiri vilivyosafirisha watu lakini akashindwa kutaja idadi akidai hana takwimu.
Waziri Lugola alikerwa na majibu hayo na kusema: “yaani wewe unaniambia mimi waziri huna idadi ya magari yaliyotaifishwa hadi sasa, wewe hufai kuwa kwenye kamati hii na kwa kuwa Idara hii ya Uhamiai ipo chini ya wizara yangu ninaagiza utolewe haraka kwani haufai.”
Waziri Lugola alitembelea mabanda mengine na baadaye alizindua mwongozo wa miaka mitatu hadi 2021 wa kukabiliana na biashara hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya kupinga usafirishaji wa binadamu, Abeatus Magere aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi katika kukabiliana na biashara hiyo.