Lugha za mapenzi...

Call me GHOST

Member
Jan 18, 2019
53
93
Kuna vitu vitatu(Imani, Tumaini na Upendo) ambavyo kama binadamu anavihitaji ila kati ya mambo hayo matatu UPENDO ndio jambo kubwa ambalo kila mmoja analihitaji kuliko mengine hayo ata Biblia imezungumzia hilo (1 Corinthians 13:13)

Kuna msemo unaosema "kila nyuma ya mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke nyuma yake.." huu msemo unamaana kubwa sana ata katika mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.

Lakini pia kuna msemo unasema "Inside every child is an EMOTIONAL TANK waiting to be filled with love. When a child really feels loved, he will develop normally but when the love tank is empty, the child will misbehave. Much of the misbehavior of children is motivated by the cravings of empty LOVE TANK" sasa huu msemo sio tu umezungumzia watoto HAPANA ila tunaweza pia utumia ata kwa sisi watu wazima na ata kwa walio kwenye ndoa.

Kila mmoja wetu anahitaji Upendo ili kuushibisha moyo wake na kupata nguvu ya kufanya kazi, kusoma n.k bila hivo lazima vitu kama stress,depression n.k viwe sehemu ya maisha yako ya kimapenzi.

Kuna msemo mwingine unasema "At the heart of mankind's existence is the desire to be intimate and to be loved by another. Marriage/relationship is designed to meet that need for intimacy and love"

Kila binadamu anahitaji UPENDO na akiupata upendo mambo mengine yana nafasi kubwa ya kwenda sawia lakini kama binadamu kila mmoja wetu ana namna yake binafsi ya kutafsiri upendo anaoupokea kutoka kwa mpenzi wake.

Sasa ili kuutafsiri upendo huo kila mmoja ana lugha yake ya mapenzi ambayo mpenzi wake akimuongelesha basi yeye anakuwa anaitafsiri hiyo lugha kama ANAPENDWA!

Kuna lugha za mapenzi zipatazo 5 na kila mmoja wetu lazima ana lugha yake moja au zaidi katika hizo lugha 5 na pengine inatofautiana na lugha ya mpenzi wake.

Lugha ya kwanza ni "Words of Affirmation", kuna mtu yeye ili aamini kama anapendwa basi ni lazima uwe unamwambia maneno ya kumsifia, lazima uwe unampa Compliment za mara kwa mara kwenye muonekano na uvaaji wake na hii sana sana ni upande wa wanawake lakini kwa upande wa wanaume wengi wanapenda kusifiwa kwenye characters au kumshukuru kwenye vitu alivyokufanyia n.k

Mark twain aliwahi kusema; "I can live for two months on a good compliment" kwahiyo maneno yana nguvu kubwa sana kwenye mahusiano yenu. Ulimi wako una nguvu kubwa ya kujenga au kubomoa mahusiano yako USIUDHARAU!

Ata Biblia imejaribu kunena jambo kuhusu nguvu ya ulimi wako ukisoma kitabu cha Mithali 18:21 inasema;

"Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake"

Na ili kuonesha nguvu ya maneno katika kitabu hiko hiko cha Mithali 12:25 Maandiko yakaendelea kusema;

" Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha."

Mstari huu unamaanisha kwamba unaweza kuwa na mafadhaiko moyoni mwako yanayokufanya unyong'onyee lakini unaweza ambiwa maneno mazuri ya hekima na upendo yakakupa nguvu na kukufanya ufurahi pia. So, usichukulie poa nguvu ya MANENO kwenye mahusiano yako.

Wanasema "If an apple a day keeps the DOCTOR away may be a compliment a day will keep the COUNSELOR away" hivyo basi kama lugha ya mapenzi ya mpenzi wako ni hii basi jitahidi kadri uwezavyo kila siku unamwambiwa maneno mazuri mazuri coz kwenye hii lugha MANENO ni ya MUHIMU sana.

Lugha ya 2 ni "Quality Time", Kuna watu wenyewe ili waamini unawapenda basi ni lazima uwape MUDA wako. Tuelewane hapa, Naposema uwape muda wako namaanisha uwape ATTENTION(undivided and focused) yako sio tu kuwa karibu yake halafu uko bize unachat kwenye groups au na rafiki zako au pengine upo nae lakini uko busy unacheza PS.

Dhumuni kubwa la Quality time ni TOGETHERNESS na sio CLOSE PROXIMITY so ni lazima umpe attention yako UMSIKILIZE kama kuna kitu anahitaji kusikia kutoka kwako MWAMBIE sasa shida ni kwamba kwenye hii lugha tunaathiriwaga sana na personality zetu coz kuna baadhi ya watu ni DEAD SEA( Ni wazuri wa kusikiliza lakini sio waongeaji) na kuna wengine ni BABBLING BROOK(ni wazuri wa kuongea lakini hawajui kusikiliza) So hapo kila mmoja wenu lazima ajiulize ni mtu wa aina gani kama sio muongeaji itakubidi ujifunze kuongea unapokuwa na mwenzako na kama sio msikilizaji lazima ujifunze kumsikiliza mwenzako.

Kuna msemo unasema "The object of love is not getting something you want but doing somwthing for the well-being of the one you love."

So kama mpenzi wako yupo kwenye hii lugha hakikisha unampa Muda wako na kama kuna kazi angependa umsaidie basi fanya hivo pia coz upande wake yeye natafsiri hii kama unampenda.

Lugha ya 3 ni "Receiving Gifts", kuna watu wao bila kuwapa/kuwanunulia zawadi mara kwa mara hawaamini kama unawapenda. Kwao zawadi zinamaanisha kuwa ulikuwa unamfikiria kabla hujaenda kununua zawadi hiyo so unapofanya jambo hili mara kwa mara inamfanya aamini unampenda coz anaamini ulikuwa unamfikiria kila mara kabla ya kununua zawadi. Tuelewane hapa, ZAWADI simaanishi umpe PESA sema itategemeana na namna mpenzi wako anavyoichukulia hiyo zawadi kama ndio lugha yake ya mapenzi.

Lugha ya 4 ni "Acts of Service", kuna watu wao ili waamini kama unawapenda lazima uwafanyie mambo fulani kwa mfano Umfulie nguo, umpikie chakula kama ni Boyfriend wako ukienda anapoishi umfanyie usafi n.k

Kuna msemo unasema "A way to a man's heart is through is stomach" so wanaume wengi japo sio wote wanaongea lugha hii kwa maana kwamba wanaume wengi wanawapenda wanawake wanaowafanyia majukumu kama kumpikia chakula kizuri, kumfanyia usafi wa nyumba na mavazi n.k kwa mwanamke kama mna usafiri wenu umfungulie/kumfungia mlango wa gari, kama mmeenda nae hotelini umvutie kiti akae, kama yuko nyumbani asubuhi kabla hajaenda kazini umvalishe viatu au kumvalisha saa au cheni yake kabla hajaondoka n.k

Lugha ya 5 ni "Physical Touch", kwa maana kwamba kuna watu wenyewe ili waamini wanapendwa lazima uwape miguso kama kumshika mkono mkiwa mnatembea barabarani, kumbusu mbele za watu, kumkumbatia mara kwa mara lakini pia kufanya nae mapenzi mara kwa mara hapo kwenye hiyo Dialect ya mwisho hiyo ya Kufanya Mapenzi ndio wanaume wengi wapo hapo ukiwa unakataa kufanya nae mapenzi mara kwa mara anaanza kuamini pengine upendo wako kwake umeshuka na pengine umeuamishia kwa mtu mwingine bila kujua pengine mnatofautiana kwenye lugha zenu za mapenzi tu.

Wanasaikolojia wanasema kwamba "Physical touch can make or break a relationship, it can communicate hate or love" ukutaka kujua ni kweli hebu kataa kumpa unyumba mpenzi wako au mume wako kwa muda mrefu uone nini kitatokea kwenye uhusiano wenu..!

Wataalamu wa afya wanasema "One medicine cannot cure all diseases" so ata kwenye mahusiano yaweza kuwa mpenzi wako ana lugha za mapenzi zaidi ya moja hivyo basi ni jukumu lako kuzijua lugha zake coz unaweza kumpa Quality time lakini ukasahau kumpa physical touch au unaweza kumpa words of affirmation ila ukasahau kumpa Acts of service na kumbe zote ni lugha zake za mapenzi.

Kuna watu wapenzi/wake zao wanawacheat wanaanza kulalamika yule mwanamke nilimpa kila kitu nilimhudumia nilimpa kila hitaji alilolitaka lakini unasahau kwamba ulimpa SAA alipohitaji MUDA wako ikiwa na maana kwamba ni kweli ulikuwa unamhudumia, pesa unampa, anaishi sehemu nzuri n.k lakini umesahau alikuwa anahitaji muda wako sasa siku akipata Mtu atakae elwa lugha yake ya mapenzi yuko ladhi kuwa nae coz ndio anampa furaha unabaki unajiuliza Mimi ni tajiri nina pesa, nina magari, nina majumba lakini mbona mke wangu ameenda kutembea na msafisha kucha kumbe issue ni ndogo tu kwamba msafisha kucha anampa words of affirmation ambayo ndio lugha yake lakini wewe ulikuwa unampa Receiving gifts pekee.

Kwa kifupi ni kila mtu ana lugha yake ya mapenzi ila changamoto ni kwamba watu wengi ile lugha yao ndio wanataka waitumie kuonesha wapenzi wao bila kujua na wao wana lugha zao ambazo pengine ni tofauti

So, Lazima ujue lugha(primary language) yako ni ipi ambayo ina nguvu zaidi lakini pia lazima ujue lugha ya mpenzi wako ni ipi yenye nguvu zaidi..!

Nimeamua niandike hivi kwa sababu kila mmoja wetu anajua kwamba "Written words have the benefit of being read over and over" so kama haitakusaidia wewe pengine itamgusa na kumsaidia mwingine siku zijazo..!!


Niwatakie mahusiano mema..!!
Till next time BYE! BYE!
 
Back
Top Bottom