Lugha na masomo shuleni jibu hili

Mapigomoto

Member
Jan 21, 2016
19
11
Lugha na masomo shuleni jibu hili

Wadauo wa elimu wanapojadili kuhusu ubora wa elimu, pia hujikuta wanaongelea lugha gani itumike kufundishia masomo shuleni. Wakiangalia sera mpya ya elimu, inasema lugha za kufundishia ni mbili; Kiswahili na English. Wanajiuliza, kati ya hizo, lugha ipi itumike? Wanajijibu kuwa sera haieleweki.

Jibu ni hivi:

Tangu wakati wa ukoloni hadi leo, lugha za kufundishia masomo shuleni ni Kiswahili na English tu. Hizo ni luhga mbili. Shule za msingi hufundisha kwa Kiswahili na shule za sekondari kwa English. Watu wote ambao wamesoma kupitia shuleni wanajua hivyo.

Unaposema lugha ya kufundishia masomo shule za sekondari na vyuo iwe Kiswahili, unasema, lugha ya kufundishia masomo shuleni iwe moja tu. Hivyo, unapingana na sera.

Kusema China na Japani shule zinatumia lugha zao, halafu huelezi miaka ambayo waliwahi kutumia English, hutaeleweka. Australia wakati wa ukoloni walitumia English na mpaka sasa wanatumia English.

Tanzania ina kazi kubwa kuimarisha ubora wa elimu kutoka shule za awali hadi vyuo vikuu. Kila ngazi inatakiwa kuboresha eneo lake bila kulaumu ngazi nyingine. Baadhi ya vitu ambavyo tunatakiwa kuzingatia ni walimu wakutosha na wenye ubora pia vitabu vya kutosha na bora.

Mtu anayesema sasa tubadili lugha na hivyo walimu wapewe kozi ya lugha na vitabu viandikwe vyote kutoka shule awali hadi vyuo vikuu na hivyo kuimarisha elimu, mtu huyo anaona mbali lakini ana kasoro ya kuona karibu. Uono huo ni gharama sana. Watu kama hao wanania ya kuiibia serikali fedha nyingi kwa kubuni mawazo ambayo hayatakuja kutekelezeka.

Ukisema sasa hivi Taasisi ya Elimu iandike vitabu vyote mwaka huu vya shule za misingi haiwezi, hali hiyo itakuwaje kwa shule ngazi zote?
 
Back
Top Bottom