Lugha 5 za mawasiliano katika mahusiano

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Katika utafiti uliofanywa na Gary Chapman katika Kitabu chake cha THE FIVE LOVE LANGUAGES cha mwaka 1995

Anaeleza kuwa..

Katika maisha ya mahusiano, kila binadamu ana lugha yake ya mawasiliano katika mahusiano. Unagundua lugha ya mpenzi wako katika mahusiano kupitia kujua ni vitu gani au mambo gani anapenda kufanya kwako, na yeye anafurahia ikiwa utamfanyia.

Zifuatazo ni lugha 5 za mawasiliano katika mahusiano zilizofanyiwa utafiti na (Gary Chapman):

Lugha ya maneno ya hamasa au uthibitisho.
Katika mahusiano kuna aina ya mtu anaetumia lugha hii ya mawasiliano katika mahusiano yake.Yeye hutoa maneno ya hamasa na hupenda kupokea maneno ya hamasa pia. Anapenda kusikia maneno ya shukrani, kupongezwa, kujali na kusifiwa ikiwa amefanya jambo fulani katika maisha yake. Aina hii ya mtu asipopata neno la hamasa au uthibitisho kutoka kwako basi ataliomba yeye mwenyewe ili alisikie likitoka kwako.

Mfano;- Anajihisi kupendwa zaidi ikiwa amepika chakula kizuri ukashukuru kwa kumwambia Ahsante kwa chakula. Ameva vizuri ukamsifia umependeza. Amekupatia zawadi ukashukuru.

Aina hii ya mtu asiposikia neno lolote la hamasa la kumsifia au kumjali huwa haamini kama unampenda. Kwenye mahusiano yako ikiwa utaona mpenzi wako anadai maneno ya kushukuru, kupongezwa, maneno ya kusifiwa au maneno ya kujali basi jua kuwa lugha yake ya mahusiano ni maneno ya hamasa au uthibitisho.

Lugha ya muda wa faragha.
Ni aina ya mtu anaetumia lugha hii katika mahusiano yake, yeye lugha yake nikuwa na mda wa faragha na wewe. Anapenda kutoka out na wewe, anapenda mle wote chakula pamoja, mda wake mwingi atapenda kuwa na wewe, atakuomba umtembelee ikiwa upo mbali nae, atapenda mtoke mtoko pamoja, atapenda kila sehemu muende pamoja.

Ukiona mpenzi wako anapenda kuwa na wewe mda mwingi, basi jua hiyo ndiyo lugha yake ya mahusiano. Huyu haitaji maneno ya hamasa kutoka kwako, anachohitaji kutoka kwako ni muda wako wa faragha na wewe. Kwake yeye hii ndoo lugha yake ya mawasiliano katika mahusiano yenu.

Lugha ya zawadi.
Ni aina ya mtu ambaye lugha yake ya mahusiano ni zawadi, yeye anapenda kutoa zawadi na kupokea zawadi. Katika mahusiano ili akupende au aamini kuwa unampenda atataka umpe zawadi.

Aina hii ya mtu kitu chochote anachopewa kutoka kwa mpenzi wake, anakithamini sana na kukifurahia haijalishi ni kikubwa au kidogo kiasi gani.

Mfano:- Ikiwa utamuaga kuwa unasafiri au unaenda sehemu yoyote ile atakwambia, Usisahau kuniletea zawadi.

Katika mahusiano aina hii ya mtu, kwake zawadi ndoo kipaumbele chake. Yeye hana mpango na maneno yako ya hamasa wala hatakudai muda wa faragha, ila usipokuwa na mazoea ya kumpatia zawadi hatoamini kama unampenda.

Lugha ya matendo ya huduma.
Ni aina ya mtu ambaye lugha yake kwenye mahusiano huwa nikusaidia, anajisikia furaha mnapo shirikiana nae katika kufanya kila jambo. Aina hii ya mtu ili aamini kuwa unampenda nilazima uwe unashirikiana nae katika kufanya shughuli anazozifanya yeye.

Mfano:- Atapenda mpike wote, atapenda mfue wote, au atapenda mfanye kazi pamoja. Ikiwa umebeba au amebeba mzigo wowote ataomba akusaidie au umsaidie.

Aina hii ya mtu kwenye mahusiano hana mpango wa maneno yako ya hamasa, hatokudai muda wa faragha, na wala hatokuomba zawadi. Ila furaha yake ni kukusaidia na wewe kumsaidia katika shughuli za maisha yenu ya mahusiano.

Lugha ya mguso au kugusana.
Ni aina ya mtu ambaye lugha yake ya mahusiano ni anapenda mgusane au mshikane. Aina ya hii ya mtu unapokuwa nae karibu atapenda umkumbatie, umpigie busu, umshike mkono haijalishi mpo kwenye maeneo gani. Usipofanya haya mambo kwake, yeye atayafanya kwako.

Mfano:- Ikiwa mmekaa sehemu fulani mmetulia utaona anakushika, anakuegamia, anakukumbatia. Kuna wakati wewe utahisi anakukera, lakini kwa yeye ndoo furaha yake na ndio Lugha yake ya mahusiano..

Lugha hizi 5 ikiwa utazifahamu vizuri, na ukaijua lugha ya mpenzi wako vizuri kabisa, na wewe ukamfanyia hivyo utapunguza vyanzo vya ugomvi katika mahusiano yenu.

Ili kugundua Lugha ya mpenzi wako Angalia nini anapenda kufanya mara kwa mara, na nini anapenda kulalamika asipofanyiwa.
 
Back
Top Bottom