Ludovick Uttoh ni Ndumilakuwili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ludovick Uttoh ni Ndumilakuwili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, May 29, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Imekaririwa katika vyombo vya habari kuwa Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na mashirika ya umma Bw. Ludovick Uttoh kuipongeza serikali pamoja na Spika Anna Makinda kwa kutekeleza maazimio ya ripoti yake kwa kuwaachisha kazi mawaziri 8. Kinachoshangaza ni kuwa Uttoh anaipongeza serikali kwa lipi? Anampongeza Anna Makinda kwa lipi? Hiyo serikali ndiyo iliyopata kigugumizi kuwachukulia hatua hao mawaziri wabadhilifu hali iliyomfanya Waziri Mkuu kuonekana kioja kwa kuwaita waandishi wa habari usiku wa manane Dodoma na kushindwa kusema alichowaitia. Hata mkuu wa nchi kuna taarifa (siwezi kusadikisha) aliposikia wabunge wa CHADEMA na baadhi kutoka vyama vingine vya upinzani (John Cheyo hakuwemo) pamoja na Wazalendo Mh. Filikunjombe na Lugola wamechachamaa na wanadai kuwajibishwa kwa mawaziri wabadhilifu mkuu alisema huo ni "upepo tu wa kisiasa utapita". Uttoh anampongeza Anna Makinda ambaye alijitahiti kadri ya uwezo wake kuzima vuguvugu la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu mpaka kufikia hatua ya kutamka zoezi la kusaka saini za wabunge lililoendeshwa na Zitto ni batili. Huyu ni wa kupongezwa?? Uttoh tafadhali fanya kazi yako, usianze kujipendekeza kwa kuwasifu viongozi walioshindwa kuchukua majukumu yao mpaka pale nguvu ya umma ilipoingilia kati. Usitake umma uamini kuwa unachokisema ni kuona aibu kwa kuwavua nguo hao mafisadi na sasa unataka kujikosha kwao.
   
Loading...