Cardinal06
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 963
- 327
Waziri Mkuu zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya kuwanyonga wauaji wa albino.
Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya kumfikia.
Rais Kikwete alisema hayo wakati wa ibada maalumu ya kuwekwa wakfu Askofu Liberatus Sangu kuwa Mhashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga.
Hata hivyo, jana Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi katika kampeni ya matembezi kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yaliyoandaliwa na Klabu za Mbio za Pole ya Temeke na kushirikisha vikundi mbalimbali vya Dar es Salaam, alisema: Ninampongeza Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukemea mauaji ya albino. Pia, nimesikia kuna watu sita wametakiwa kunyongwa lakini kwa maelezo ya Rais hukumu hizo hazijamfikia, hivyo nawaomba mfanye msukumo ili Rais asaini.
Kutokana na kukithiri mauaji hayo, Lowassa aliiomba Serikali kuunda kamati maalumu itakayokuwa ikichunguza mauaji ya walemavu hao bila kutegemea kamati za mikoa ili kuongeza ufanisi wa kuilinda jamii hiyo.