Lowassa: Wanaotakiwa kuwajibika wawajibike

Anasema anataka vijana wa ccm wanaomsema waendelee kwani hata yeye alipokua kijana alizani tatizo ni wazee
 
Aweke majina yao hadharani ili kumshinikiza msanii. Hawa hawatakosa kwenye list hiyo. Ngeleja, Malima, Mkullo, Ndullu, Utoh, Edward Hoseah, Jairo......
 
Lowasa kaazisha gazeti la JAMHURI ili litumike kumpigia debe kuelekea uchaguzi 2015.Deo Balile dhambi hii ya kuwatumikia mafisadi itakuandama hadi kaburini.
 
Lowasa kaazisha gazeti la JAMHURI linalosimamaiwa na Deo Balile ili litumike katika mbio za kuelekea 2015.Kazi kweli kweli
 
Huyu bwana hakujiuzulu kwa kuwajibika kwa yale yaliyofanyika. Yeye mwenyewe alisema kwamba ana-grant wish ya wabaya wake waliokuwa wanautaka uwaziri mkuu. Maelezo mengine yote ni unafiki.
 
Yaan kimsingi ni kweli jamaa keshaona wenzie wamekomaa na inawezekana kabisa kila akiwashtua hawa-respond kwa hyo anataka kumwaga ugali, mbeleni atawataja tu mi nakwambia tena hvi karibuni maana wakati wanyuma alisha mpigwa kwala swahiba wake kwamba akiamua 2015 haviki akiwa rahisi ndo yanakoelekea haya.
 
huyu jamaa atakufa kwa stress namna hii..urais ni kazi ngumu katika nchi masikini sasa akitumia nguvu zote na hela zote kutimiza hizi ndoto zake itakua ni tatizo maana yake itabidi apumzike na kurudisha nguvu na hela alizopoteza kuupata huo urais...hatari....mungu inusuru Tanganyika yetu
 
Lowasa ataka viongozi wanaotuhumiwa wajiuzulu
Send to a friend
Saturday, 10 December 2011 09:13
0digg

lowassa-top2.jpg
Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa

Raymond Kaminyoge WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amewataka viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali nchini wawajibike kama alivyofanya yeye alipoachia ngazi wakati wa sakata la Richmond.

Lowassa alijiuzulu mwaka 2008 kutokana na kashfa ya mkataba wa Richmond, baada ya kamati ya Bunge kubaini ukiukwaji wa taratibu za Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kumtaka apime mwenyewe uzito wa sakata hilo. Alifafanua kwamba, uwajibikaji ni moja ya uamuzi mgumu ambao viongozi wanapaswa kuchukua kwa maslahi ya wananchi.

Lowassa alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), kuhusu tathmini yake ya miaka 50 ya Uhuru. Mbunge huyo wa Monduli aliulizwa swali kuhusu baadhi ya viongozi kushindwa kuwajibika kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu Julius Nyerere licha ya tume kuundwa na kutakiwa wafanye hivyo.

Akijibu alisema, “kumbe mimi ni mfano mzuri? Basi nawashauri viongozi waige mfano wangu,” Uamuzi mgumu Alipoulizwa huwa anamaanisha nini kuhusu kauli zake za kufanyika uamuzi mgumu, alisema, “hilo sitaki kulizungumzia tena maana nilivyolizungumza nilipata maadui wengi”.

Lakini, akasisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuchukuliwa uamuzi mgumu na kwa wakati muafaka bila kuogopa. “Watanzania wananielewa ninaposema kuhusu uamuzi mgumu, ni lazima tuamue na kwa wakati bila kuogopa vinginevyo nchi itaendelea kubaki nyuma,” alisema. Lowassa aliongeza, “ bila kuchukua maamuzi magumu na kwa wakati treni itatuacha na hatutakuwa na njia nyingine ya kusafiri unajua treni ikishakuacha ndiyo basi”.

Madini Akizungumzia kuhusu malalamiko kwamba licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa ukiwamo wa madini lakini bado iko nyuma kimaendeleo, alisema ingawa kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu sekta ya madini, kinachotakiwa kufanyika ni kuangalia upya sera na sheria za nchi.

Alisema badala ya kuwatukana wawekezaji wa madini ni vizuri kama taifa likafanya marekebisho ya sera na sheria ili madini yaweze kuonekana na manufaa. “ Tunawahitaji sana wawekezaji kwa maendeleo ya taifa letu, tusiwatukane kwani haitatusaidia badala yake tuangalie miongozo yetu,” alisema Lowassa. Umeme Akizungumzia nishati ya umeme, alisema ili uchumi uweze kukua kwa kasi, sekta ya umeme ni muhimu kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda.

Alisema ingawa serikali iliwekeza katika umeme wa nguvu ya maji, juhudi zinatakiwa kufanyika ili kuwekeza zaidi katika vyanzo vingine vya umeme. “ Umeme wa kutumia mafuta una gharama kubwa, serikali ijikite zaidi kwenye vyanzo vya maji, gesi na upepo kwa kuwa gharama zake ni ndogo,” alisema.

Lowassa aliongeza, “ Tanesco wanapandisha bei ya umeme kwa sababu ya kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta, wasipopandisha bei watashindwa kujiendesha, tutakaa gizani.”
Alisema njia pekee za kuondokana na adha ya kupandishwa kwa bei ya umeme ni kwa serikali kuwekeza kwenye vyanzo vingine. Muungano Lowassa alisema hakuna kitu cha kujivunia katika medani za kimataifa kama ulivyo Muungano wa Tanzania.

Alisema pamoja na kuwepo kwa kero za muungano ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na watu, bado muungano huo ni wa kujivunia. “ Mimi najivunia sana na kuupenda muungano. Zipo kero za muungano na kuna vyombo vinavyoshughulikia kuzimaliza lakini kuna mambo mengi ambayo watanzania wananufaika na muungano,” alisema.

Akifafanua zaidi, Lowassa alisema hivi sasa watu wa pande mbili za muungano wanaweza kuishi na kufanya kazi mahali popote Tanzania bila kuulizwa na yoyote. Lowassa alitoa mfano akisema sasa hivi wapo Wapemba waliopo maeneo ya mbali ya Tanzania bara na wapo Wabara ambao wapo Zanzibar na kuhoji, kama muungano utavunjika hao watakwenda wapi. Alisema muungano wa Tanzania ni wa pekee kwani zipo baadhi ya nchi barani Afrika zilithubutu lakini zikashindwa.
 
Wanasiasa bwana huwa wanafikiri watu ni wajinga. Huyu huyu wakati ni waziri mkuu alitwambia uchumi unapaa, leo yuko nje ndo anaona kwamba treni lauchumi linatuacha! Disgusting.

Hao watuhumiwa wa ufisadi wenye tuhuma ni pamoja na huyo aliyetutajia (kwenye kikao cha NEC kilichoisha) akimuuliza kwa nini anasakamwa peke yake wakati alimhusisha kila hatua? Hapa kweli hapa ni lazima tufe maji wote.
 
Ama kweli kweli mambo karibu yataiva. Ngoja ntarudi na mchango mpya maana bila shaka kabla ya mwaka 2015 yatakuja mengi.
 
Eg
....Mafisadi wote wanatakiwa kujivua gamba ndani ya chama wasipofanya hivyo chama kitawavua kwa nguvu...........hili tunalisubiri ingawa tunaweza tukangoja milele bila mafanikio.

....Je, hawa wanaotakiwa kuwajibika wasipo wajibika ..... nini kifanyike dhidi yao???
 
Back
Top Bottom