Lowassa: Tutachukua jimbo la Arusha kama uchaguzi ukirudiwa!

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Lowasa akiongea kwenye uchaguzi wa mwenyekiti, amewapa Salamu Wapinzani kuwa uchaguzi ukirudiwa Arusha watalichukua jimbo Mapema iwezekanavyo. Chadema walitumia udhaifu wao kulichukua jimbo.

Wapinzani wanapata kichwa na Maandamano, mikutano mikubwa lakini hawaiwezi CCM, CCM ina nguvu ya Umma, angalia uchaguzi wa Viongozi tu nchi nzima ilitetemeka.

CCM ni chama chenye NGUVU KUBWA.

Source: Radio 5
 
Wape maneno,wape maneno babaaaa kwa hakika uchaguzi unavyoendlea ndani ya c.c.m nakubaliana na sofia simba kuwa we ndio mwanaume pekee ndan ya c.c.m,lowasaaaaa bhaaaaaaaassssss
 
Ameshakuwa msemaji wa chama.Mbona siku hizi anasikika kuliko Nape na Mukama.
 
Walisema CCM ikisimamisha mgombea na CDM wakisimamisha jiwe, watapigia kula Jiwe..!!! Arusha siyo pwani bwana EL..!
 
Hivi alishapona maradhi yake? prof wake anasema macho yake yapo sawa ama? maan inaonekana ugnjwa umemzidia
 
Kweli Mgema akisifiwa sana tembo hulitia maji.

Baada ya Lowassa ''kuwanyoa vipara'' Sitta na Membe kwenye chaguzi za ndani za CCM, sasa anatamba kuwa anaweza kuwashinda Chadema Arusha mjini!!

Naona huyu mmasai anatupia jiwe kwenye mzinga wa nyuki, wale jamaa wa people's power hawanaga mchezo watamnyoa zile mvi kwa mikono!!

Namshauri kwanza apime upepo wa marudio ya uchaguzi wa daraja mbili halafu ajiulize je CCM ilishindwaje Arumeru Mashariki?
 
Ni kweli nchi ilitetemeka kwa chaguzi za ndani za ccm kwa kukwapua pesa za mishahara ya watumishi wa serikali na kupandisha bei ya mafuta ili kupata fedha za kulipana posho za kuendeshea vikao vya ccm
Mzee EL hujajua tuu kwamba hata wewe mwenyewe unazungukwa ndani ya ccm na mwisho wako utakuwa mbaya sana wakati ccm inazikwa na nchi kuchukuliwa na upinzani.
 
Lowasa habari yake kwisha zaidi ya Monduli hakubaliki kwingine hata Monduli siyo 100%
 
Kuna mijitu mingine inaudhi sana. Yaani inataka kutuendesha kama yenyewe ni miungu watu. Yaani kutudhulumu itudhulumu bado itucheeeke kwa unafki. Watz tushtukage mapema jamani.
 
Back
Top Bottom