Lowassa the 5th president

Lowassa the 5th president

Mfilisti

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
3,727
Reaction score
19,465
jiandaeni wale wana UKAWA na watanzania wote kusherehekea kutangazwa kwa raisi wetu wa awamu ya tano Hon. EDWARD NGOYAI LOWASSA
 

Attachments

  • 1445920428415.jpg
    1445920428415.jpg
    7.8 KB · Views: 379
  • 1445920468788.jpg
    1445920468788.jpg
    55.8 KB · Views: 896
  • 1445920508734.jpg
    1445920508734.jpg
    18.3 KB · Views: 866
LUBUVA anatumika vibaya, ila waungwana tunafahamu LOWASSA ndiye mshindi.

Kitendo cha mwenyekiti wa NEC kuanza kutangaza zile sehemu MAGUFULI anazoongoza ni mbinu ya kuwakatisha tamaa wanamabadiliko!

Unajidanganya mkuu! fatilia vzr kanda ya ziwa utashangaa na roho yako,majimbo mengi yanavyoenda ccm ndo rais wa ccm anavyochanja mbuga.mwaka huu hakuna kuibiwa kura,nilichokiona Nyamagana na mimi mwenyewe nimekua mpiga kura jimbo hlo,hakuna ujanja ujanja mwaka huu,alopigwa kapigwa tu
 
MUNGU AMESHAWAFUNULIA WATUMISHI WAKE VIONGOZI WATAKAOTAWALA NCHI YETU KATIKA AWAMU YA TANO.

Tulia usome na uelewe.
Mungu uyafahamu majira na nyakati na viongozi wanaotawala katika nyakati hizo.

Imeandikwa "Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake" -- (AMOSI 3:7).

Maombi yetu hayatufanyi tuweke kiongozi tunayetaka bali maombi yetu hutusaidia kumpata aliyekusudiwa na Mungu, soma MATENDO YA MITUME 1:23-25 ("wakaweka wawili, Yusufu aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya, kisha wakaomba wakasema, wewe Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuoneshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili....wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya naye akahesabiwa kuwa pamoja na Mitume kumi na mmoja").

Kura ni mfumo ambao Mungu amewapa wanadamu kumpata kiongozi ila tunapaswa kufahamu kuwa hukumu (maamuzi) ya nani awe kiongozi huwa katika uwezo wa Mungu.
Soma MITHALI 16:33 ["kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini maamuzi (hukumu) zake zote ni za Bwana"]. Hii inamaanisha kuwa kura Mungu ameamuru ziwepo kama njia ya kufikia mpango wa Mungu lakini tayari Mungu huwa tayari anamfahamu kiongozi ni yupi.

Tangu mwanzo Mungu aliwatumia watumishi wake kuyasema mapema yatakayotokea katika uongozi na viongozi watakaotawala hata kabla haijatokea(Daniel 11:1-4)

Hii si mara ya kwanza mimi kuandika haya bali niliwahi kuandika haya mwezi wa saba na mwezi wa nane mwakaa huu, katika unabii nilioandika awali japo ulikuwa katika mafumbo makubwa ila ulielezea nani atakuwa Kiongozi mkuu wa nchi hii. Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi mkuu ninayaandika haya kwa aina nyingine ili uelewe na yatakapotimia ujue yupo Mungu wa Israel ajuaye majira na nyakati.

KWA MARA NYINGINE NALIONESHWA MAONO HAYA.

Naliona pepo (wind) zikizuka katika nchi na kuelekea nchi nzima, lakini pepo mbili ndizo zilikuwa na nguvu sana kuliko nyingine sita (6). Mmoja ulitokea Ziwa Victoria na mwingine ulitokea mlima Meru.

Pepo hizi zilipata nguvu zaidi kila zilipovuma kila kona. Naliona miti mingi bara na visiwani ambayo ilifurahi kwa sababu ya pepo hizo, jinsi zilivyovuma zilionekana kushindana pale zilipokaribia miti ili kupata upepo utakaovuma katika miti.

Kisha nikaona upepo uliotokea kanda ya ziwa ukipata alama nyingi za kukubalika siku ya kwanza ya uchambuzi wa alama kiasi kwamba ilisikika kila kona upepo huu utatawala miti ile. Ghafla siku ya pili ya uchambuzi wa alama za kukubalika, upepo unaotokea mlima Meru ukapata alama zaidi na kuishangaza miti mingi, japo nguvu yake kubwa iliongezeka kutoka kwa miti mingi ya visiwani. Miti hii ya visiwani iliokoa na kuongeza zaidi alama za upepo uvumao kutoka Mlima Meru. Kisha nikaona malaika akiandika alama katika ubao na hesabu yake ilikuwa mikono kumi na mmoja na nyongeza ya nukta kadhaa.

Naliona utata ukitokea katika kuwekwa wazi kwa alama hizo lakini baada ya msuguano Mungu aliingilia kati, kisha nikaona miti ikishangilia sana kwa sababu ya upepo utokao mlima Meru. Haikuwa rahisi alama hizi, mikono kumi na mmoja na nyongeza ya nukta kadhaa kuwekwa wazi lakini Mungu aliingilia kati na nikaona ubaoni andiko hili (MITHALI 16:31).

Mwisho wa maono.

Mungu ibariki Tanzania:
Naiombea Tanzania amani itawale na haki itawale kwa jina la Yesu. Amen

Apostle Mtalemwa Dionis
Kwa maulizo +255766247455
 
waliahidi goli la mkono saaizi wanatekeleza tu.
TUTAZAA NAO
 
Unajidanganya mkuu! fatilia vzr kanda ya ziwa utashangaa na roho yako,majimbo mengi yanavyoenda ccm ndo rais wa ccm anavyochanja mbuga.mwaka huu hakuna kuibiwa kura,nilichokiona Nyamagana na mimi mwenyewe nimekua mpiga kura jimbo hlo,hakuna ujanja ujanja mwaka huu,alopigwa kapigwa tu


Yericko anasema kutokana na majumulisho waliyoyafanya kutoka kwenye form za mawakala wa vituoni nchi nzima ikwemo kanda ya ziwa ambayo ni ngome ya ccm. Wewe unabisha kwa takwimu zipi za jumla? Kumbuka hadisasa ni majimbo 27 tu yametangazwa kati ya 260* na magufuli anaongoza kwa margnin dogo sana. Unaimani gani kwamba kura hazitasawajika?

Acheni kulazimisha ushindi kwa hasira.
 
Kijipa matumaini ni jambo zuri lakini sio katika mazingira kama hayaa Magufuli ndo Rais wetu.
 
Mzee lubuva anatumika kwa hakika, pale aliposema watu wakae 200mtr, matokeo ya yabandikwe vituoni hii ni hali harisi kuwa kila kitu kipo wazi na wananchi wana matokeo yote ya uchaguzi mpaka sasa, iweje mzee wetu aanze kutumika?

Dar ipo mdomoni mwa tume lakini ndiyo mkoa ambao mpaka sasa bado kutangazwa jimbo hata moja why? Matokeo yake yanatangazwa matokeo ya pemba eti kwa sababu mh. Edward kashinda kwa kishindo!.

Lakini kutumika huko kwa mzee lubuva ni pamoja na kuruka ruka na kutangaza matokeo yanayoonesha ccm inaongoza ili kuwadhoofisha wale wa ukawa kwanza na baadaye lile goli lipatikane, kazi ipo!!.
 
Hawa hawa kina Yericko Nyerere ndo walitangaza kuwa Slaa 2010 alishinda, baadae hawa hawa wakatuambia wameamua kumpitiasha Lowasa kwakuwa Slaa asingeweza kushinnda, wkt ukiangalia kuanzia 2010 CDM ilikuwa imeongezeka sana mvuto lkn pia kuwepo kwa muungano wa UKAWA kulikuwa kumeongeza nguvu zaidi, sasa mtu aliyekuwa ametoka kumshinda the serving president ktk mazingira niliyoyataja hapo juu angeshindwaje kushinda Magufuri, wanachokifanya hawa watu ni kutaka tu kuwasababishia watoto wa wanaume na wanawake wenzao matatizo, kata na ubunge inaonyesha CCM imeshinda sehemu nyingi, na kwa nature ya watanzania uwezo wa kuchagua tofauti ni mdogo, ndo maana waliposhinda kata nyingi CCM AU CDM unakuta pia na ubunge wameshinda, kitu ambacho kitakuwa hivo hata kwenye urais, LOwassa hadi sasa anamajimbo 10,mengi ni ya Pemba ambayo yana kura 6000 au 7000, Magufuri anaendelea kumtusua, yaani CDM hamjatoboa kabisa ile mikoa royal kwa CCM, kibaya zaidi kanda ya ziwa CCM na Kigoma
wametusuwa, and mind you miaka yote kanda ya ziwa inaamuaga, kwahiyo labda mnazungumzia urais wa Arusha hapo sawa.
 
jiandaeni wale wana UKAWA na watanzania wote kusherehekea kutangazwa kwa raisi wetu wa awamu ya tano Hon. EDWARD NGOYAI LOWASSA

Hiyo Tweeter ya Regina inasomeka tarehe 25 October saa tatu PM wakati mda bado sana au mkoani kwao... sasa iweje awe happy na results so far..

Mabadiliko Bado Sana Tanzania... Muungeni mkono Magtufuli tu atawaletea Mabadiliko Trust me....

Long live our Nation
 
Haya ni majira ya Lowassa, 2015-2020 Edward Lowassa rais
 
Tarehe 25 saa 3 asbh anasema we are happy with the result? Au result za wale vijana 161?
 
Back
Top Bottom