MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Lowassa ana kila haki kutafuta haki yake katika hili jambo. Nimekuwa nikiwaeleza hapa jamvini toka mwanzo kwamba Lowassa alionewa katika hili suala, hakupewa muda kabisa wa kujieleza mbele ya tume ya Mwakyembe. Tume ya Mwakyembe ilikuwa na madaraka ya kumuita mtu yeyote bila kujali cheo, rangi, kabila wala mali kwani ilipewa mamlaka hayo na Mkuu wa nchi.
Kwanini tume Iliweza kuwasikiliza na kuwatembelea watuhumiwa wote isipokuwa Lowassa?. Jamani huwezi kumuhukumu mtu bila kumsikiliza ama kumpa nafasi ya kujieleza. Na ningeomba muelewe kwamba uzuri wa shillingi ni kuiangalia pande mbili na wala si pande moja. Welldone Lowassa.
kwa kweli i hope.. TBC watawapa kina Mwakyembe nafasi ya kujibu hoja zao.. kwani bado anaamini kuwa suala zima lilikuwa ni "Uwaziri Mkuu", na anasema aliwajibika kwa makosa ya watu waliochini yake na kuwa yeye yuko "clean"
Na anaamini ilikuwa ni suala la uwaziri kuu wa lowassa
..Lowassa is right hakutendewa haki...wekeni ushabiki kando....kauli ya Mwakyembe ya kumtaka achague mwenyewe ..wakati wanajuwa hawakumuhoji ilikuwa ya kiuonevu.....kama hawakumuhoji hawakuwa na haki ya kumuambia aamue hatima yake!!!
Lakini lazima mjue Lowassa aliokoa serikali nzima ya Kikwete kuanguka...kama angeng'ang'ania madaraka tulikuwa tunaelekea kutokea uchafuzi wa hali ya hewa.......wanamkakati wapinzani wa Kikwete ndani ya chama kwa kujua kuwa Lowassa ndie alikuwa robot ya mtandao ....lengo lao lilikuwa kuangusha serkali ya Kikwete na kufanikiwa kujiuzulu kwa Lowassa ...lengo lilikuwa ni kuidhoofisha serikali ya Kikwete......
Naafikiri Kikwete na Lowassa ...they could achieve more together than what is claimed to be achieved today.....Lowassa anamjua vema Kikwete na udhaifu wake na alikuwa akiweza vema kuziba nyufa...ndio maana ....serikali ya Kikwete iliweza kuvuka ile miaka miwili migumu ya mwanzo....na bado wakaweza kujenga shule kila kata.............
Tusiwe wachoyo wa fadhila ......kwa kikwete na lowassa...as a team...
Ukiangalia kwa sasa kikwete anapwaya kwa sababu bado PINDA Hajamudu kuelewana vema ni Kikwete kikazi..... Pinda ni conservative ....civil servant, wakati Kikwete ni chakaram....sasa ukizingatia tena Shein ana sifa kama za Pinda .....basi kidogo imeleta gap......i mean wasaidizi wa rais mpole kama JK .....wanatakiwa wawe na ushawishi mkubwa .....na nguvu ya kisiasa....
Check your facts!!
watanzania mmelishwa nini? Heri sisi huku UK
WanaJF mliopo Nyumbani, kwenye maojiano na TBC1 , Mh.waziri mkuu mstaafu kasemaje kuhusu rich mond?
watanzania mmelishwa nini? Heri sisi huku UK
PM..
a. kwanini Lowassa hakutoa hoja Bungeni siku ile asubuhi na kutaka Bunge liahirishwe ili aweze kupitia hoja za wabunge zilizotolewa jana yake na kutoa majibu?
b. Kwanini hakutoa hoja kuishutumu kamati teule kuwa haikumpa nafasi ya kujitetea na kuomba Spika ampe muda mbele ya Kamati hiyo iweze kumhoji kabla haijachukuliwa hatua nyingine?
c. Kwanini Lowassa baada ya kuona Bunge limegawanyika hakutoa utetezi wake wa kile alichokifanya/kutokifanya kuhusu Richmond na baadaye kutaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye?
d. Kwanini licha ya kutoitwa na Kamati Teule, Lowassa hakujitetea mbele ya Bunge ambalo ndilo lilikuwa na nguvu na lina nguvu kama Kamati Teule kwa mujibu wa Kanuni za Bunge? Kwa kukataa nafasi yake ya kujitetea mbele ya Bunge (aidha kama Bunge au kama Kamati) yawezekana alijinyima yeye mwenyewe nafasi ya kujitetea aliyoiomba na kupewa?