Lowassa ni taasisi isiyo rasmi

Lowassa ni taasisi isiyo rasmi

Myelife

Senior Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
164
Reaction score
107
Ndugu watanzania wenzangu,

Kuna habari nyingi sana kuhusu Mh Ed Lowasa, tangu mwaka mmoja na nusu uliopita kawa gumzo sana hapa Tanzania, hii ni kwakuwa ni mwasasiasa mkomavu/ mkongwe na pia mvumilivu sana.

Kuhusu ufisadi sina ushahidi wowote juu ya hili kwa hiyo namwachia yeye na Mola wake, mimi kama binadam ningepata ushahidi ningeweza kusema jambo, au kama mitambo ya Dowans ingetaifishwa pia ningeweza kuwa na maswali hasi juu yake, na ndiyo maana namwachia Mungu.

Suala la matumizi ya fedha na utajiri wake, tunamhukumu bure kwani A. Chenge angeanza kuhukumiwa kabla ya ED Lowassa ningeona kuna mazingira salama katika mchezo lakini pia ni nani anaependa umasikini?

Mimi nina mtizamo wa kiliberali, napenda kuwakumbusha pande zote mbili za CCM JK na CCM Lowassa kuwa, CCM wanapaswa kujua sasa vita hawapambani na Lowassa kama mtu bali wanapamba na Lowassa kama Taasisi hatarishi katika karata yao, hii nina maana kama itatokea ED Lowassa akaihama nchi leo taasisi hii itaendelea kubaki nchini na kuwa kama kansa itakayoendelea kuwatafuna CCM, hivyo wanapaswa kuiheshimu na kubadili mbinu ya vita.

TeamLowassa nao wanapaswa kujua kuwa wao sasa ni kama taasisi wanapaswa kujipanga kwa spidi ya kijeshi, waache kutoa matamko kila mara, na pia wao ndiyo wanauwezo wa kuamua kwa sasa chama kipi wakipe ushindi, kama wanataka kuvuka mstari wakati ni sasa, maana wakichelewa watachelewesha ushindi katika chama chochote, ila kama hawajaamua kuvuka mstari wajue wanaweza kuondoka katika siasa kwa kipindi fulani kwani teamLowassa ni ngumu kunusa au kulamba hata udiwani kwani watakuwa na kashfa ya kukiyumbisha chama.

Hivyo nawashauri kama hawavuki mstari kwenda chama kingine hata form ya udiwani wasichukue. ila kama wanataka kuendelea kuwepo katika siasa wafanye mara moja. pia teamLowassa hii isiwe na unafiki uliopitiliza wa kusema maneno mabaya kuhusu CCM hali ya kuwa wanaendelea kuzimiliki kadi za CCM.

Tungependa kuona watu wafanye wanachosema na siyo kuendelea kuongea wakiwa katika kivuli cha wapenda mabadiliko hali ya kuwa hawana meno yoyote katika chama.
katika taasisi hii kuna mkakati mmoja utakuwa unapikwa lakini ni lazima wajue muda si rafiki tena.

Pia wasiogope kwenda vyama mmbadala na pia vyama mmbadala wasisite kumpokea yeyote, kwani kabla ya kiongozi yeyote kumkatalia Lowassa uanachama anapaswa kujiuliza, je yeye hajawahi kuhama chama au ameshawapokea wanachama wangapi kutoka vyama vingine na ndiyo atoe maamuzi.

wamarekani wana msemo wao, "America has no permanent enemy but permanent interest" katika siasa husema hakuna adui wala rafiki wa kudumu katika siasa.

Karibuni wanajamvi.
 
I made a part of that fizzled bomb and, I can promise you, IT'S REALLY FIZZLED AND DIFFUSED! JUST A MATTER OF TIME!
 
Rafiki yangu Mmoja alikuwa akichukuwa form ya Kugombea ubunge kupitia CCM alichonieleza ni kwamba "ndugu yangu CCM ni rushwa kila mahali, Kama hauna fedha hautapitishwa, lazima utoe rushwa kwa Katibu wilayani lazima uhonge kwenye mashina na pia mkoani.;na hii rushwa inatplewa kwa ustadi mkubwa Sana"

Hapo ndipo ninapo iona CCM ni habari. Lowassa nafikiri alipanga kuinyoosha haya maovu ya CCM Bahati mbaya wakamshutukia haraka yangu akiwa Waziri mkuu wakamuundia zengwe wamtoe asije akawahaaribia ya kwao.

Wengi wa wana CCM wanasema yupo kwenye siasa kufanikisha dili zetu. Hii ni hatari sana kwa taifa changa Kama Tanzania. Tutakapo fanikiwa kupigana na rushwa kwa vitendo Kama alivyokuwa anafanya Lowassa nchi hii Leo ingukuwa mbali.

Mfano kuzembea kwa mtumishi wa umma kazini ni sura ya rushwa, kutoa kibali kujenga maghorofa marefu osterbay na Masaki kwenye makazi ya watu ni rushwa, kujenga majengo chino ya Kiwango huku manispaa wanaona ni rushwa, kuchelewesha maamuzi katika kuwapa watu haki zao ni rushwa, kujenga barabara chini ya Kiwango ni rushwa, kupunguza upana wa barabara kutoka 6.5 m to 5.7m ni rushwa.

Endeleeni tena kwa kazi zaidi kuishabikia CCM siku mmoja mtajikuta rasilimali zote zimeshaondoka. Tujitahidi tutafute mabadiliko yatatusaidia kutoka kwenye mfumo huu mmbovu wa CCM.

Haya yote yameasisiwa na...
 
Lowasa jembe ni mchapa kazi maccm yamemfanyia fitina
 
Kwa kweli kwa mtindo huu hatutafika popote ccm hizo pesa mnazo hongwa kwa kila kitu form za kugombea mhogwe ajira hivyo hivyo hamtosheki ni watu wa haina gani nyie
 
We we ni mchonganishi mambo yameshaanza kupoa unataka kuyapandisha chamsingi wakubali yaishe wajipange kwa awamu nyingine, nakubaliana na wewe uliposema kwamba Lowassa ni taasisi
 
Team lowasa ni hatari kwa siasa ya bongo nimeligundua hilo

Wangekuwa hatari wasingeshindwa kumpitisha mgombea wao, TeamED ni vidagaa vinavyo m surport Papa kwa hiyo vimemezwa kwa mkupuo na mapapa ya Kamati
 
needeseela

Lowassa hajawahi kupambana na Rushwa wa ufisadi na kibaya zaidi hajawahi kutamka kwa kinywa chake neno Rushwa au Fisadi.
Fisadi hawez kupambana na Fisadi,
kashfa ya Richmond ilikuwa ya ufisadi na Lowassa alijiuzulu kwa kuhusika moja kwa moja katika kashfa hiyo,.
Kama siyo fisadi why alijiuzulu yeye na siyo Zitto?
 
Last edited by a moderator:
Ni taasisi iliyopatikana kwa nguvu ya pesa sio nguvu ya mabadiliko..Watz tuna akili zakushikiwa sana.. Lowssa huyu huyu watu leo wanapiga vifua mbele nakusema hawaoni ufisadi wake kweli!!! Hivi na ufisadi wa Mhongo, Tibaijka, Rostm, AG mstaafu na Chnge kuna siku mtahoji uko wapi? Halafu lazima tujiulize inakuaje mtu anang'ang'ania kwenda Ikulu? Kama mtu hakuhusika kwa nini asiruhusu mahakama imchunguze ili tujue ukweli? Ukimya ndio jibu mnalofikiri mtu yuko safi?

Inakuaje mtu anatumia gharama kubwa eti kutoka kwa wafadhili ambao wengi wameifilisi nchi hii akiingia ikulu atawatumia wao au wananchi? mnajiuliza haya? Tuache ushabiki wa ukanda na kupenyezewa visent, nchi haihitaji mtu mwenye doa la ufisadi wala shaka la uhujumu uchumi tumechoka kutumiwa!!
 
Lowassa ndie ataamua Rais wa nchi hii, awe yeye au amsupoti yeyote yule ndie atakuwa Rais, ana pendwa na ana wafuasi wengiiiii sanaaaa, kushinda kwake au atakaye mpa supoti iko wazi....
 
Mkuu: Lowassa sio Taasisi isiyo rasimi, bali ni TeamLowassa ni CHAMA ndani ya CHAMA. Hiyo TeamLowassa sasa iko tayari kuimega CCM.

Haya yote ni matokeo ya udhaifu wa JK, kumuachia Lowassa kuanzisha CHAMA chake ndani Chama (CCM)

Ndani ya CCM Lowassa anao Wenyeviti wa mikoa > 20, Wabunge wa CCM >100, hawa wote ni wafuasi WATIIFU wa Lowassa na wako tayari kumfuata popote pale atakapokwenda hata kama ni ACT-wazalendo! (No disrespectful to ACT-Wazalendo)
 
Hiyo team Lowassa yote jana wamechukuwa fomu za kugombea ubunge kupitia CCM.
 
Shughuli imeishaisha Dodoma CCM wamemchagua Dr.Magufuli nyie endeleeni kujifariji na Lowassa.
 
Back
Top Bottom