kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Nina imani sana na kabila la kimaasai kwa utendaji kazi wao na kuchukua maamuzi ya haraka na yenye manufaa. Labda hii inatokana na aina ya malezi, makuzi na mafundisho wanayopewa ndani ya jamii yao yanaozingatia uwajibikaji na utoaji taarifa sahihi kwa ngazi zao za juu kwenye familia. Mgawanyo wa kazi (division of labour) na kuheshimiana (respect) ni miongoni mwa mambo ambayo jamii nyingi zinapaswa kujifunza kutoka kwa wamasai. Hawana matani wala kuchekacheka kwenye mambo ya msingi, ni wakweli na wenye msimamo usioyumba. Hata mtoto mdogo anaweza kufanya kazi ya kuchunga na kuhesabu ndama na mbuzi kwa usahihi kabisa.
Kila mtu alikunwa na sifa na uongozi wa Sokoine (rip) alipokuwa mtumishi wa serikali na waziri Mkuu, alikuwa kiboko ya uhalifu na wahalifu nchini hadi akawa tishishio hata kwa watendaji wenzake kwa speed yake ya kufanya kazi na kuchukia uzembe na wizi. Hatumchagui mtu kutokana na kabila lake tu, lakini ni kweli pia yapo makabila mengine ambayo yana idadi kubwa ya watu wavivu, waongo, wazembe, wapenda porojo na wasiothamini kazi. Wanafundishwa kucheza ngoma usiku kucha, kuoa na kuolewa mapema na kucheza bao mchana kutwa.
Lowassa ana sifa za kuchapa kazi, kuchukuwa maamuzi haraka na kuchukia umaskini, hizi ni sifa halisi (typical) za kabila za kimasai, sio za kujifunza tu darasani. Mmasai amefundishwa kuwa na mali (ng'ombe) nyingi, hivyo sishangai kusikia Lowassa kuwa tajiri ana asili navyo.
Huwenda Lowassa akafanana kiutendaji na mmasai mwenzake hayati Edward Moringe Sokoine, tena wote ni ma-edward