kwanza kabisa niwasalimu,
Lengo langu la kuleta uzi huu ni kumpongeza ndugu Edward Lowassa mbunge wa Monduli kwa haya yafuatayo,
Kwanza kabisa kuwasomesha baadhi ya watanzania wasio na uwezo,ndugu Lowassa amejitahidi sana kusomesha wanafunzi wengi sana wasiojiweza katika shule mbalimbali ikiwemo Manyara sec,Oltinga secondar,Makuyuni,Masai Girl na kujenga shule hiyo kwa kusaidia jamii ya kimasai kupata elimu.
Kasaidia si wamasai tu bali wananchi wa makabila mengne kwa kuwasomesha vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi na kufanya waweze kutimiza malengo yao.
Pili Lowassa amejitaidi sana kwa kipindi kifupi alichokua waziri mkuu kuboresha huduma mbalimbali kama barabara,maji,elimu na afya ukijaribu kuangalia kwa kipindi alichokua waziri mkuu hakukua na migomo ya hovyo kama sasa hivi iliyoko.
Tatu ndugu Lowassa yupo karibu sana na watu wake hata kufiki hatua ya kuwa na sherehe kila mwanzo wa mwaka kuanzia mwaka 1995 hadi sasa,embu jiulize ni wanasiasa wangapi wenye uwezo wa kuwa na upendo wa namna hyo kwa watu wao japo uchaguzi umesha?wengi wao wanaishia kupita na magari kama hawakupigiwa kura na wananchi wa hapo.
Pia ndugu Lowassa yupo karibu sana na walimu wa shule mbalimbali nakumbuka siku moja alikuja katika shule fulani akawakuta walimu wapya na aliwajua akawauliza majina wakamwambia akawasilimu,alikuwa na makamu wa rais siku hiyo nakumbuka.
Mwisho ni Lowassa ni muhudhuriaji mzuri wa kanisani na ni jambo zuri sana kwa mtu kuhudhuria katika nyumba za ibada kwa kuwa hakuna alie msafi
LENGO LANGU MIMI NI KUTAKA KUWAELEZA WATANZANIA KUWA MANENO NA VITENDO NI VITU VIWILI TOFAUTI, WANASIASA WENGI HAPA NCHINI NI WATU WA MANENO BILA VITENDO HASA HASA WA CCM ILA BWANA LOWASSA YUPO TOFAUTI.
Nieleweke wazi kuwa mimi ni mwanaCHADEMA ila sijafungwa katika chama bali nazingatia utendaji wa kazi na uadilifu tofauti na wengine wengi ambao akiwa chama hiki etI kumsifia wa huku ni dhambi.
MUNGU AKUBARIKI