YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,003
Binadamu waweza poteza kila kitu lakini kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa kuhakikisha kuwa hukipotezi kitu hicho ni heshima yako mbele ya jamii ya watu wote.Waweza kuwa huna mali wala cheo lakini ukawa na heshima mbele ya jamii kila mtu akawa anahitaji msaada wako nk
Lowasa na Sumaye walipoteza uongozi kwani si mawaziri wakuu tena,Wakapoteza pesa nyingi sana kwenye kampeni za kugombea uraisi ndani ya CCM na CHADEMA.
Sasa hivi wako mbioni kupoteza lulu pekee iliyobakia maishani mwao ambayo ni heshima mbele ya jamii yote.
Ushauri wangu walitakiwa wastaafu siasa wawe tu watu wa kushauri hapa na pale.Active politics kwao zinakwenda kumalizia lulu ya mwisho.
Jina Lowasa na Sumaye lilikuwa jina kubwa kila kona mtu kujisifia kuwa mimi ndugu yake LOwasa au Sumaye ilikuwa sifa kubwa na passport ya kuhudumiwa kipekee popote iwe sekta binafsi au umma.
Lowasa na sumaye wameharibia vizazi vyao majina .Wao walishakula vya kutosha na ma-uongozi ya kutosha ilitakiwa watulie walee heshima za majina yao kwa ajili ya vizazi vyao vilivyopo na vijavyo kama akina Mwinyi,Kawawa,nk
Hawajavitendea haki vizazi vyao. Walipostaafu siasa ilibidi watulie kama wastaafu kama wenzao ili kulinda heshima za majina yao.