juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,480
Nachelea kusema ni mikataba mibovu au la,,ila swali langu ni je hawa ambao leo tunawaona kama lulu ndani ya chama chetu CHADEMA(LOWASA na SUMAYE),ambao mimi binafsi sijawahi kuwa na love nao kwa sababu naamini hawakuja kwa sababu wanapenda upinzani bali walikuja kama sehemu ya kupata faraja baada ya kutoswa huko CCM.
Sasa leo najiuliza hivi sisi wafuasi wa CHADEMA tumeshawahi kujiuliza kwamba hawa watu wawili walikuwa wapi wakati hiyo mikataba ya madini inapitishwa?
Maana wakati huo wote wawili walikuwa ni wabunge na mawaziri na huyo mmoja alikuwa ni waziri mkuu,tena kwa miaka 10 mfululizo.je hawakuiona hiyo mikataba?najiuliza maswali haya baada ya kuona wafuasi wengi wa CHADEMA wameshupalia kwamba Magufuli alikwepo wakati mikataba hii inapitishwa,sasa je na hawa akina Lowasa na Sumaye hawakuwepo??
Nadhani ni muda muafaka wa hawa watu wawili kutueleza waTanzania ni kwa nini hawajawahi kutoa maoni kama hii mikataba haikuwa sawa? Najua kuna watu watawatetea kwamba huwezi kutofautiana na chama, lakini tukumbuke hawa watu mwaka juzi 2015 walipotoswa kwenye uraisi walitofautiana na chama hadi wakaja huku kupata faraja.
Tunaomba Mbowe na Lisu wawahoji Lowasa na Sumaye kwamba ilikuwaje walikuwa serikalini na walikubali tukasaini mikataba ambayo tunaaminishwa ni mibovu? Kwa nini hawakuwa tayari kuhama chama wakati huo kwa kutetea maslahi ya wananchi??