Lowassa na Sumaye lipeni msukumo mpya wazo la CHADEMA kuwa na media zake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Mh.Sumaye,baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa kikao cha kamati kuu cha(CC) nakushauri ukiwa kiongozi uliopewa heshima hiyo kubwa itumie vizuri kuchochea mabadiliko ndani ya CHADEMA na ningekushauri kwenye vikao vya chama uibue upya swala la chama kuwa na media zake(tv na gazeti la chama).

Halikadhalika,mh.Lowassa, nawe kwa nafasi yako kama mgombea wa chama katika uchaguzi mkuu uliopita, ni vizuri ukatumia heshima kubwa uliopewa kusaidia kujenga chama ikiwa ni pamoja na kushawishi viongozi wa chama waoene umuhimu wa chama kuwa na media zake.

Shirikini pia kutoa mawazo yenu ni namna gani chama kinaweza kupata fedha za kuanzishia media hizi.Chama kina hazina ya viongozi walio na upeo wa kutosha tu ila sometimes kinachokosekana ni nguvu tu ya ku-push mawazo/mambo mapya.

Nimekuja na wazo hili kwa nia njema tu ili 2020 tuingie kwenye uchaguzi tukiwa tumejipanga vizuri ili tuweze kukabiliana na nguvu ya CCM hasa katika matumizi ya media kwenye kufanya campaign.

Tujifunze kutokana na makosa,miaka mitano si mingi kama wengi tunavyodhani.Wenzuni wameshaanza campaign zisizo rasimi mapema sana.

Mh.Sumaye na Lowassa,atakaefanikisha wazo hili kati yenu atakuwa amejijengea legacy na heshima kubwa sana ndani ya chama pengine kuliko hata kuwa mgombea wa chama au kuteuliwa kuwa mjumbe wa CC katika chama.

NB:Wakati tunachelewa kutekeleza mawazo yetu haya,wapinzani wetu wanaweza wakachukua mawazo yetu haya hasa kuhusu swala la tv na wakawa wa kwanza kuyafanyia kazi na sisi tutakapokuja kuyafanyia kazi mawazo haya,watesema tumeiga kutoka kwao(kutuiga ni kawaida yao)
 
Wazo zuri sana hili, ila wawe waangalifu isije kuwa kama uhuru kazi yake ni kusifia tu Serikali na kuponda upinzani matokeo yake linaendeshwa kwa ruzuku au TBC ambayo inaendeshwa kwa ruzuku tu, vyombo hivyo viwe na habari zilizo balance kama mwananchi, majira, Tanzania daima na nipashe au itv
 
Mbowe anakula hidden Profit kuna Nyumbu wengi wakiona Tanzania daima au Mwanahalisi wanayanunua hata kama hakuna habari ya maana kwa lengo la kuchangia mfuko wa Chama hawajui kuwa kile ni kipeperushi binafsi cha Freeman na kingine ni cha freeman ila kinatangazwa cha kubenea kuficha umiliki sasa wazo la kuanzisha gazeti la chama ni kuwakorofisha kubenea,mbowe vs chama
 
Mbowe anakula hidden Profit kuna Nyumbu wengi wakiona Tanzania daima wanalinunua hata kama hakuna habari ya maana kwa lengo la kuchangia mfuko wa Chama hawajui kuwa kile ni kipeperushi binafsi cha Freeman sasa wazo la kuanzisha gazeti la chama ni kuwakorofisha kubenea,mbowe vs chama
Uhuru maoni sometimes ni shida!!
 
chadema TV ni story ilianza kitambo sana ! .. hakuna lolote
 
Kuna siku nilitumiwa clip ya Mbowe WhatsApp ikiwa na nembo ya Chadema media sijui nini ila ilisomeka kama inayomilikiwa na Chadema.
Anyways... Hili ni wazo zuri,nafikiri walengwa wakiamua kulifanyia kazi ni jambo dogo sana.
Nami ningependa kuona likifanyiwa kazi.
 
Lowassa hakikisha unafuga watu wa kamati kuu kama ulivyowafuga wale wa nec ya ccm, 2020 lazima ugombee tena, kama kuna vifungu vya kushindanisha wagombea hakikisha vyote vinafutwa.

Hizo media zikianza hakikisha ni wewe tu uwe unapewa promo na wala si chadema... " Lowassa mabadiliko, mabadiliko Lowassa" ndio iwe mbinu ya kukupromoti. Hakikisha ile kauli mbiu ya kushusha nguvu kwa wanachama isijirudie maana itakushusha ( ile ya peopleeees power).

Wewe Lowassa ni alpha na Omega hapa CDM......
 
Mleta mada nafikiri hii kitu unaijua kwa undani basi tu ulitaka kuwajambisha majipu fc,
lowasa hakuja cdm kimakosa wala sumaye wala kingunge wewe kama unataka kujua kuwa hakuja kimakosa muulize dr casava ana jibu tosha. Hilo swala mbona sio la kushauri tena? Mbona mikakati iko ukingoni kabisaa!!! Watajamba moshi majipu fc media zetu hasa tv ndo itakuwa habari ya mjini. Huwezi kukurupuka kufanya hilo jambo lazima utafute nguvu kazi inayojitambua. Stay tuned.
 
Mleta mada nafikiri hii kitu unaijua kwa undani basi tu ulitaka kuwajambisha majipu fc,
lowasa hakuja cdm kimakosa wala sumaye wala kingunge wewe kama unataka kujua kuwa hakuja kimakosa muulize dr casava ana jibu tosha. Hilo swala mbona sio la kushauri tena? Mbona mikakati iko ukingoni kabisaa!!! Watajamba moshi majipu fc media zetu hasa tv ndo itakuwa habari ya mjini. Huwezi kukurupuka kufanya hilo jambo lazima utafute nguvu kazi inayojitambua. Stay tuned.
Mkuu, sikuwa na taarifa yoyote juu ya jambo hili ila kwa muda mrefu nimekuwa nikitaka kuona jambo hili linatekelezwa ila kama liko mbion basi ni habari njema.Mimi ni shabiki wa CHADEMA ambae siko karibu na viongozi wa chama au watu wengine muhimu katika chama wanaoweza kunipa taarifa kama hizo.
 
Wazo zuri sana hili, ila wawe waangalifu isije kuwa kama uhuru kazi yake ni kusifia tu Serikali na kuponda upinzani matokeo yake linaendeshwa kwa ruzuku au TBC ambayo inaendeshwa kwa ruzuku tu, vyombo hivyo viwe na habari zilizo balance kama mwananchi, majira, Tanzania daima na nipashe au itv
Huwezi kupata mawazo mapya toka kwa Edward na Fredrick.Hawa ni "spent forces"/maveteran wa vita.
 
Back
Top Bottom