Lowassa na Membe acheni chama kifanye kazi yake

Lowassa na Membe acheni chama kifanye kazi yake

kitukuu_

Senior Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
160
Reaction score
68
Ni wazi watu hawa wawili ,edwad lowasa na benard membe wamekiumiza chama vya kutosha.watu wote hawa wawili wanapata msaada kutoka pande mbili tofauti,wakati lowasa anapata msaada kutoka kwa wafanya biashara wengi wenye asili ya asia wakiongozwa na makampuni makubwa kutoka mashariki ya mbali na marekani,membe yeye msaada wake upo kwenye taasisi za usalama za ndani. Ukweli ulio wazi ni kwamba iwapo ccm itaamua kuwaengua mafahari hawa wawili itakua imefanya mambo muhimu kama ifuatavyo
(1)kukatwa jina kwa lowasa katika mbio hizi za uraisi ,itasaidia kukiondoa chama katika mikononi mwa watu wachache na hasa wafanya biashara wenye asili ya asia na kukirudisha chama mikononi mwa wakulima na wafanya kazi,ndugu zangu watanzania mkubali msikubali leo hii lowasa akiwa raisi rostam azizi na marafiki zake wenye asili ya asia ndio watakao faidika na rasilimali zetu,leo hii wafanya biashara wameweka nguvu zao zote kwa lowasa kwa kumpa sapoti ya mabilioni ya shilingi,wafanya biashara hawa sio wajinga wanajua pesa zao zita rudi kabla hata hakuja pambazuka.

(2)kama lowasa akishika madaraka ya nchi hii wakati wake utakapo isha atahakikisha anamuacha mfanya biashara mwenzake katika kiti cha uraisi,kitendo hiki kitakua kuwatupa nje ya chama watu wote walio na uwezo na hasa waakulima na wafanaya kazi,lakini hali hii haita ishia hapo wenye chama na hasa wakulimawatakapo porwa chama,hawata kaa kimya ni wazi machafuko yatatokea nchini n njia pekee ya kuepukana na haya ni kuachana na lowasa ,lakini kuna hili la lowasa kujiuzulu kutokana na kashfa ya richmond ,baada ya lowasa kusomewa mashtaka yake na kamati teule ya richmond lowasa alipewa nafasi kujibu hoja tena angeweza hata kutumia siku nzima kujibu hoja akiwa kama waziri mkuu,lakini lowasa hakufanya hvyo matokeo yake aliamua kujiuzulu bila kujibu hoja,kwa watu wenye akili walijua maana ya lowasa kukataa kujibu hoja ,maana kama lowasa angejibu hoja ingeilazimu kamati teule kuja kuthibitisha yale Waliyo mtuhumu nayo lowasa ,lowasa hakutaka hilo litokee kwake ilikua ni afadhali kijiuzulu alafu kuja kulalamika nje ya bunge ,lakini kuna hili la bosi wake kutia saini barua yake ya kujiuzulu,hii inaonyesha bosi wake alilidhika na mambo yote yaliyosema juu ya lowasa,lakini tusisahau raisi anavyombovingi vya kumsibitishia kama aliyo tuhumiwa nayo lowasa ni kweli,kitendo cha raisi kuweka saini kimeondoa shaka yote na niwazi lowasa alihusika katiaka kashfa ya richmond.sasa swali la kujiuliza je kikwete na timu yake watatuletea lowasa kama mgombea kupitia ccm pamoja na yeye mwenyewe kama raisi kuujua uchafu alio ufanaya?

MEMBE :kuenguliwa kwa jina membe katika kinyan'ganyiro hiki kutasaidi sio tu kutuliza gathabu katika kambi ya lowasa lakini pia itavifanaya vyombo vya usalama kurudi katiaka mstari na kurudisha imani kwa wagombea wengine,
kwa vyovyote vile iwe edwadi lowasa au benard membe mmoja wao kati ya hawa akipata uraisi ccm itambue mpasuko katika chama hicho kikongwe hautaisha kesho wala miaka. Kumi ijayo,iliyo wazi ni kwamba lowasa na membe wana uhasama wa muda mrefu sana migutano yao ndani ya chama cha mapinduzi haikuanza jana wala mwaka jana ni kwamiaka mingi watu hawa wamekua na uhasama na hasa uhasama uliosababishwa na kupigania madaraka,huu ni muda muafaka kwa ccm kumaliza fujo zao ndani ya chama ,ni wazi lowasa na membe wamekiumiza chama kwa muda mrefu,watu hawa wanakoelekea wanaweza hata kutuletea machafuko nchini,njia pekee ya kuiponya nchi kutokana na fujo zinazoweza kuletwa na watu hawa ni kuwaengua wote katika kinyang'anyiro cha uraisi.

USHAURI WANGU KWA CCm
ccm ni taasisi kubwa na yenye. Hazina ya rasilimali watu,kitendo cha baadhi ya wagombea kukitisha chama kuwa wasipo chaguliwa watahama chama ni upuuzi mtupu,kinyago ukichonge mwenywe leo kije kukutisha hai wezekani,ni nani kati yao aliekuwa na nguvu kama mrema je mrema yuko wapi sasa.wanasiasa wote hawa wanaweza kuonekana wakubwa sana na wenye nguvu pindi wawapo ndani ya ccm lakini wakiwa nje ya ccm hawana nguvu yoyote na uzuri wa hili wanalijua wao na wapambe wao.

Ccm ambacho wnatakiwa kujua ni mtu wa namna gani wanatakiwa kumsimamisha kwa kipindi tulichopo ili apambane na mgombea wa ukawa ambaye bila shaka atakua dk slaa.pamoja na sifa zote ambazo ccm mtaziweka lazima mtu huyo awe na sifa hizi
(1) Awe msomi - dunia tuliyonayo sasaivi inahitaji msomi kukabiliana na changamoto
(2) Mchukia rushwa- Wananchi watataka mtu ambaye kwa historia yake anachukia rushwa na wala rushwa
(3) Mtu mkali - wananchi watapenda ccm imsimamishe mtu ambaye sio tu anatambulika kwa historia hiyo bali kiongozi ambaye atawachukulia hatua watumishi wote wazembe serikalini
(4) Asiye mfanya biashara wa aina yoyote ile
(5) Asiye na kashfa yoyote ile - ili iwe rahisi kumnadi
(6) Asiye na maamuzi ya pupa
(7) Mbunifu - anayeweza kuwa mbunifu wa mambo kulingana na changamoto zilizopo
 
Wakatwe mara ngapi? kama wakiuka maadili ya chama chako? Maadili ya Taifa utayaweza?
 
Ni vizuri kujiandaa kisaikolojia kwani hata vijijini sasa wanasema kuwa Raisi ajaye atatoka UKAWA!!!!
 
Mbona shughuli ya Membe imeshaisha leo
 
Hivi ndani ya ccm kuna wakulima, wafugaji na wafanyakazi hebu nitajie watu watatu wenye sifa hizo?
 
nmegundua pro CDM wanafuatilia kwa makini chaguzi za CCM...
 
Uchambuzi wako ni murua lakini tatizo linalozuka ni jinsi ya kumpata ndani ya ccm mtu mwenye sifa za uongozi ulizoziainisha!! Hakuna mtu ndani ya ccm mwenye usafi unaoutakiwa kwa kiongozi nchi yetu inayemuhitaji!!
 
Uchambuzi wako ni murua lakini tatizo linalizuka ni jinsi ya kumpata ndani ya ccm mtu mwenye sifa za uongozi ulizoziainisha!! Hakuna mtu ndani ya ccm mwenye usafi unaoutakiwa kwa kiongozi nchi yetu inayemuhitaji!!

Mimi nadhani kwenye upinzani ukimtoa Lipumba na Mbatia hakuna anayefaa na tunaomhitaji...
Ccm kina hazina kubwa ya wanachama na wapo wengi sana wanaofaa kutuongoza na wasafi. Hata huyo LOwassa na udhaifu wake lakini ni kiongozi makini na hakuna mpinzani anaemfikia , huu ni ukweli.
Unajua tatizo kubwa la vyama vya upinzani ni ubinafsi, miaka 23 ya vyama vingi sura zile zile na wanashindwa kujenga taasisi zao kuwaandaa vijana kuwa viongozi ,
Viongozi wa kuzuka tu ni kama sungura wa majaribio...bado mapema kuwapa nchi....kama makosa yapo ni ya adminstration iliopo akija mwengine atakuja na staili ingine
 
Kama unaamini kuwa tatizo ni uongozi uliopo sasa basi kama kweli hicho chama kinataka kurudia historia yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na sio chama cha wafanyabiashara; mtu anayeweza kuwarudisha huko ni PHILLIP MANGULLA baada ya Kikwete kufunga virago vyake!!
 
muengue lowassa ktk mbio ushuhudie ushindi WA kishiindo wa UKAWA!/

ukishindana na nguvu za mungu Juu ya mteule wake / what's the next / hasira za mungu zikoje?/ CCM ndio itakayotuletea machafuko baada ya uchaguzi kuisha / reason ni /// ITASHINDWA KUKABIDHI MADARAKA! huu no utabiri tu wangu binafsi/ thanks
 
Kama unaamini kuwa tatizo ni uongozi uliopo sasa basi kama kweli hicho chama kinataka kurudia historia yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na sio chama cha wafanyabiashara; mtu anayeweza kuwarudisha huko ni PHILLIP MANGULLA baada ya Kikwete kufunga virago vyake!!

Huyo Mangula ndo nani ? KIPI cha ajabu alifanya ? Kinana ni shupavu sana amemfunika hata huyo Mangula.
Tangu lini ccm ikawa chama cha wakulima ? Porojo za mitaani tu.
Hivi bado mna ndoto za siasa korea kaskazini ? Za zidumu fikra ?
Ccm inajua nyakati japo iko slow kubadilika. Hatuhitaji kurudi kwenye ukomonisti
Siasa na uingozi wa nchi uko wazi kwa yeyote mwenye uwezo awe mkukima mfanya biashara au mfanya kazi. Vivo hivyo kwenye ubunge.
 
Ukiwa na haraka huwezi kumjua Philipo Mangula.soma historia ya viongozi waadilifu na wachapa kazi hodari
 
Huyo Mangula ndo nani ? KIPI cha ajabu alifanya ? Kinana ni shupavu sana amemfunika hata huyo Mangula.
Tangu lini ccm ikawa chama cha wakulima ? Porojo za mitaani tu.
Hivi bado mna ndoto za siasa korea kaskazini ? Za zidumu fikra ?
Ccm inajua nyakati japo iko slow kubadilika. Hatuhitaji kurudi kwenye ukomonisti
Siasa na uingozi wa nchi uko wazi kwa yeyote mwenye uwezo awe mkukima mfanya biashara au mfanya kazi. Vivo hivyo kwenye ubunge.

Ukitaka kujua hasara ya kuchanganya siasa na wafanya biashara wewe chunguza michango humo bungeni ya wakina Mohamed Dewji mbunge wa Singida njiji na wenziwe; wapo humu kulinda maslahi yao ya kibiashara tu na sio kuwatetea wananchi, uchaguzi ukikaribia wanakwenda majimboni mwao kugawa vibaba vya unga na maharage basi wanakuwa tayari kuchaguliwa upya!!! Je hawa ndio wawakilishi wanaoweza kuwaletea wananchi maendeleo? Mangulla kwa bahati mbaya humfahamu, lakini kwa wanaomfahamu ni mwanachama mzalendo wa ccm ambae ni tegemeo lao kubwa kwa maamuzi magumu.
 
Hahaha michango ya vijembe
Huyo dewji amefanya mengi zaid jimboni kwake kuliko mbunge yoyote yule.
Leo unachagua waliga domo.
Bora watu wa vitendo.
Namfahamu sana mangula ulimshinda kutatua mgogoro wa znz mpaka ikabidi znz wenyewe waufanye utatuzi nje ya chama
 
Back
Top Bottom