WanaJF,
Mtu ambae alikuwa akijipambanua kuwa ni rafiki wa madereva boda boda, mama ntilie na wamachinga katika kipindi chake chote cha kuusaka urais tangu akiwa CCM, leo hii marafiki zake hao wamepatwa na balaa la kubomolewa makazi yao, hawana mahali pa kulala, lakini Lowassa yupo kimya kama hajui nini kinaendelea kwa watu hao, ambao kimsingi walimuunga mkono katika safari yake ya mabadiliko, na pia walimpa kura nyingi kwa nafasi aliyogombea ya urais.
Pamoja na hayo, Lowassa huyu huyu amekaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akiwa anatetea kundi la wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kodi ya serikali na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato. Bila ajizi, Lowassa aliwatetea wafanyabiashara hao kwa kauli yake iliyosema, "Naionya serikali iache kuwasumbua sumbua marafiki zangu wafanyabiashara kuhusu mambo ya kodi kodi."
Kwahiyo basi, Lowassa amepata muda na morali ya kutetea marafiki zake ambao ni wafanyabiashara wakubwa tena wakwepa kodi, lakini wale marafiki zake wengine/walalahoi (kama ambavyo amekuwa akituaminisha kuwa ni rafiki zake) suala lao la kubomolewa makazi sio tu ameshindwa kuwapa msaada hata wa debe la sembe, lakini ameshindwa hata kutoa pole kwa waathirika wa zoezi la bomoa bomoa.
Aidha, baadhi ya waathirika wa bomoa bomoa hawakusita kueleza masikitiko yao kutokana na kile walichodai kupuuzwa na viongozi wa CHADEMA taifa. Baadhi yao wamesema walijaribu kuwasiliana na Lowassa, Sumaye na Mbowe kuhusu namna walivyo athirika na bomoa bomoa inayoendelea, lakini matokeo yake simu zao zimekuwa hazipokelewi na viongozi hao wa CHADEMA wala jumbe zao za maneno (sms) hazijibiwi kwa takribani wiki tatu sasa tangu wameanza kuwatafuta.
Je Mbowe na Lowassa, hii ndio namna ya kushukuru watu walio kuungeni mkono katika kampeni zenu? Mlianza kuwasaliti Wapemba kwa kuwatosa viti maalum pamoja na kuwapa kura tele. Sasa imekuwa zamu ya Dar kusalitiwa!