sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,489
Lowassa asingekimbia CCM angekubali kumuunga mkono raisi wake na waziri mkuu wake kwa kujaza fomu ya maadili aorodheshe mali anazomiliki ama angegoma kama miaka mingine?
Ni lini Lowasa na Mbowe watajaza fomu za maadili na kutaja mali walizo nazo ndani ya chama chao? Kwanini utaratibu wa kuweka wazi mali ulizo nazo hauwalengi wapinzani? Upinzani utafsiriwe kama chaka la mafisadi na wezi kwamba hawana utaratibu wa kuweka wazi mali walizo nazo na wamezipataje?
Kwakuwa awamu hii ya tano ni ya uwazi, uwepo utaratibu wa kimaadili kila mwenye mali ajulikane chanzo cha mali alizo nazo na idadi ya mali alizo nazo.
Natamani kuona upinzani unakuwa mfano wa uadilifu na siyo ushabiki. Leo hii Masamaki akijiunga Chadema watampokea na kumsafisha. Huwezi kuuza kibanda cha pipi halafu umiliki ndege! Huwezi kuwa mchungaji halafu umiliki ndege, utakuwa unawaibia waumini kwa maneno matamu. Huwezi kuwa mwenyekiti wa chama halafu una mali nyingi na hutoi vielelezo kuwa unazipataje, pengine unatumia picha na kadi za wanachama kuwaombea misaada ya kuendesha chama halafu unazitaifisha.
Miaka nenda rudi zaidi ya 20 ya upinzani, wanaonufaika kwenye chama ni wale wale. Mashabiki wa chama hutumiwa kama mtaji wa kukipatia chama mapato ila yanaenda mfukoni kwa viongozi. Unatumikia chama miaka mingi huna chochote, huna nafasi ya kuuliza ama kuhoji chochote, upo upo tu kufuata maelekezo ya viongozi. Amkeni enyi wapiga tarumbeta, ngoja nijionee mlivyotekwa akili japo ni jambo la msingi nimelibainisha.