Lowassa na agenda ya umasikini

Lowassa na agenda ya umasikini

Naomba kujua Umaskini wa wanaMonduli ameshaumaliza????

Maana naona masai wenzake wanahangaika tu, kudhurura kila mahali na ng'ombe zao! maji wanachangia na ng'ombe!

Teamlowasa msitusababishie msiba usiokuwa wa lazima aisee!
 
Angekuwa na uchungu sana kutokomeza umaskini angeanzia jimboni kwake maana kule ndiko umaskini ulikokithili maana watu wake mamia kwa mamia wanakuja mjini kufanya kazi za kulinda mageti
Tusitake kudanganyana hapa hana dhamira ya kweli kutokomeza umaskini zaidi ya kutaka kutufirisi na hicho kidogo kinachopatikana yeye na genge lake la kihalifu la akina Chenge,Rostam na wengineo wengi tu
 
Hivi utuibie alafu utuambie hupendi umasikini? Ninaipenda nchi yangu na kwa imani ikulu hutokwenda.ulishindwa arumeru kwakutuletea mkweo sasa utashindwa nchi nzima kwa kutuletea list ya wizi wenzako Namalizia kwa kusema kwa matendo yako wewe ni KIRANJA WA MAFISADI TANZANIA
 
sina jingine zaidi ya kuamini umasikini wa watanzania, matatizo katika elimu na ajira ni wakati muafaka sasa kupata msukumo mkubwa katika utendaji na utatuzi wake. daima ukisema unatenda huwa hivyo tunakuamini na tupo wote katka safari ya matumaini. Mungu awe upande wako daima

Mungu awe upande wa fisadi! Mmh mshaurini akatubu kwanza, ili asamehewe.
 
Mm binafsi namkubali sana huyu mtu. ss kama lengo ni tupate viongozi masikini wa kupretend sijui kama tutafika. Maana wengi ni wale wanaotaka nchi iwafanyie jambo siyo wao wataifanyia nn nchi. Ss tumechoka na umaskini kama anakuja tena rais masikini tuendelee kushare umaskini kazi ipo. Lowasa ameshasema anauchukia umaskini sana so huyu ndo mtu wa kututoa hapa tulipo

Monduli kunanuka umasikini, miaka yote 30, kafanya nini? Hajaeleza mkakati wowote, anaimba tu kubabaisha watu wasiotafakari matamshi holela
 
Ukitaka kujua definition ya umaskini karabu monduli. Nzi mpaka midomoni hali mbaya sana jamani
 
Akina lowasa na wenzake ndiyo walikua wasisi wa kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania kauli hiyo haina tofauti na kuuchukia umaskini Leo hii kila mtu anajua maisha bora yalivyokua kinyume kwa msingi huo hakuna jipya atakaloweza kulifanya zaidi ya maisha kua magumu zaidi
 
LOWASSA NA AJENDA YA UMASKINI!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nitakuwa mnafiki na mchoyo wa fadhila kama sitokiri kuwa awamu zote za uongozi wa nchi yetu kuanzia Mwl Nyerere hadi Dr Kikwete kuwa wamefanya mengi, makubwa na mazuri katika kupambana na umaskini wa Tanzania.

Awamu zote ki ukweli zinahitaji sifa za kipekee katika jambo hili maana lazima tukubali kila zama na kitabu chake na waliotangulia wametimiza wajibu wao na sina budi kuwapongeza sana kwa niaba ya wote wapenda ukweli

Lakini haijawahi tokea tangu tupate uhuru mgombea wa chama chochote kuuzungumzia umaskini kama Lowassa anavyo uzungumzia


Lowassa kila anapopita anaweza kusahau kusalimia lakini haachi wala hasahau kuzungumzia umaskini wa Tanzania.

Wapo wagombee ambao wanapita kila mahala wakitoa kauli mbaya kwa wenzao lakini Lowassa kwake muda wa kuuzungumzia umaskini na nini atawafanyia watanzania akiwa jukwaani hautoshi.

Lowassa anatamani usiku na mchana azungumzie njia za kumaliza umaskini wa watanzania.


KAZI NZURI ALIZOZIFANYA MONDULI KAMA MBUNGE ZINA SADIFU HAYA ANAYO YAONGEA LEO.

Lowassa watanzania wamechoka na umaskini, na ajenda yako ya kuuchukia umaskini ina wagusa watanzania wa rika zote.


Mungu akubariki baba tupo tayari kwa mchaka mchaka.

Tumegundua kuwa chuki, fitina, wivu na majungu ndivyo vilivyotufikisha hapa tulipo na hatupo tayari tena kusikiliza wanao abudu mambo hayo.
Hebu tuambie Monduli umasikini umeisha? Kafanya nini Monduli katika miaka yake zaidi ya 30 akiwa mbunge? Kama kashindwa kumaliza umasikini Monduli kijiwila kidogo kwa zaidi ya miaka 30 ataumalizaje umasikini wa watanzania milioni 45 kwa miaka kumi?
 
Hebu tuambie Monduli umasikini umeisha? Kafanya nini Monduli katika miaka yake zaidi ya 30 akiwa mbunge? Kama kashindwa kumaliza umasikini Monduli kijiwila kidogo kwa zaidi ya miaka 30 ataumalizaje umasikini wa watanzania milioni 45 kwa miaka kumi?

Usanii mwingine haufai. Mnatakana kuwafanya watanzania wote wajinga
 
Back
Top Bottom