Lowassa na agenda ya umasikini

Lowassa na agenda ya umasikini

IamPrince George

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
412
Reaction score
168
LOWASSA NA AJENDA YA UMASKINI!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nitakuwa mnafiki na mchoyo wa fadhila kama sitokiri kuwa awamu zote za uongozi wa nchi yetu kuanzia Mwl Nyerere hadi Dr Kikwete kuwa wamefanya mengi, makubwa na mazuri katika kupambana na umaskini wa Tanzania.

Awamu zote ki ukweli zinahitaji sifa za kipekee katika jambo hili maana lazima tukubali kila zama na kitabu chake na waliotangulia wametimiza wajibu wao na sina budi kuwapongeza sana kwa niaba ya wote wapenda ukweli

Lakini haijawahi tokea tangu tupate uhuru mgombea wa chama chochote kuuzungumzia umaskini kama Lowassa anavyo uzungumzia


Lowassa kila anapopita anaweza kusahau kusalimia lakini haachi wala hasahau kuzungumzia umaskini wa Tanzania.

Wapo wagombee ambao wanapita kila mahala wakitoa kauli mbaya kwa wenzao lakini Lowassa kwake muda wa kuuzungumzia umaskini na nini atawafanyia watanzania akiwa jukwaani hautoshi.

Lowassa anatamani usiku na mchana azungumzie njia za kumaliza umaskini wa watanzania.


KAZI NZURI ALIZOZIFANYA MONDULI KAMA MBUNGE ZINA SADIFU HAYA ANAYO YAONGEA LEO.

Lowassa watanzania wamechoka na umaskini, na ajenda yako ya kuuchukia umaskini ina wagusa watanzania wa rika zote.


Mungu akubariki baba tupo tayari kwa mchaka mchaka.

Tumegundua kuwa chuki, fitina, wivu na majungu ndivyo vilivyotufikisha hapa tulipo na hatupo tayari tena kusikiliza wanao abudu mambo hayo.
 
Mi binafisi sitomsahau mpaka naingia kaburini baada ya kutuletea maji katika jimbo letu la kahama.
 
Mm binafsi namkubali sana huyu mtu. ss kama lengo ni tupate viongozi masikini wa kupretend sijui kama tutafika. Maana wengi ni wale wanaotaka nchi iwafanyie jambo siyo wao wataifanyia nn nchi. Ss tumechoka na umaskini kama anakuja tena rais masikini tuendelee kushare umaskini kazi ipo. Lowasa ameshasema anauchukia umaskini sana so huyu ndo mtu wa kututoa hapa tulipo
 
Yaani mimi issue ya elimu tu!! Hata mtoto wamkulima alijisemea wazi tunamshukuru Edward kwakusimamia vyema shule za kata zikajengwaa haraka maana mkoa wangu wa iringa ulikua unaongoza kwakutoa mabeck tatu! Beee sasa hivii hawaji kufanya kazi ng’oooo wote wanaenda shuleeee najua shule zakata zinachangamoto ila naamini akipata nafasi tenaa atamalizia alipoishiaaa!! Vivaaa Lowassa tegemeo la watqnzania na elimu yetu inayoyumbayumba!! Mungu ibariki Tanzania Mungu mbaliki Lowassa! Ameni
 
Hilo ni Jembe ole wao wakate jina lake wata tubu tupo pamoja mzee wetu
 
Hatuwezi kuwa na rais mwizi - refer report ya bunge ya uchunguzi wa richmond
 
sina jingine zaidi ya kuamini umasikini wa watanzania, matatizo katika elimu na ajira ni wakati muafaka sasa kupata msukumo mkubwa katika utendaji na utatuzi wake. daima ukisema unatenda huwa hivyo tunakuamini na tupo wote katka safari ya matumaini. Mungu awe upande wako daima
 
Hatuwezi kuwa na rais mwizi - refer report ya bunge ya uchunguzi wa richmond

Ukiweza kuithibitishia umma wizi wake utakuwa umefanya jambo la busara, lakini kueneza chuki nakuona kama mkaanga sumu, polee, LOWASSA anawaumiza kichwa sana Mwaka huu
 
Ulitaka akwambie kuwa ataleta umasikini ndio uamini kuwa Lowassa atakuibia siku atakapofani kiwa kuingia Ikulu?kwani Lowassa ni mjinga lazima akwambie maneno matamumatamu ili umchague,utakapo mchagua ndipo atakapo kunjua makucha yake ambayo utashindwa kuyakata kwa kuwa tayari yuko kwenye himaya yake.
 
Hatuwezi kuwa na rais mwizi - refer report ya bunge ya uchunguzi wa richmond

Jitahidi uwe unakuja na story mpya hizo zilipendwa.hakuna wa kumzuiya lowassa kwenda ikulu labda Mungu wake tu,na alipangalo Mungu hakuna wakuzuiya
 
Mpwa mi natamani kujua miradi ya kuondoa umasikini katika jimbo hilo. . . .

Mkuu nikipata majibu yenye kuridhisha ya swali lako na lile nililouliza pale awali itakuwa vyema...

Labda wenye kufahamu watatoa majibu...
 
Hakuna takwimu za kuelezea ambition zinazoonekana, kuliwahi kuwa na mafuriko kusini namba gani alicheza hata alikowahi fanya kazi wenye kujua ukweli waseme, imekuwa jembe jembe na taifa star jembe
 
Jitahidi uwe unakuja na story mpya hizo zilipendwa.hakuna wa kumzuiya lowassa kwenda ikulu labda Mungu wake tu,na alipangalo Mungu hakuna wakuzuiya

Hizo ngonjera tu, ikulu sio pango LA wezi na watoa rushwa
 
Mkuu nikipata majibu yenye kuridhisha ya swali lako na lile nililouliza pale awali itakuwa vyema...

Labda wenye kufahamu watatoa majibu...

Ngoja nimualike kaka Pasco huwa ana taarifa za huyu mtangaza nia. . . . .labda anaweza kutukwamua hapa
 
Last edited by a moderator:
Ukiweza kuithibitishia umma wizi wake utakuwa umefanya jambo la busara, lakini kueneza chuki nakuona kama mkaanga sumu, polee, LOWASSA anawaumiza kichwa sana Mwaka huu

Wizi wake ulithibitishwa bungeni ndio maana akaachia ngazi.hatuhitaji wezi na mafisadi ktk ikulu yetu.Tunamtaka rais. atakayepambana na ufisadi na rushwa
 
nilimkubali pale aliposema waziri mkuu wa Uingereza aliambiwa ataje mambo matatu atakayoyapa kipaumbele akasema education!education!education lowassa anataka watu wke wapate elimu..pambana laigwanan
 
Back
Top Bottom