Lowassa, Msabaha hapatoshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Msabaha hapatoshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Ni katika sakata la Richmond
  Kila mmoja apanga kujinasua


  Na Saed Kubenea
  MwanaHALISI

  HATMA ya Edward Lowassa kujinasua kwenye kashfa ya mkataba tata wa kampuni ya Richmond, ipo mikononi mwa Dk. Ibrahim Msabaha, MwanaHALISI limeelezwa.

  Dk. Msabaha ametajwa kuwa mwenye taarifa juu ya kila hatua na tukio katika kukamilisha mkataba wa Richmond; kampuni ambayo ilipewa tenda ya kuzalisha umeme huku ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi.
  Taarifa za ndani zilizopatikana wiki moja baada ya gazeti hili kufichua mpango wa Lowassa kutumia mkutano wa sasa wa Bunge kujisafisha na ikibidi kumhusisha hata Rais Jakaya Kikwete, zinasema "mwokozi au mwangamizaji wa Lowassa ni Dk. Msabaha."

  "Ndiye mwenye uamuzi. Lazima wamshike kama mboni ya jicho. Aweza kuamua kumuopoa au kumtosa. Itategemea uhusiano wao wa sasa," ameeleza mtu wa karibu wa Lowassa.

  Mjadala juu ya kampuni ya Richmond Development Company (LLC), unatarajiwa kufanywa wiki ijayo mara baada ya serikali kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya bunge.
  Dk. Msabaha, waziri wa zamani wa nishati na madini aliyejiuzulu nafasi yake kutokana na kashfa ya Richmond, ni mtu muhimu pia hata kwa upande wa serikali.

  Aidha, mawasiliano ya siri miongoni mwa watendaji wa serikali ambayo yamevujishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini, tayari yamewaweka Lowassa na Msabaha katika hali ya "urafiki wa mashaka."
  Wakati Lowassa alimwitaji Msabaha kuficha kila alichokijua juu ya mkataba, upande wa serikali ambao unatishiwa kuingizwa kwenye kashfa, unataka aiokoe kwenye sakata hili.

  Tayari taarifa zimeonyesha jinsi Msabaha alivyokuwa "mesenja" kati ya waziri mkuu, wizara yake ya nishati, Shirika la Umeme (Tanesco) na bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo.

  Nyaraka zipatazo saba ambazo zimewekwa saini na Msabaha, zinaonyesha kitu kimoja; kwamba alikuwa anaagizwa na Lowassa na anasisitiza msimamo wa "waziri mkuu" bila kutetereka.
  Kwa mfano, katika barua ya 12 Aprili 2006 yenye Kumb. CDB 88/286/01 kuhusu mashine za kukodi, Msabaha anaelekeza kwa Balozi Fulgence Kazaura, mwenyekiti wa bodi ya Tanesco kufuata maamuzi ya waziri mkuu.

  "…Pasiwe tena na picha kama vile menejementi ya Tanesco imerejeshewa kazi hiyo, maana huko kutakuwa kukiuka maagizo ya mheshimiwa waziri mkuu," anaandika Msabaha.
  Alikuwa akionya juu ya kuingiliwa kwa Kamati ya waziri mkuu iliyoteuliwa kushughulikia suala la Richmond na kueleza kuwa yote yanapaswa kufanywa "kwa kadri Kamati inavyoona inafaa."

  Kamati ya waziri mkuu ya kushughulikia suala la mashine za umeme za Richmond ilihusisha katibu mkuu wa hazina; katibu mkuu wizara ya nishati na Madini na mwanasheria mkuu wa serikali.

  "Nadhani hatukuelewana vizuri," anaandika Msabaha na kuongeza akimwandikia Kazaura, "Suala la kushughulikia gas turbines za kukodisha lilishashughulikiwa na mheshimiwa waziri mkuu." Yeye aliliona kama "baba mkwe."
  Imedhihirika kuwa kuanzia pale ilipoanza kunong'onwa kuwa Richmond yaweza kuwa bomu, Msabaha alianza kupeleka nakala za mawasiliano yake kwa rais.


  Haikufahamika mara moja rais alikuwa anatoa maoni gani juu ya kile alichokuwa akipelekewa taarifa juu yake.
  Hata hivyo, Rais Kikwete akijibu swali na mwananchi kwa njia ya televisheni, miezi miwili iliyopita, alisema alizuia waziri wake kulipa Richmond kwa kuwa "inaweza kuwa kampuni ya mfukoni."
  Taarifa zinasema ni kwa uzito huu wa Msabaha, kambi ya Lowassa imekuwa ikimpigia magoti ili asiweze kutoa siri ya jinsi Lowassa alivyoshiriki katika mkataba huo.

  "Nakuambia, kina Lowassa wanahaha ili kumzuia Msabaha asizungumze. Maana Msabaha anajua kila kitu na hivyo siku akiamua kutoka hadharani, itabidi Lowassa afiche sura yake," kimesema chanzo cha habari ndani ya serikali.

  Mjadala juu ya Msabaha kuokoa au kuzamisha Lowassa pale (Lowassa) atakapoibuka kujitetea, umekuja mwaka mmoja tangu mbunge huyo wa Kibaha Mjini atishie kuweka hadharani kile kinachoitwa, "Siri ya Richmond."
  Taarifa za Msabaha kutishia kuanika kilichotendeka zilisikika kwa mara ya kwanza wiki moja baada ya Lowassa kukana kuhusika na mkataba wa Richmond.
  Kanusho la Lowassa lilitolewa jimboni kwake, Monduli mkoani Arusha, wiki moja baada ya kujizulu nafasi ya waziri mkuu. Alinukuliwa akisema ameponzwa na Msabaha na watendaji wengine serikalini.

  "Kama siyo busara za mmoja wao katika kambi ya Lowassa; kuingilia kati na kumtuliza Msabaha, angekuwa amelipuka zamani," ameeleza mtoa habari.
  Taarifa za ndani ya serikali zinadai hata kuondolewa kwa Msabaha katika wizara ya nishati na madini, na nafasi yake kuchukuliwa na Nazir Karamagi, kulitokana na tabia yake hasa alipoanza kutilia mashaka mkataba wa Richmond.

  Hata hivyo, nyaraka mbalimbali ambazo MwanaHALISI imeona, zinaonyesha kazi yote ya kusimamia, kuidhinisha na kupitisha mkataba wa Richmond ilifanywa chini ya uangalizi wa waziri mkuu.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kile kinachoelezwa kuwa tahadhari ya Lowassa juu ya mkataba huo, kinavunjwa na barua iliyoandikwa na Lowassa mwenyewe.

  Wakati Lowassa anamwandikia Msabaha ajiridhishe kuwa Richmond itaweza kutekeleza kazi zake, tayari kampuni hiyo ilikuwa imepewa mkataba.
  Katika barua hiyo ya 21 Septemba 2006, waziri mkuu anaonyesha kumpa Msabaha kazi nje ya ofisi ya serikali kwa kumtaka "kufuatilia kwa karibu" ili kuhakikisha walioomba mkataba na wakapewa kwa nguvu ya serikali, wanaingiza mitambo ya umeme nchini.

  Mkataba kati ya serikali na Richmond ulisainiwa 23 Juni 2006, wakati barua ya Lowassa iliandikwa miezi mitatu baadaye.
  Kwa kipindi chote cha kusubiri mashine za umeme, mawaziri wa nishati, Msabaha na Karamagi walifanya kazi kama ya "maofisa uhusiano" wa Richmond, kwa kuisemea hata ilipokuwa haina la kujitetea kuhusu kuchelewa kuzalisha umeme.

  "Barua hii ya Lowassa ni feki. Aliiandika wakati tayari serikali imeshafunga mkataba na Richmond na baada ya kuona mambo yameanza kuharibika," ameeleza waziri anayejua vema mkondo wa mkataba wa Richmond.

  Amesema Msabaha anayajua yote haya na kuongeza, "Mtafute akueleze." Msabaha hakuweza kupatikana kwa simu yake ya mkononi. Iliita bila kupokelewa.

  Madai kwamba Lowassa alikuwa akipeleka taarifa kwa rais kwa kila hatua, haikuweza kuthibitishwa, kwani hata barua ya kutaka Msabaha achukue tahadhari, ambayo uhalali wake unatiliwa mashaka, haikunakiliwa kwa rais.

  Hata hivyo, barua ya Lowassa imejaa kila aina ya utata, kuanzia tarehe iliyoandikwa, mahali ilipoandikwa na ilipopatikana.
  Wakati andishi hilo linaonekana lilitoka Dodoma, S.L.P. 981, lilipokelewa hukohuko Dodoma kupitia Fax Na. +255 026 2331955.

  Uthibitisho mwingine wa nafasi ya Lowassa katika sakata la Richmond ni barua ya Msabaha ya 13 Julai 2006 ambayo inamsisitiza katibu mkuu wa wizara ya nisahati na madini "kuheshimu maagizo ya waziri mkuu" Lowassa.

  Lakini kuzagaa kwa taarifa hizi mpya na kuwapo kwa taarifa kwamba Msabaha anaweza kuibukia bungeni ili "kuanika ukweli," kunaweza kuvuruga kabisa mipango yake.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Kitu ambacho huwa sipati picha je, ni nini lengo la mwandishi?

  1. Msabaha afike bungeni na hii taarifa iwe classified
  2. Msabaha asitimize lengo lake? maana kama habari imevuja, serikali watafanya kila iwezavyo ili wao wasiwe pabaya.
  3. Au ni kuuza gazeti kwa taarifa yeyote ile hata kama hiyo taarifa hana tija kwa taifa?

  Naamini kna taarifa kama kweli kuna watu ni wapinga ufisadi hawatakiwi kuzianika kwa lengo la kutovuruga mipango, lengo zuri la hao watu!


  ''Nakuambia, kina Lowassa wanahaha ili kumzuia Msabaha asizungumze. Maana Msabaha anajua kila kitu na hivyo siku akiamua kutoka hadharani, itabidi Lowassa afiche sura yake," kimesema chanzo cha habari ndani ya serikali''

  ''Lakini kuzagaa kwa taarifa hizi mpya na kuwapo kwa taarifa kwamba Msabaha anaweza kuibukia bungeni ili "kuanika ukweli," kunaweza kuvuruga kabisa mipango yake''


  Je baada ya taarifa hii kuandikwa gazetini Msabaha atafanya anavyotaka??

  My take ni mbona taarifa serious kama hizi zinakosa seriousness ya kuwa investigative news, na zinageuka kama udaku fuani vile

  Ni maoni tu, siyo mwandhi wa habari lakini sijajua lengo ni kuuza gazeti, Kukwepesha jambo fulani au sijajua bado labda wachunguzi wanaweza kunisaidia

  I submit
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Lengo la mwandishi ni kuwafamisha Watanzania (Wasomaji wao) chochote kile wachokifahamu kinachoendelea kuhusiana na sakata hili la Richmond.
   
 4. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #4
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Saeed Kubenea, my friend ambaye I have a lot of respect kwake na ujasiri wake wa kusimama na kuhesabiwa, ila sometimes na yeye huwa anapitiwa, au ndio biashara yenyewe sijui,

  - I mean, serikali yetu sasa hivi ina ushahidi tosha wa kuwashika wale wote waliohusika na Richimond, infact bunge limeidhinisha hatua kali za kuchukuliwa kwa kuwataja majina wale wote waliohusika, leo anakuja kutuambia eti Msabaha ndiye mwenye ukweli, ukweli upi tena huo?

  - Tizama, kule US Mr. Kerik alitaka kuwa waziri wa Homeland Security, akatuma CV yake kwa ofisi ya rais, ambapo hakusema ukweli ofisi ya rais ilipogundua kuwa hakuwa mkweli, ikamuweka pembeni na kumtosa, lakini FBI automatically wakaingilia kati na kutaka kujua ukweli aliouficha wakagundua kwamba ana matatizo ya kushirkiana na Mafia, wao hawakusubiri bunge lichunguze, au katibu wa rais amuandikie katibu wa bunge, au kuanza kuwapigia simu Kerik na Mafia, wao walichofanya ni kumburuza Kerik mara moja kwenye sheria kwa kuidanganya ofisi ya rais wa US, Full Stop.

  - Ndugu zangu hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa kwenye utawala unaoheshimu sheria, Takukuru walitakiwa kuwa wameshawaburuza wote waliotajwa kuhusika na Richmond pale tu ripoti ya kamati ya bunge ilipopitishwa na bunge, lakini kwa sababu ni Banana Republic tizama tulipo na hii ishu, mara Hosea amesema hawana makosa, mara kikao cha NEC kimewasafisha, mara kuna habari zingine hazikutolewa kuinusuru serikali, mara sasa Msabaha ndiye ana ukweli wote, foolishness!

  Hivi hili taifa tumelogwa na nani? wakati hizi ishu zingine ziko so open huhitaji hata kuwa mwanasheria au mwanasiasa kuzielewa, kwamba hawa mafisadi wanazidi kutuchezea akili tu!

  Ahsanteni.

  William.
   
 5. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0

  Zile tetesi za kukamatishwa milioni 80 zinaweza kuwa kweli!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  CCM na serikali yake wameoza basi hakuna jingine....
   
 7. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkulu Billy,

  Hawa mafisadi wako juu ya sheria na wana uwezo wa kufanya lolote na kokote. Nchi ni mali yao na sisi wengine ni wageni na watumwa ndani ya nchi yetu. NINI KIFANYIKE?
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  jibu lako lipo kwenye hiyo pupple
   
 9. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  nani kapewa milioni 80.
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Itabidi nilifanyie kazi sana hili, ili kujua uwezo na uafanyaji kazi wa vyombo vya habari ni kupasha habari yoyote tu, au vinaweza vikawa chachu ya mabadiliko muhimu sana.

  Kama kweli hili gazeti linataka mambo yawe 'uchi' nafikiri wangeibana hii taarifa hili Msabaha aanike 'huo ukweli' ambao ungesaidia sana.

  Otherwise I am getting confused, SUPPOSE kesho Msabaha akakanusha!
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wala usipipoteze your precious time on this, nobody is taking Kubenea serious including so called "wapiganaji". Jamaa na mjanja wa fulani wa mjini anaeganga njaa kwa ku terrorise viongozi apate ujira wake.

  Huwezi kukuta utumbo kama huo kwenye gazeti makini kama Mwananchi. Kubenea kwenye Mwanahalisi yeye ni kila kitu editor, reporter, msambazaji, accountant, dereva etc. Yote hayo from form four failure!
   
 12. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  mkuu bwana kubenea ana watu makini kama wakili mabere marando ndio mshauri wake kisheria.
  Ulipoainisha kazi zake basi tumuite robot.
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Last time I checked, advocate Marando ana run law firm yake mwenyewe. Kumtetea Kubenenea mahakamani haina maana kuwa ni muajiriwa wake niliyo list hapo juu ni kazi za Mwanahalisi kama gazeti.

  Kwa mwendo huo una maana Kubenea akienda kutibiwa muhimbli na Dr xxx huyo nae ni mwajiriwa wake?

  U can do better than this....
   
 14. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  mkuu naona umejaa jazba ngoja nikuache.au ndio wewe mliosema kuwa kubenea anaandikiwa story.
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kubenea na wewe umezidi bwana...kila mara kutuweka roho juu then hakuna kinachotokea...personally iam getting tired of you...
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  bana huyu Kubenea anabore sasa..I dont trust him anymore...
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jazba ipo wapi hapo? wewe vipi unakuwa kama sio mjinga!
   
 18. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  haya maswala ya mafisadi kusema kweli sasa tumechoka kusikia kwani yanazidi kutia uchungu kwa vile hakuna mtu yoyote anayechukuliwa hatua.watu wana kila ushahidi lakini wanawaogopa wahusika.urafiki kwenye mali ya umma ni kitu kibaya sana.
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Masatu punguza uongo ndugu yangu ... kama hizo kazi zote anazifanya yeye, wakati ule alipoenda India Gazeti la MwanaHalisi nalo lilienda India?

  Hayo majina ya waandishi wa habari ambayo yanawekwa kwenye Gazeti la MwanaHalisi ina maana ni ya kubuni?

  Ndimara Tegambwage alipomwagiwa tindikali alikuwa wapi na anafanya nini? Alipohojiwa alisema yeye ni mshauri wa kuhariri habari za gazeti la MwanaHalisi.

  Tatizo lako ni kwamba mapenzi yako kwa CCM na kwa watu fulani ndani ya CCM yamekufanya uwe kipofu na kiziwi. Ikiguswa CCM kidogo tu tayari unakuja na hoja zisizo na mashiko, zimejaa uzushi na uongo.

  Wakati ule Sitta anakaangwa na NEC kule Dodoma ulishangilia sana, yalipoanza kurushwa mawe baada ya NEC ukawa kimya kabisa. Wewe, Makamba akina Chiligati hamna tofauti kabisa, agenda yenu ni kutetea mafisadi kwa nguvu zote.

  Baada ya kikao cha NEC wenzako (Makamba, Chiligati + all pro ufisadi) walitoka wanashangilia, mawe yalipoanza kurushwa wakakaa kimya, mara mjomba wako Makamba akaenda Urambo kujikomba kwa kuwa alishajua kwamba alichemsha. Chiligati alikaa kimya wala hakutaka kuongelea tena kwa mbwembwe swala la maamuzi ya NEC.

  Last time ulidanganya hapa kwamba JKT ilikuwepo mpaka zama za Mkapa, wakati hakuna ukweli wowote na wewe mwenyewe ukasema kwamba ulienda JKT zama za Mkapa, uongo mkubwa! Nilikuomba uthibitishe ukaingia mitini. Tuache kupakaza.

  Je, unataka na leo tuamini huo uongo wako kwamba Kubenea ni kila kitu? Kwamba ni mwandishi, mhariri, msambazi, dereva, mhasibu, etc?

  Kaazi kweli kweli!
   
 20. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kwani mimi ni kijana wa chadema hadi niwe Mjinga.kwa mujibu wa Kibanda vijana wa Chadema wanaomsapoti Zitto ndio wajinga.Mzee nikuache naona leo umeniamkia mimi,naona Nimron anachelewa kukujengeeni chuo kikuu labda mtapunguza Jazba.
   
Loading...