Lowassa, Meghji, Airo hoi bungeni

Lowassa, Meghji, Airo hoi bungeni

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426


Na Mwandishi wetu

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, Zakia Meghji (mbunge wa kuteuliwa) na Lameck Airo (CCM) ni miongoni mwa wabunge ambao wamechangia na kuuliza maswali machache bungeni tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bunge, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) ndiye anashikilia rekodi ya ukinara wa kuchangia akifuatiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) na Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki (CCM).

Utafiti huo ambao hauhusishi takwimu za mkutano wa Novemba haukuwajumuisha mawaziri, manaibu wao, Spika, naibu wake, wenyeviti watatu wa Bunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile nafasi zao zinawapa uwezekano mkubwa wa kuchangia hoja wakati wowote.

Katika rekodi hiyo, Mnyika ambaye hiki ni kipindi chake cha kwanza bungeni, amechangia mara 184, kuuliza maswali ya nyongeza 28 na ya msingi 7, Zitto amechangia 79, maswali ya nyongeza 25 na maswali ya msingi 8, huku Zambi akiwa amechangia mara 70, maswali ya nyongeza 26 na ya msingi 9.

Kulingana na takwimu hizo, wabunge kumi waliochangia na kuuliza maswali mara chache ni Mwanakhamis Said Kassim (CCM), ambaye rekodi inaonesha hajawahi kuuliza swali la msingi wala nyongeza isipokuwa amechangia mara mbili tu.

Anayefuata ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu mwaka 2008, Lowassa ambaye vile vile hajawahi kuuliza swali la msingi wala nyongeza bali kachangia hoja mara mbili.

Katika kundi hilo wamo Mbunge wa Rorya, Airo aliyechangia mara tatu, maswali ya msingi matatu, wakati Muhammed Amour Chombo (CCM) hajawahi kuuliza swali bali amechangia mara nne.

Muhammed Seif Khatib (CCM), hajawahi kuuliza swali bali amechangia mara tatu huku Ali Haji Juma (CCM), ameuliza swali moja la msingi, moja la nyongeza na kuchangia mara nne.

Wamo pia Anna Maulida Komu (CHADEMA) na Shwawana Bukhati Hassan (CCM) ambao wamechangia mara tano bila kuuliza maswali wakati Meghji akiwa amechangia mara tisa bila kuuliza swali.

Rekodi hiyo pia inawaonesha Dk. Abdulla Juma Saadalla (CCM), Said Suleiman Said (CUF) na Salim Hassan Turky (CCM) waliochangia mara saba, na kuuliza swali la nyongeza moja.

Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM), ndiye anafunga orodha hiyo akiwa amechangia mara tano na kuuliza swali moja la msingi na moja la nyongeza.

Katika kumi bora ya wabunge waliochangia mara nyingi, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) anashika nafasi ya nne akiwa amechangia mara 93, ameuliza maswali ya nyongeza 19 na msingi 7, akifuatiwa na Diana Chilolo wa Viti Maalumu (CCM) aliyechangia mara 61, maswali ya nyongeza 41 na msingi 9.

Nafasi ya sita inashikiliwa na Halima Mdee wa Kawe (CHADEMA) akiwa na amechangia mara 59, maswali ya nyongeza 15 na ya msingi 6 akifuatiwa na Moses Machali wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi) mwenye michango 57, nyongeza 30 na maswali ya msingi 7.

Chritowaja Mtinda (CHADEMA) amechangia mara 53 na kuuliza maswali ya msingi 12 na nyongeza 19 akifuatiwa na Magdalena Sakaya (CUF) aliyechangia mara 52, maswali ya nyongeza 13 na ya msingi 4.

Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo (CCM) alifuatia kwa michango 51, maswali ya nyongeza 10 na ya msingi 6.


Source: Tanzaniadaima newspaper
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!
 
Airo anajulikana ni kilaza hata kwenye kampeni alijinasibu hivyo
 
Sasa waseme nini kama hawana cha kusema.
Simple:
Ama ni kutokana na uwezo mdogo wa kuchambua yanayoendelea Bungeni au anakuwa hana cha kupinga Mafisadi au kuwashambulia mafisadi endapo yeye naye ni mmoja wao au ni wakala wao!
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!

Mjinga wewe kazi ya mbunge iko bungeni, kutunga sheria, kujadili na kupisha bajati, kuwakilisha wananchi, na kuisimamia serikali, haya yote unayafanya ukiwa ndani bunge sessions kwa zaidi ya asilimia 90 kazi ya kutekeleza sera na mipango ya maendeleo ni ya serikali maana ndo yenye bajeti! Kwahiyo mbunge akiwa bubu bungeni inamaana hatekelezi wajibu wake!
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!

Zubeda you sound so cheap! samahani lakini; nipe kiwango chako cha elimu na jina la chuo ulichosoma if any. Samahani lkn!
 
Mjinga wewe kazi ya mbunge iko bungeni, kutunga sheria, kujadili na kupisha bajati, kuwakilisha wananchi, na kuisimamia serikali, haya yote unayafanya ukiwa ndani bunge sessions kwa zaidi ya asilimia 90 kazi ya kutekeleza sera na mipango ya maendeleo ni ya serikali maana ndo yenye bajeti! Kwahiyo mbunge akiwa bubu bungeni inamaana hatekelezi wajibu wake! Msameheni Zubeda

NI WAKATI WA KUWA NA MAGAVANA ili watanzania wajue tofauti ya Mbunge na Mtawala, mtu atakwambia hata Mbunge wake akiwa bubu ni sawa ili mradi maendeleo analeta, maendeleo anapata wapi hela naye siyo mtawala kama hajanunuliwa mahali, Mbunge ndo mana akaitwa Mbunge lazma achangie bungeni kwa bidii zote, kweli watz bado Vilaza wengi,
 
Rorya tuna tatizo la kukosa mbunge 2010 - 2015! Lakini tume ya taifa ya UCHAKACHUAJI (NEC) haijatangaza uchaguzi mdogo. Kwa hiyo nawaasa wanarorya wenzangu kuwa tuvumilie mpaka 2015 tutakapompata mbunge bora na siyo bora mbunge.
 
1. kukiwa na ufisad na mapungufu na matatzo nchin kiwango hik halaf huna hata cha kuchangia bungen iko namna. 2. heko mnyika, zito na zambi kwa michango iliyoenda shule 3. sio rahis mbunge akawa mchangiaj mzur bungen halafu akawa 0 jimbon
 
Mnyika he so active.........anastahili kuwa kinara.
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!

ulichokiandika na jina lako vimebalance! Usichukie lakini, jina lako (zubeda) linasound kitaarabtaarab vile...!!
 
Yaani katika purukushani za migomo ya walimu na wafanyakazi,harakati za kuandika katiba mpya,mfumuko wa bei, Wanavyuo wanaokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo, usafirishaji haramu wa nyara za serikali, mafuriko ya jangwani, wizi kwenye nguzo za umeme, polisi kutumia nguvu kubwa kutekeleza sheria, kuongezeka kwa vyakula, dawa na bidhaa feki sokoni,

Mgogoro wa Tanzania Vs Malawi, benki kuwa na riba kubwa isiyowanufaisha masikini, miundombinu hovyo vijijini,mabadiliko ya hali ya hewa, usiri katika mikataba ya madini n.k

Ukiona mbunge wako ana machache ya kuihoji serikali kati ya makubwa niliyoyataja hapo juu, basi ujue pengine ni mgonjwa kama Mwandosya, au ulimchagua kwa kuwa alikuhonga kanga/t-shirt au kofia au alipita kwa kuchakachua!
 
yah ni kwli si lazima uchangi tusimshambulie mwenetu kiasi hiki wajameni
 
Waropokaji bungeni wako wengi kama akina Anne Kilango! Hawana madhara! Watu wasioongea kama akina Lowassa wakiongea neno moja lina impact kubwa!
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!
je, utasaidiaje kama hutatoa kilio chako bungeni?
au ndio kwa kubeba mabegi ya mawaziri
 
Sio lazima uropoke ropoke ovyo bungeni hoja ni jee, unasaidiaje kuleta maendeleo jimboni mwako?
Kuna Wabunge wengine hutafuta umaarufu kwa kuandikwa andikwa kila siku magazetini!

ndo maaana ukaitwa Zubeda
 
Back
Top Bottom