Lowassa kwa maono ya Le Mutuz!!!

CCM imewekwa na wananchi wanaoipenda na haijiweki yenyewe.
Na sisi tulio wengi tunafaidika na CCM Kuwa madarakani.
Ninyi wachache endeleeni kuishabikia Ukawa ili mushindwe.
Kwa demokrasia iliyopo ni wengi wape.

Lowassa hajachoka kuwa CCM ila ana uchu wa madaraka na ninyi ndio ngazi ya ndoto yake ya urais.
Hana mchoko wala uchungu, na kujidai vinginevyo ni kujidanganya nafsi yo bure!
 

Usiwatishe vijana, hapo hakuna fact yoyote. Wewe unataka watu wote wawe na mtazamo mmoja? haiwezekani, lazima katika maisha ya kidemokrasia watu wawe na mitazamo tofauti. Naunga mkono maana mitazamo tofauti miongoni mwa wanajamii huleta majibu sahihi kwa changamoto zinakabili jamii husika.
 
Kwamba Bashe ndiye kipimo cha akili za akina Le Mutuz, kweli? This is too low to grasp.
 
Mzee Mwinyi aliposema Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu hakukosea!

Jinsi wingi wa "big up" "Salute" "Habari ndio hiyo" na sifa kibao kwa kunyonyeshwa "FACTS" tena kutoka kwa wengi ambao mnajiita Great THinkers, si kuwa kunanisononesha kuwa kuna ujinga wa hali ya juu, Bali kunanionyesha kuna upumbavu wa hali ya juu na watu wengi wanahitaji kupewa Udaktari wa Falsafa ya UPUMBAVU!

Fact 1. Wabunge wa CCM walioanguka kura ya maoni ni chini ya 50
Fact 2. Wabunge wa CCM walioamua kutorudi kwa hiari ni chini ya 20
Fact 3. Hakuna masjala au usajili wowote unaoonyesha ni mbunge gani wa Lowassa na yupi si wa Lowassa. Ama hakuna anayejua waliojulikana kuwa ni wapambe wa Lowassa wamebakia kwa makusudi ndani na hata kushinda kura za maoni (Serukamba, Bashee) na si lazima wakimbilie UKawa
Fact 4. Wenyeviti wa CCM walioondoka CCM, si wote walitaka kugombea ubunge au kuwa walitaka madaraka ya Ubunge
Fact 5. KUsindikizwa na watu, wadhamini au wenyeviti wa mikoa hakuna maana wote watahama kwa mkupuo mara mmoja. Je haitakuwa FACT kuwa wamebakizwa ndani ya chama kwa malengo ya kuhujumu CCM au kuibana CCM isitumie goli la mkono (Majasusi, including Nchimbi, KImbisa na Sopha)?
Fact 6. Si kweli wabunge 150 wa bunge lililopita la CCM wameangushwa au eti ni watu wa Lowassa

NI upumbavu wa hali ya juu kuamini kauli za mtu mmoja ambazo ni wazi zina mwelekeo wa mipasho au worse kabisa udaku na zikafanywa kuwa ni habari za uhakika.

Ni udhaifu huu wa kujituma na kufikiri unawafanya watu washangilie "mafanikio" ya Takwimu za Magufuli kudai Kikwete amejenga barabara urefu wa Kilometa 17,000 na vibarua ni wachina, huku barabara zilizokamilika hazifiki Kilometa 7,000 na hao "Vibarua" Wachina ndio waliotoa mkopo wa kujenga barabara na wanaleta watu wao kujenga hizo barabara!

Sitashangaa hili kundi la WAPUMBAVU wa kufikiri watakapoamua kushangilia ----- unaoitwa FACT na hata kukubaliana na kila kinachosemwa bila kukaa chini na kutafakari kama kinachosemwa kina mantiki au kuna ukweli. Ni kundi hili hili la wavivu wa kufikiri siku ya kupiga kura watapiga kura za kufuata mkumbo badala ya kura ya uamuzi wao wa kupima wagombea.

Hao wanaotoa FACT wanawaona wapokea FACT na washangiliaji wa FACT kama mabozo na majuha na ndio maana Tanzania tumeendelea kuburuzwa na Watanzania wenzetu wanaotudharau na kutupuuza kisa tunashangilia FACT.

Basi tuwape nao shadaha za Udaktari wa Hamnazo kama yule anayekusanya Shahada kila kona ya dunia!
 

Mag3,

Uselule umezidi kwa Watanzania! Kila mtu anapenda kuhadithiwa kijiweni na kumshangilia "stelingi" wa maneno..!phew!
 
Mkuu wapumbavu wako wengi, na wewe huna tofauti sana na hao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…