Lowassa kumshtaki Kikwete

Lowassa kumshtaki Kikwete

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,624
Reaction score
930
Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”

Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake binafsi.

“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na kiongozi huyo.

Hakuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.

Chanzo:Mwanahalisi Online
 
Yap, mawazo ya mtu hayapingwi ni vyema ukafikisha ujumbe mkuu
 
Maji yameshamwagika hayazoleki. Abakie kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu, na apiganie haki na mabadiliko akiwa ndani ya chama.
 
Kilichotokea Dodoma si kinajulikana kuwa alikatwa kwa kuonewa,sasa anatueleza nini? Tunataka atueleze uozo uliopo CCM sio kilichotokea CCM.Upinzani wasipokuwa makini watakaribisha garasa
 
Taabu yake ni kuwa Edo mwenyewe ni muoga mno wa kusema ukweli na hilo limemgharimu mno. Hata kueleza kile kilichojiri kwenye Richmond anapata kigugumizi na kushindwa kufunguka mpaka leo, Naamini hana mpya ya kutupasha,
 
Kila siku mnasema atasema sijui atasema lini daah hii ishakua kero sasa
 
Yeye amejuaje kwamba alikuwa ndiye mawazo ya wengi? Wengi hao ni wangapi kati ya wangapi ambao ni wachache?
 
Awahi kwa mafisadi wenzake huko kaskazini, sisi tunakwenda na Maghufuli.
 
Maji yameshamwagika hayazoleki. Abakie kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu, na apiganie haki na mabadiliko akiwa ndani ya chama.
Siyo Lowassa tena, Rostam analiendesha Robot, elekea huku linakwenda, simama, linatii. Ni shiida.
 
mbona wote hawa wanapiga kodi zetu kwa kuachiana zamu...

nani atakubali aharibu maslahi ya mwezake!
 
Kama maamuzi magumu aliyokuwa akithubiria ndio yangekuwa yanapigiwa danadana hivi, hana tofauti na Mk*ere, tofauti mikwara tu.
 
hahaha ameshindwa kuzuia mafuriko kwa mikono.hahaha sidhan kama itamsaidia anapaswa kutulia
 
Maji yameshamwagika hayazoleki. Abakie kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu, na apiganie haki na mabadiliko akiwa ndani ya chama.
Mafuriko yameshazuiwa wa mkono, na Edo ndio kesha tinga CHADEMA.
Sasa Nape anatayarisha makombora akisha kusikia ndogo ndogo zitakazorushwa na Edo wa piiiipoz!
 
Back
Top Bottom