assadsyria3
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 6,909
- 4,057
Wakati akiongea na vyombo vya habari, Lowassa amesema aliondoka CCM na kujiunga na CHADEMA kwa sababu ya kusakamwa kwa maneno ya kejeli, vijembe na vitisho na kuitwa gamba na fisadi.
Wacha weeKilichomwondoA CCM sio kuitwa gamba.Aliitwa Gamba sana tu akiwa CCM hakuondoka.Kilichomwondoa CCM ni baada ya Jina lake Kukwatwa asiwe mgombea Uraisi CCM.Mzee Lowasa kweli anapoteza kumbukumbu.Akawadanganye CHADEMA.PANGA LA KUMKATA LILIPOPITA NDIO AKATIMKA MKUKU KUKIMBILIA CHADEMA.Lowasa wanasema hawezi kukimbia hana mbio lakini lilipokatwa jina CCM mbio alizokimbia kwenda CHADEMA sijawahi ona.Angeweza pata hata medali ya OLYIMPIC
Lowassa anashangaza sana!Lowasa Mwongo.
KilichomwondoA CCM sio kuitwa gamba.Aliitwa Gamba sana tu akiwa CCM hakuondoka.Kilichomwondoa CCM ni baada ya Jina lake Kukwatwa asiwe mgombea Uraisi CCM.Mzee Lowasa kweli anapoteza kumbukumbu.Akawadanganye CHADEMA.PANGA LA KUMKATA LILIPOPITA NDIO AKATIMKA MKUKU KUKIMBILIA CHADEMA.Lowasa wanasema hawezi kukimbia hana mbio lakini lilipokatwa jina CCM mbio alizokimbia kwenda CHADEMA sijawahi ona.Angeweza pata hata medali ya OLYIMPIC
Huyu Mzee analazimisha uongo!Atawadanganya hao hao wajinga,
Jina lake lisingekatwa angeondoka CCM???
Huyu mzee anajipa moyo tu ila kiukweli kishapoteza dira.
Na kama aliamini manadiliko hayawezi kuletwa na CCM nini kilikuwa kinamfanya atafute nafasi ya urais kupitia CCM? kama alikuwa mwana mabadiliko maana yake ni kwamba angetoka mapema CCM kabla ya mchakato, na hayo mabadiliko alokuwa anasema ni yapi wakati yy ndo bingwa wa mafisadi. ni kweli manyumbu ni wengi na ataendelea kuwadanganya sana.Lowassa bado anaendelea na usanii wake. Anajaribu kudanganya kwa nguvu!
Kusema aliondoka CCM kwa sababu ya kuitwa fisadi na gamba ni kuwafanya watanzania kama wajinga!
Lowassa aliondoka CCM kwa sababu jina lake lilikatwa na kama lisingekatwa, leo hii angekuwa bado ni mwanachama hai wa CCM.
Hata hivyo nimpongeze Lowassa kwa kuwa na vision ambayo inachagizwa na fani yake ya usanii.
Baada ya kukatwa jina lake ndani ya CCM na ndoto zake zake za kuwa Rais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM zikayeyuka. Aliamua kupiga ndege wawili kwa kutumia jiwe moja.
Kwanza, aliamua kujiunga CHADEMA ili wamsafishe na kulitua zigo la kuitwa fisadi ambalo wao wenyewe CHADEMA walimtwika kwa zaidi ya miaka minane.
Pili, Kwa kulishuka zigo ambalo walimtwika, aliwapa pia Viongozi wa CHADEMA kazi ya kumnadi kwa Watanzania ili wamchague kuwa Rais wa Tanzania.
Kazi hiyo ya kumsafisha mpaka sasa wanaendelea nayo!
kwahyo ccm iliwatuma wakina Lema, Nassar, Mbowe na Dr slaa bila kumsahau lisu ili wamtukane lowasa? Ama maana sielewiMagamba povu linawatoka ile mbaya! Kwani ni uongo hawakutumwa watu kumtukana Lowassa?