Lowassa: Kikwete Ameharibu Uchumi

CASTRO PEMBA

Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
85
Reaction score
50
Katika mkutano wa kihistoria, mh" rais mtarajiwa amesema JK ameharibu uchumi, watu weng wamekua maskini, bidhaa juu, hoi

 
Ni kweli kabisa, maisha ni magumu sana na mbaya zaidi yanazidi kuwa magumu..Kila kitu kiko juu, hakuna unafuu.
Ni wakati wetu sasa Watanzania kuitumia hii turufu kuchagua viongozi bora watakaotumia madaraka yao vyema.
#PamojaTutashinda
 
Huyo lowassa alikuwa wapi? Unafiki huu wa kiwazimu kweli, Halafu hana cha kusema ila tu ntawafanya Watanzania matajiri kwa njia ipi? Holaa hakuna anachojua zaidi ya ajira ni bomu na ntawafanya watz matajiri, nyumbu hata hawawazi utajiri huo utatoka wapi
 
Hivi wakati lowasa yupo PM kwenye senate walikua hawafuati ushauri wake?
 
Aliyoyasema yako wazi hayahitaji ushahidi, mpaka chumvi imepanda bei kwenye huu utawala dhalimu. Watakaobisha ni wale walioshiriki kutuharibia uchumi.

Liwike, lisiwike Lowassa all the way to the white house.
 
Ni kweli kabisa, maisha ni magumu sana na mbaya zaidi yanazidi kuwa magumu..Kila kitu kiko juu, hakuna unafuu.
Ni wakati wetu sasa Watanzania kuitumia hii turufu kuchagua viongozi bora watakaotumia madaraka yao vyema.
#PamojaTutashinda

Hapo kwenye blue bado ni shida mkuu
 
Lowassa kachoka sana, kwani tunamchagua JK ama tunamchagua JPM? alafu mbona yeye alikuwa ni mmoja wa watumishi katika serikali anayoilaumu? kama ilishindwa na yeye tunamhesabu ni mmoja wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…