Lowassa kesho ndani ya Azam Two

Lowassa kesho ndani ya Azam Two

Area 56

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,546
Reaction score
4,040
Aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa anatarajiwa kufanyiwa mahojiano na Tido Mhando katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Azam Two.

Lowassa anatarajiwa kutoa ya moyoni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, pamoja na mtazamo wake kuhusu hali ya kisiasa na uchumi inayoendelea kwa sasa hapa nchini.

Usikose kumsikiliza na kumuangalia live nguli huyu wa siasa kuanzia saa 3:00 asubuhi ya kesho Jumapili naamini ana mengi kwa sisi Watanzania.
61A301C5-3C1A-411F-A909-270FE75078AE_mw1024_s_n.jpg
 
Mtamuua Magufuli.
Anadhani baada ya Tamko lake la Jana, basi kila kitu kitakuwa shwari na watu watanyamaza. Ndio kwanza kawasha moto.

Halafu Magufuli anadai kuuza nyumba zote za umma, Dar Es Salaam. Ni lini Bunge lilikaa na kukubaliana azimio hilo la kuuza nyumba za umma?

Na ni kampuni zipi zimepata tenda ya Auction a.k.a kuendesha mnada? Na lini tenda imetangazwa?

Haya ni maamuzi ya Kichwani au Baraza la Mawaziri? Au ni mzuka wa kulazimisha matukio badala ya kubadili mfumo kisheria kikanuni na kitaratibu za nchi?
 
Back
Top Bottom