Lowassa avamia mikutano ya CHADEMA Monduli

Lowassa avamia mikutano ya CHADEMA Monduli

Acha uongo . Monduli Chadema haipo.
kweli umelowa, yaani uko ndembendembe, CHADEMA wamesimamisha wagombea wa serikali za mtaa pale Monduli sasa wewe unasemaje CHADEMA hawapo Monduli? Acha ushabiki wewe punguani, mbona mnakera kama jini? Yaani ccm ni lazima mukae mwaka huu, nyumbu nyie.
 
Katika hali ya kushangaza mbunge wa Monduli mh.Edward Lowassa ameingilia ratiba ya mikutano iliyopangwa kwa ajili ya kampeni za serikali za mitaa na kufanya mikutano ya chama chake maeneo ambayo CHADEMA ilipaswa ifanye mikutano.

Leo katika kijiji cha Losirwa kilichopo kata ya Eslalei vijana wa CHADEMA walishtushwa kuona CCM wakivamia na kuanza kufunga vyombo na vifaa vya kampeni kwenye eneo walilokuwa wakiliandaa kupigia kampeni kwa madai kwamba mbunge ndiye anayekuja kuhutubia huku wakijua fika kwamba ratiba haiwaruhusu.

Viongozi wa CHADEMA walipolifikisha suala hili kituo cha polisi Mto wa Mbu OCS wa kituo hicho alijaribu kuwasiliana na mtendaji wa kata na mtendaji wa kijiji ambao wote waligoma kutoa ushirikiano kwa madai kwamba wapo wilayani Monduli.Hata hivyo viongozi hao wa CHADEMA walishangazwa sana na kauli ya OCS huyo kwamba mbunge ana haki ya kufanya mikutano bila kujali ratiba.

Juzi pia mh. Lowassa aliingilia ratiba ya mkutano wa CHADEMA uliokuwa ufanyike Mto wa Mbu na hivyo CHADEMA kulazimika kutumia siku iliyofuata ambayo ilikuwa ndiyo ya CCM katika ratiba. Uongozi wa CHADEMA wilaya ya Monduli tayari umeshafikisha malalamiko katika ofisi ya mkuu wa wilaya leo kuonesha kutoridhishwa kwake na jinsi mbunge huyo anavyokandamiza demokrasia wilayani Monduli.

Mbunge huyo anahaha kukinusuru chama chake wilayani Monduli baada ya chama hicho kuzidiwa nguvu na CHADEMA wakati mbunge huyo alipokuwa nje ya nchi.

Wiki iliyopita pia uongozi wa CHADEMA wilaya ya Monduli uliiandikia ofisi ya mkuu wa wilaya barua inayoelezea njama na hujuma zinazopangwa juu ya viongozi na wagombea wa CHADEMA wakati huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kama anataka urais aache fujo za kitoto kwa kuwa zitamharibia sana. Yeye afanye mikutano ya kistaarabu kama anaweza vinginevyo ajue anajitafutia kuchafuliwa zaidi.
 
Chadema monduli? Hahahahah achen kutafuta maujiko hakuna anayeweza kusimama akaongea monduli zaidi ya lowasa
 
Sipati taswira nzur ktk sehem nying tz kuelekea 2015 general election, i can observe th criteria for th unfair election!
 
Ndiyo aina ya mtu ambaye watu wanashabikia awe rais wa nchi huyu ambaye hafuati utaratibu,mtemi,mbabe mwenye tabia za kidictator zinazoweza sababisha uvunjifu wa amani.Kama hawezi kufuata utaratibu mdogo tu huo uliowekwa na serikali ya chama chao chenyewe ana kila dalili ya kufanya vibaya zaidi ya hayo akipata madaraka makubwa zaidi.Kivyangu nashukuru Mungu sana kwa kuwa sijawahi kuona anafaa kuwa rais wa nchi pamoja na mshikaji wa Kikwete.
 
Hicho ni kiburi. Ata maandiko yanakataza. Huu ubabe ni kwa kuwa mhimili wa dola ameuweka mfukoni. Amesahau upo kwa kodi yetu. Tutammlilia mola atupe jinsi . yeye si mwisho
 
Chadema monduli? Hahahahah achen kutafuta maujiko hakuna anayeweza kusimama akaongea monduli zaidi ya lowasa

Bila shaka hii ndiyo post ya kimasikini na ya kichovu kupita zote kwa mwaka 2014 ! Very poor .
 
Bila shaka hii ndiyo post ya kimasikini na ya kichovu kupita zote kwa mwaka 2014 ! Very poor .

Poor ni ndugu zako walioko kijijini wakitegemea mvunje amani ya nchi yetu kwa madai mnatafuta haki,tunaitaji demokrasia ya kweli lakini chadema jipangeni tena sana!
 
Kweli unaijua vizuri ajabu hujagombea hata ubunge mwakani jaribu ukaungane na ashumta kabla hajatukabidhi Mali zetu
 
Poor ni ndugu zako walioko kijijini wakitegemea mvunje amani ya nchi yetu kwa madai mnatafuta haki,tunaitaji demokrasia ya kweli lakini chadema jipangeni tena sana!
Mapovu ni kielelezo cha kuelemewa na hoja .
 
Poor ni ndugu zako walioko kijijini wakitegemea mvunje amani ya nchi yetu kwa madai mnatafuta haki,tunaitaji demokrasia ya kweli lakini chadema jipangeni tena sana!

Kuvuruga ratiba ya kampeni iliyowekwa ndiyo demokrasia ya kweli? Huna tofauti na kuku
 
Back
Top Bottom